Tundu Lissu apinga vikali adhabu ya Mdee na Bulaya

Tundu Lissu apinga vikali adhabu ya Mdee na Bulaya

Kwikwikwi Lisu lini amewahi kushinda kesi yoyote!? Lisu ni mweupe sana.
Kwenye hili atatoka kapa. Mwanasheria gani huyo anaogopa kushitakiwa!?
Lissu aogope kushitakiwa? Labda wewe unaishi kwa Wagagagigikoko,Lissu anakesi zaidi ya 5 kafunguliwa na serikali ya awamu ya tano na anachomoa moja baada ya nyingine.
 
Siku hizi viongozi wa idara nying hapa nchi huwa wanatoa maamuzi ili mkulu hawasifie nahic na huyu ndugai ni mmoja wao

Ndungai mgonjwa jamani,maamuzi yake hayawezi kuwa sawa kwani anatumia dawa kali mno so mental he can't be stable.
 
Hakuna Bunge la hovyo kama hili la Ndugai na Tulia

Bunge utadhani ni NEC ya CCM!Bunge ukilinganisha na enzi za akina MSEKWA japo ilikuwa chama kimoja wabunge walikuwa wanauhuru mkubwa zaidi wa kuichachafya serikali na wakati mwingine ilibidi hata kufanyia marekebisho BAJETI zao za wizara husika.

Leo Wabunge wakipigwa mkwala kwenye Jengo lao hapo Dodoma wanalowa kama wamenyeshewa na mvua ya kiangazi,wamejikunyata kwa uoga utadhani vifaranga vilivyomwagiwa maji.

Wanakuwa hawana confidence kabisa ,sielewi kwanini wanagombea ubunge wakati wanashindwa kabisa kuwatetea watanzania,wanashindwa kabisa kuiwajibisha serikali,ukiwaangalia akina Lusinde,Keissy,Musukuma na yule Mtoto wa Celina Kombani,kwa uchache sioni chochote wanachochangia kumsaidia mtanzania ambaye ndiye aliyewaweka pale.

Sioni kama kweli Bunge ni lwa wananchi zaidi naona Bunge ni serikali.SIjui kama watanzania tunaelewa kwanini kuwe na Bunge,sidhani kama tunaelewa,tungekuewa tuanelewa sidhani kama tungekuta hoja za kumsifu Ndugai kupindisha sheria za Bunge kwa matakwa yake na chama chake.

Watanzania,tuamke sasa,wakati unakwenda asubuhi imefika,amkeni vijana naona huruma viongozi wa kesho watakuwaje.
 
Huyu spika nilikuwa namuheshimu sana sana, ila naona anataka kujiharibia yani nimemshangaa sana jinsi alivyomdhalilisha Mh. Mnyika then kutoa adhabu kwa waheshimiwa Bulaya na Mdee! binafsi bado namshangaa huyu baba yetu kichwa chake kimeingiliwa na nini jamani? Tumuombee, nadhani kuna kitu kikubwa sana kitakuwa kinamchanganya kichwa chake...
 
Wewe ni mweupe kichwani. Kwikwikwi. Mzee wenu wa CUF alisema anapeleka kesi kuhusu Zanzibar sasa kabakina na Kesi ya Lipumba tu. Mwambie Lisu wako ajaribu utaona matokeo yake. Spika na Jaji mkuu wapo katika level moja. Mbunge yeyote kwenda kumshitaki Spika ni kujinajisi mwenyewe maama yeye atashughulikiwa bungeni. Somo chukua hilo.
Kumbe wajivunia ukandamizaji! Bunge ni mhimili, lakini panapokuwa na kutofautiana ndani ya Bunge, haki hutafutwa mahakamani. Speaker hayuko juu sheria za nchi, na hana ufalme huo unaompa na anaotaka kujipa. Ukiyatazama mambo haya kwa jicho la haki, ushabiki ulonao utajifia.
 
Kweli mkuu,kauli ile ya ndungai eti waende popote na itakuwa mwanzo wa constitutional crisis ktk nchi sijaelewa kabisa
Kauli haikuhusu ndio maana hujaelewa za level yako huwa unazielewa haraka
 
Kwikwikwi Lisu lini amewahi kushinda kesi yoyote!? Lisu ni mweupe sana.
Kwenye hili atatoka kapa. Mwanasheria gani huyo anaogopa kushitakiwa!?
Kesi ipi mmewahi kimshitaki mkatoka washindi,wewe inaonekana ni mgeni hapa Tanzania.. rejea kesi mbalimbali ambazo amekua akiwaburuza.
 
Hivi ile issue ya wabunge wa Africa Mashariki mbona aliangukia pua!?.
Mwambie akafungue hiyo kesi. Ninakuhakikishia hao akina Bulaya na Mdee wanakosa ubunge. Hapo anaongea siasa tu. Mwambie apige hatua yoyote kishitaki. Maana hayo ni maamuzi ya bunge akiwamo yeye.

Hapo anabwabwaja tu.
Kuwa nasubira,wanatoka msibani anaanza kushughulikia hilo suala,rejea kesi ya Lijuakali
 
Tungemshangaa asingepinga. Ameumbwa ili apenge ukweli wowote.
Tunaomba uite press conference usapoti maamuzi ya Ndugai kisheria,acha kuandika hapa kishabiki bila kushirikisha ubongo.
 
Mbona mbunge anafukuzwa na wabunge kwa kukiuka kanuni za bunge!? Soma kanuni za bunge 74(5).
Fafanua hiyo kanuni au ilete hapa tuisome kama inahalalisha kilichofanywa kwa hao akina dada.
 
Hivi Lissu asingekuwepo bungeni hawa vilaza CCM bunge lingekuwa na hali gani? shame on them
Hivi Mh Lissu akijirekebisha kuwa mwungwana atakosa nini. Haoni aibu kubwatuka kila mara akidhani yeye ni bora zaidi kuliko mwingine.

Mstaarabu ni mtu mwenye hekima na busara ambazo hutawala mawazo ya mtu na kumpelekea kuchagua maneno na lugha ya kutumia, kwa nyakati mbalimbali kulingana na mahala na wahusika/walengwa.

Pia mtu makini, akiwamo mwanasheria, hajigambi hovyo hovyo kufungua kesi mahakamani. Ila huaandaa mashitaka kwa utulivu na umakini wa hali ya juu kwanza.

Mh Lissu amejionesha kutokuwa na subira, uvumilivu, umakini katika taaluma yake. Badala yake amekuwa mropokaji.

Mh Lissu hadi lini utabadilika urudishe heshima yako. Naamini unasoma mijadala ya JF na wanaokupamba humu ndani, hawakutendei haki. Nina amini pia, huko CHADEMA, viongozi wenzio wanakuvumilia tu.
 
Kwikwikwi Lisu lini amewahi kushinda kesi yoyote!? Lisu ni mweupe sana.
Kwenye hili atatoka kapa. Mwanasheria gani huyo anaogopa kushitakiwa!?
Labd ungesema aliwah kushindwa kesi gani ningekuelewa. Inaonesha ww umetoka kolomije jana
 
Kwikwikwi. Ngoja nikucheke tu. Maamuzi yameshatolewa sasa Lisu issue iko kwake aende aendako. Apeleke kesi mahakamani utaona nguvu ya spika. Hapo anabwatuka tu baada ya hapo atajifungia shimoni kama panya kasikia paka.
Huna chochote ukijuacho kuhusu sheria kama spika ambavyo hajui chochote kuhusu sheria,unatoaje adhabu inayozisdi hadi muda ambao mtuhumiwa asipohudhuria vikao sio mbunge..¿
 
Kwikwikwi. Unanichekesha sana ulivyo mweupe kichwani.
Mimi sina weledi wa sheria,nimekutaka uweke hapa hicho kifungu kwa mapana yake ili nikuonyeshe udhaifu wa maamuzi ya spika,wewe si unataka kuhalalisha alichoamua spika?
 
Back
Top Bottom