Tundu Antipas Lissu on BBC HARDtalk - 21 January 2019

Tundu Antipas Lissu on BBC HARDtalk - 21 January 2019

Hii yaweza kuwa habari mbaya mno kwa wale wote wanaomtakia mabaya Tundu Lissu , nimeona taarifa huko instargram kuhusu viewers wa hii BBC HARDTALK iliyotikisa dunia , hii iliyomhusu Lissu The Greatest , habari zinaeleza kwamba imeangaliwa na zaidi ya watu milion 320 .

Mwenye taarifa rasmi atuwekee hapa .

Mungu mbariki Tundu Lissu
Ndo maana kule Lumumba ni jambajamba mwanzo mwisho!
 
Jamani mnaojua hii lugha ilikuja na meli hebu tuwekeeni kwa namna hii
Steve: Bebe nkoi lisu..................?
Lissu: Umanile...............
Hii itatufanye tuchangie wengi sasa hivi mmetupatia kazi ya ku LIKE tu au tunavhangia kile tunawaza bila kujua yale mazungumzo sasa tena mmesema " mere allegation"
Yaaani hiiii bagosha kandamizeni kwa mpango huo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sawa kuna watu wanafeli tena zero kabisa na kiingeleza wanakijua kwelikweli wanaongea na kuandika kwa ufasaha kuliko aliepata A na B+ lakini kumbuka kiingeleza ni lugha tu, na hakuna chochote alichofanya pale Tundu Lissu.
Baadhi ya wabongo wanaona kaongea point sababu ya lugha ila ukimchukua mtu ambaye english ni lugha yake asilia, atakwambia mbona jamaa alikuwa anaongea kwa mihemko tu, hajaongea kitu.
 
Sawa kuna watu wanafeli tena zero kabisa na kiingeleza wanakijua kwelikweli wanaongea na kuandika kwa ufasaha kuliko aliepata A na B+ lakini kumbuka kiingeleza ni lugha tu, na hakuna chochote alichofanya pale Tundu Lissu.

Sioni uhusiano na nilichoongea boss. Kijipange urudi. Niachie akina Misuli na akina Philipo ndio wana akili nzuri, ww nenda kwa wendawazimu wenzio.
 
Ndugu zangu,

Kama wazungu wanatambua kuwa tuhuma za akina Tundu Lissu, Zitto Kabwe na wenzao kuwa ni za 'kutengeneza' basi wabadili mbinu.

kitendo cha waandishi wa media za kimataifa kuyaita madai ya Lissu kuwa ni ''base less allegations'' au ''inflamatory statement ni dhahiri wapo uchi.

Huenda Zitto Kabwe naye hajatupa mrejesho wa Mwenyekiti wa jumuiya za madola baada ya kuambiwa ''your allegations against Hon.Ndugai with respect to CAG are utter baseless''

Tuliwahi kusema hapa uongo haudumu na ndicho kilichotokea na zaidi umewaumbua watu mchana.

Ni dhahiri hata ule mpango wa akina Ngurumo kutafuta ''hadi ya ukimbizi'' Finland umeshindwa.

Tanzania yetu sote, tuipende,tuikumbatie.

Huyu ni yule wa buku7 pale lumumba opposite na jengo la gsm makao makuu ya silent ocean
 
Ungependa asemeJe ?!
Kuwa fair.
Hebu mpereke jamaa yako kama ata perform kuliko Lissu [emoji12][emoji3][emoji23][emoji1787][emoji1787]

Sent using Jamii Forums mobile app
Rais wetu his actions speak, hamna haja ya kwenda huko. Kama unabisha muulize Steve Suckur, alikiwa kamletea lissu na ushahidi wa approval uliofanywa na observer wa nje. Yeye lissu alienda na maneno ya mdomoni.
 
Tundu lissu yuko vzr kihoja,kiingereza chake hata mm nimeshangaa sana sikutegemea kwawel kama jamaa atatema ngeli nzuri kiasi hicho ....waTz wachache sana wanaongea kama yy!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi nimependa sana yale mahojiano , yalimvua mtu nishai, Tundu Lissu alibaki mtupu kabisa , alikuwa anamung'unya maneno mpaka basi na mara nyingi ameambiwa wewe ni mwanasheria si vizuri kuongea bila ushahidi.
Kwahiyo mnacho kataa ni kwamba hakupigwa risasi?
 
Muasisi wa Taifa la Tanzania , Mwl. Julius Nyerere aliwahi kusema kuwa tumuogope kama ukoma mtu anayetaka kwenda ikulu kwa gharama yeyote. Mtazamo huu wa Mwalimu juu ya watu wa namna hiyo unafikirisha sana na kufanya tutafakari sana na kujiuliza maswali yafuatayo: kama mtu ana ndoto ya kuwa rais, si ataipigania ndoto yake kwa namna yeyote ili aende ikulu kuwa rais? Je, mwalimu aliona nini mpaka kufikia kutoa kauli kama hiyo?

Nimetafakari na kuona kuwa maneno ya Mwalimu Nyerere yalikuwa sahihi ya kwamba tumuogope mtu wa namna hiyo kwa sababu kuna wengine wanapelekeshwa na tamaa ya kuwa Rais kuliko matarajio yao na hivyo kutumia kila njia kutimiza tamaa zao na si matarajio yao. Moja ya watu wenye Tamaa hiyo ni Tundu Lissu, tamaa hiyo inampeleka puta haswa hata kufikia hatua ya kuichafua nchi yake na Rais wake.

Kiukweli kwenye mahojiano aliyofanya kwenye kipindi cha BBC HARDTALK kimeonesha ni kwa namna gani Tundu Lissu akipelekeshwa na tamaa ya urais mpaka kufikia hatua ya kuichafua nchi yake na Rais wake. Ni mara nyingi katika kipindi hicho alikuwa akiulizwa kama ana ushahidi wa yale anayoyasema dhidi ya serikali yake kwa shutuma kama hizo na yeye kusema inafahamika hivyo kama jibu.

Ni aibu na fedheha kubwa sana kwa mtu kama Tundu Lissu ambaye ni msomi wa sheria kuishutumu serikali imehusika na hiki na kile kwa shutuma kubwa za kuhatarisha amani na usalama bila kuwa na ushahidi. Ni vile tu mwandishi hakusema ila angepata nafasi angemwelezea kuwa kwa kosa kama hilo la kuishutumu serikali bila ushahidi kwa hapa uingereza ni kosa kubwa sana na adhabu yake ni kubwa.

Mwandishi wa kipindi kile kasaidia kwa namna kubwa sana kuamsha hisia za watanzania kwa kufichua ubabaishaji wa Tundu Lissu kwa dunia na uhatari wa anayoyafanya kuwa yanaweza kuhatarisha amani na usalama wa nchi. Shutuma anazozipeleka kwa rais wetu ni kubwa na zinahitaji ushahidi wa kutosha kuzitoa kwa sababu zinasababisha wawekezaji na watalii kupungua kutokana na hali mbaya ya kiusalama na uvunjifu wa amani unaoratibiwa na serikali kama Tundu Lissu anavyotaka iwe .

Serikali kama mlinzi namba moja wa usalama na amani ya nchi na raia wake hauna sababu za kueleza sababu za kiusalama kisiasa hasa zile ambazo hawana kithibitisho kuwa zimesababishwa na nini. Katika suala la Tundu Lissu kuna nadharia nyingi juu ya kushambuliwa kwake hivyo Lissu kuishutumu serikali kufanya hivyo moja kwa moja ni kosa na hivyo wenye akili inabidi tujiulize ni kwa nini serikali tu?

Jibu ni kwamba, Tundu Lissu anapelekwa puta na mawazo ya kuwa Rais hivyo ameanza kujipanga taratibu kwa kujenga chuki kwa wananchi kuwa CCM ndio wahusika hivyo wanapata nguvu ya kufanya fujo pale CCM inapowashinda kwenye uchaguzi mkuu wakisaidiwa na wanaowatuma kufanya hivyo.

Tundu Lissu , Dunia nzima sasa inajua lengo lako si zuri kwa nchi yako na waandaaji wa BBC hardtalk wameona aibu kumuhoji mtu ambaye hana data wala ushahidi wa tuhuma anazozitoa kwa serikali ambazo kwao wenyewe wanajua kwa tuhuma kama zile kwa nchi kama uingereza ni makosa makubwa. Umeamua kuichafua nchi yako kwa kupelekwa puta na urais ambao huna hakika utapata ama laaa .

Ushauri

i. Tundu Lissu asinyamaziwe, kwa nguvu ile ile anayoitumia kuichafua nchi kwa shutuma za kuokoteza zisizo na ushahidi ni vyema serikali ikatumia nguvu hiyo hiyo kumjibu . Tundu Lissu ajibiwe kisiasa na kitaalamu.

ii. Tundu Lissu atakapo rudi Tanzania kuandaliwe mdahalo kati ya Tundu LIssu na mwanaCCM mmoja ,watumie jukwaa hilo kumjibu kwa sababu Tundu Lissu hajaichafua serikali katuchafua pia CCM kwa kuwa ndio tunaongoza serikali.

Hitimisho

Tundu Lissu anajiona anajua sana kwa sababu anaamini hakuna mwanaCCM mwenye uwezo wa kumjibu ila akijibiwa atanyamaza kimya. Kila mtanzania mwenye akili timamu anamjua Tundu Lissu anafanya anayoyafanya kwa sababu ya tamaa ya Urais na anatengeneza mazingira mapema ili kushindana na nguvu ya Lowassa ndani ya CHADEMA.

na Karlo Mwilapwa
Naona mapepo ya chuki karibia yatawatoka. Tundu Lissu chochea karama yako!
 
Ndugu zangu,

Kama wazungu wanatambua kuwa tuhuma za akina Tundu Lissu, Zitto Kabwe na wenzao kuwa ni za 'kutengeneza' basi wabadili mbinu.

kitendo cha waandishi wa media za kimataifa kuyaita madai ya Lissu kuwa ni ''base less allegations'' au ''inflamatory statement ni dhahiri wapo uchi.

Huenda Zitto Kabwe naye hajatupa mrejesho wa Mwenyekiti wa jumuiya za madola baada ya kuambiwa ''your allegations against Hon.Ndugai with respect to CAG are utter baseless''

Tuliwahi kusema hapa uongo haudumu na ndicho kilichotokea na zaidi umewaumbua watu mchana.

Ni dhahiri hata ule mpango wa akina Ngurumo kutafuta ''hadi ya ukimbizi'' Finland umeshindwa.

Tanzania yetu sote, tuipende,tuikumbatie.
Acha watape tape sisi tunasongabele na Magu mpaka 2025
 
Back
Top Bottom