Tundu Antipas Lissu on BBC HARDtalk - 21 January 2019

Tundu Antipas Lissu on BBC HARDtalk - 21 January 2019

Hivi hardtalk una uzoefu nazo ama ulivizia hii ya TL tu, mara kibao iwapo mgeni yuko upande wa kulia mtangazaji hukaa kushoto makusudi ili iwe hard talk.

SASA NYINYI MBUMBUMBU MZIUNGU WA RELI, comprehension ndio shida yaani hujui kitu unadakia kama kidaka tonge kwa maneno ya bi hindu.

WAZUNGU WANAJUA KULIKO UNAVYODHANI, na wanafanya kazi kujua zaidi


Ndugu zangu,

Kama wazungu wanatambua kuwa tuhuma za akina Tundu Lissu, Zitto Kabwe na wenzao kuwa ni za 'kutengeneza' basi wabadili mbinu.

kitendo cha waandishi wa media za kimataifa kuyaita madai ya Lissu kuwa ni ''base less allegations'' au ''inflamatory statement ni dhahiri wapo uchi.

Huenda Zitto Kabwe naye hajatupa mrejesho wa Mwenyekiti wa jumuiya za madola baada ya kuambiwa ''your allegations against Hon.Ndugai with respect to CAG are utter baseless''

Tuliwahi kusema hapa uongo haudumu na ndicho kilichotokea na zaidi umewaumbua watu mchana.

Ni dhahiri hata ule mpango wa akina Ngurumo kutafuta ''hadi ya ukimbizi'' Finland umeshindwa.

Tanzania yetu sote, tuipende,tuikumbatie.
 
dah kwa Lissu alitoa ushahidi? weka hapa jamvini
Yes, irudie tena kama unajua lugha. Steve ndio alikuwa anaelezea maovu ya serikali halafu anajifanya kumsukumia maswali Lissu ili afafanue vizuri maovu ya serikali, Lissu na mwandishi lao moja ila hukumwelewa.

Mzungu gani anayependa uminywaji wa haki za binadamu, watu kuuawa na kutekwa. Kumbuka wao walimwita ili dunia ijue kuhusu uovu wetu, ndio maana alikuwa anayaanzisha mambo.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yaani mzungu anageuka kuwa mtanzania mzalendo kuliko mtanzania anayehojiwa, anamwaga data halafu TL anaanza kazi nzito ya kujenga hoja!.

Mzungu mwaka 1884 Berlin alikuwa anaijua afrika kuliko muafrika anavyoijua, muafrika anahaingaika na moto wa vijiti mzungu tayari anao umeme na anajua afrika inaanzia wapi na inaishia wapi!

Yule mtangazaji wa BBC alikuwa anamchora TL kiaina, tangu alivyomkaribisha unaona kabisa anamtazama katika jicho la kumjua kwa undani.

Halafu mzungu alivyo nyoko, siku zote akikudharau huwa anaongea kwa kunyenyekea ili usimgundue kuwa anachokifahamu ni zaidi ya unachokifahamu.
 
Alitoa mbona,kwamba viroba vyenye miili ya watu inaokotwa kwenye fukwe za bahari na kwenye mitaro ya maji machafu.

Kwamba kuna watu waliuawa kibiti,mkuranga na maeneo mengine

Kwamba wapinzani kila kukicha wao wapo mahakamani kwa kusingiziwa Kesi

Kwamba wale watu ambao walidaiwa kuwa ni wezi wa madini na kamati ya wale maprofesa wazoefu waliotuambia kuwa kila m-tz atapata Noah moja, Mtukufu raisi aliwaita kuwa ni Wanaume na watalipa kifutajasho cha $300 million ambazo hazijalipwa Hadi leo

Kwamba biashara imekuwa ngumu Sana,wafanyabiashara wakubwa na wawekezaji wamefunga biashara zao kwa figisu za serikali hii

Na nyingine kibao. Kama hizi sio evidence kwako, naomba usi-quote comment yangu maana utakuwa hujitambui
Mkuu hao ndio BBC,wana uzoefu mkubwa wa maswala ya nchi zetu.
Lissu kabanwa atoe proof and not allegations.
Nimejifunza kitu,ni ngumu wazungu hasa waingereza kuwaletea ngonjera zetu bila kuwa na ushahidi uliotukuka.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yule sio tuu ni Mwandishi wa habari bali ni jasusi fulani wanataka mjibu maswali ambayo wao wana uhakika nayo ila mkiwathibitishia watayafanyia kazi inatakiwa uwe na akili sana kumuelewa yule jamaa angalia vipindi vyake vingine na pia kama umezoea kusikikiza maswali ya waandishi wa habari wanapooitwa Ikulu wanapindisha pindisha ili kutomkwaza aliewaita huyo huwezi kumuelewa kabisa...
 
Muasisi wa Taifa la Tanzania , Mwl. Julius Nyerere aliwahi kusema kuwa tumuogope kama ukoma mtu anayetaka kwenda ikulu kwa gharama yeyote. Mtazamo huu wa Mwalimu juu ya watu wa namna hiyo unafikirisha sana na kufanya tutafakari sana na kujiuliza maswali yafuatayo: kama mtu ana ndoto ya kuwa rais, si ataipigania ndoto yake kwa namna yeyote ili aende ikulu kuwa rais? Je, mwalimu aliona nini mpaka kufikia kutoa kauli kama hiyo?

Nimetafakari na kuona kuwa maneno ya Mwalimu Nyerere yalikuwa sahihi ya kwamba tumuogope mtu wa namna hiyo kwa sababu kuna wengine wanapelekeshwa na tamaa ya kuwa Rais kuliko matarajio yao na hivyo kutumia kila njia kutimiza tamaa zao na si matarajio yao. Moja ya watu wenye Tamaa hiyo ni Tundu Lissu, tamaa hiyo inampeleka puta haswa hata kufikia hatua ya kuichafua nchi yake na Rais wake.

Kiukweli kwenye mahojiano aliyofanya kwenye kipindi cha BBC HARDTALK kimeonesha ni kwa namna gani Tundu Lissu akipelekeshwa na tamaa ya urais mpaka kufikia hatua ya kuichafua nchi yake na Rais wake. Ni mara nyingi katika kipindi hicho alikuwa akiulizwa kama ana ushahidi wa yale anayoyasema dhidi ya serikali yake kwa shutuma kama hizo na yeye kusema inafahamika hivyo kama jibu.

Ni aibu na fedheha kubwa sana kwa mtu kama Tundu Lissu ambaye ni msomi wa sheria kuishutumu serikali imehusika na hiki na kile kwa shutuma kubwa za kuhatarisha amani na usalama bila kuwa na ushahidi. Ni vile tu mwandishi hakusema ila angepata nafasi angemwelezea kuwa kwa kosa kama hilo la kuishutumu serikali bila ushahidi kwa hapa uingereza ni kosa kubwa sana na adhabu yake ni kubwa.

Mwandishi wa kipindi kile kasaidia kwa namna kubwa sana kuamsha hisia za watanzania kwa kufichua ubabaishaji wa Tundu Lissu kwa dunia na uhatari wa anayoyafanya kuwa yanaweza kuhatarisha amani na usalama wa nchi. Shutuma anazozipeleka kwa rais wetu ni kubwa na zinahitaji ushahidi wa kutosha kuzitoa kwa sababu zinasababisha wawekezaji na watalii kupungua kutokana na hali mbaya ya kiusalama na uvunjifu wa amani unaoratibiwa na serikali kama Tundu Lissu anavyotaka iwe .

Serikali kama mlinzi namba moja wa usalama na amani ya nchi na raia wake hauna sababu za kueleza sababu za kiusalama kisiasa hasa zile ambazo hawana kithibitisho kuwa zimesababishwa na nini. Katika suala la Tundu Lissu kuna nadharia nyingi juu ya kushambuliwa kwake hivyo Lissu kuishutumu serikali kufanya hivyo moja kwa moja ni kosa na hivyo wenye akili inabidi tujiulize ni kwa nini serikali tu?

Jibu ni kwamba, Tundu Lissu anapelekwa puta na mawazo ya kuwa Rais hivyo ameanza kujipanga taratibu kwa kujenga chuki kwa wananchi kuwa CCM ndio wahusika hivyo wanapata nguvu ya kufanya fujo pale CCM inapowashinda kwenye uchaguzi mkuu wakisaidiwa na wanaowatuma kufanya hivyo.

Tundu Lissu , Dunia nzima sasa inajua lengo lako si zuri kwa nchi yako na waandaaji wa BBC hardtalk wameona aibu kumuhoji mtu ambaye hana data wala ushahidi wa tuhuma anazozitoa kwa serikali ambazo kwao wenyewe wanajua kwa tuhuma kama zile kwa nchi kama uingereza ni makosa makubwa. Umeamua kuichafua nchi yako kwa kupelekwa puta na urais ambao huna hakika utapata ama laaa .

Ushauri

i. Tundu Lissu asinyamaziwe, kwa nguvu ile ile anayoitumia kuichafua nchi kwa shutuma za kuokoteza zisizo na ushahidi ni vyema serikali ikatumia nguvu hiyo hiyo kumjibu . Tundu Lissu ajibiwe kisiasa na kitaalamu.

ii. Tundu Lissu atakapo rudi Tanzania kuandaliwe mdahalo kati ya Tundu LIssu na mwanaCCM mmoja ,watumie jukwaa hilo kumjibu kwa sababu Tundu Lissu hajaichafua serikali katuchafua pia CCM kwa kuwa ndio tunaongoza serikali.

Hitimisho

Tundu Lissu anajiona anajua sana kwa sababu anaamini hakuna mwanaCCM mwenye uwezo wa kumjibu ila akijibiwa atanyamaza kimya. Kila mtanzania mwenye akili timamu anamjua Tundu Lissu anafanya anayoyafanya kwa sababu ya tamaa ya Urais na anatengeneza mazingira mapema ili kushindana na nguvu ya Lowassa ndani ya CHADEMA.

na Karlo Mwilapwa
 
*LISSU ATAABIKA SANA, AISHIA KUAIBIKA LONDON, ABANWA VIKALI NA KUTOA MAPOVU*

_NA Mwamba wa Kaskazini_

Leo ndio msemo kuwa Kiingereza sio maarifa umethibitika.

Tundu Lissu ana uwezo wa kutosha tu kuongea Kiingereza lakini asubuhi ya kuamkia leo kukosa maarifa kujawa na umbea, uongo na uzushi na uzandiki dhidi ya nchi yake kumemtokea puani akifanya mahojiano na Kipindi cha Hard Talk cha BBC.

Sikiliza haya.

*1.Aonesha Chuki Binafsi Kwa Magufuli*

Kosa la kwanza ni kutojadili hoja bali mtu.Kila alipoulizwa aliishia kutaja jina la Magufuli hata asipohusika.

Mtangazaji mzungu akabaki anashangaa na kumbana kwa maswali zaidi akaishia kutoa macho maskini.

*2.Lissu Hakutegema*

Hakika hata mimi sikutegema kama yule mzungu angefanya utafiti kiasi kile na kuyajua mengi ya Tanzania kiasi cha Lissu mwanzoni tu kubabaika na kuanza kuzusha uongo.

*3. Jaribio la kumdanganya Mzungu lakwama*

Baada ya kuzoea kuandika viwaraka vyake na kuwapa akina Martin Malera wa Tanzania Daima au Ibrahim Yamola wa Mwananchi leo Tundu Lissu kakutana na mwanahabari wa level nyingine.

Akajikuta anakosa ushahidi...anaambiwa unalalamika kila siku Serikali imekushambulia, unaushahidi gani anasema niliona gari inanifuatafuata, mzungu akambana kwani gari ziko ngapi na mtu yeyote si anaweza kukufuatilia kwani umeshafanya kazi ngapi za kukuweka katika risk ikiwemo kuwa wakili, Lissu akajikuta anakiri kuwa ni kweli hana ushahidi wa moja kwa moja bali ushahidi wa mazingira.

Asante sana mzungu, huyu Bwana leo baada ya mbwembwe nyingi sasa kakiri hana ushahidi zaidi ya mazingira tu ambayo pia yanaweza kuonesha chama chake kinahusika au hata dereva wake.

*4.Akosa maarifa kwenye madini*

Maskini hapa ndio jamaa alitoa mimacho tu baada ya mzungu kumbana kuwa yeye alipigania sana masuala ya nchi kufaidika na madini haoni kuwa JPM anachukua hatua nzuri?

Kwa hakika na mimi hapa nilipoteza Kiingereza changu[emoji3][emoji3]Sikumbuki hata Lissu alikuwa anajibu nini, aliishia maskini kutaabika na kuruka ruka huku na kule.Mzungu akaona isiwe shida, akahamisha mada!

Kwa kifupi hapa Lissu alijikuta anatamani kumpinga Magufuli, lakini pia akawaza anampinga kwa lipi?Kurekebisha mikataba ili nchi ifaidike? Akabaki anataja taja tu majina mara uwanja wa ndege Chato wakati nchi nzima vjwanja zaidi ya 15 vinajengwa[emoji3][emoji3]

*5.Mtangazaji aamua kutaja mwenyewe mazuri ya Tanzania.*

Baada ya kuona Lissu hana analolikubali katika nchi yake mzungu wa watu akaamua kutaja mwenyewe mageuzi makubwa yanayoendelea Tanzania.

Akataja mapambano dhidi ya rushwa, akataja kuongezeka kwa mapato akataja kutekelezwa kwa miradi mbalimbali ya kijamii na miundombinu.

Usiniulize wakati wote huu mzungu anashusha nondo Lissu alikuwa kwenye hali gani[emoji3][emoji3]Kumbuka mwenyewe kisa cha chura aliyebanwa na mlango[emoji3]


*6. Atoa mfano wa kitoto, wamuumbua*

Akieleza kwa nini wapinzani wenzake wamekuwa wakirejea CCM kuunga mkono juhudi za JPM Lissu aliishia kirusha matuhuma ambayo hadi mtangazaji akamuonya aache kuropoka bil ushahidi.


Lakini yotrme hii ni kwamba alishachanganyikiwa. Sasa sikia hii: akapewa mfano wa Masha aliyetoka CCM na kwenda upinzani (ingawa badae alirudi CCM) kama naye alihongwa huko upinzani? Usiniulize Lissu alikuwa katika hali gani hapa tena[emoji3]

*7.Akata fahamu, aunga mkono ushoga*

Akiwa hoi bin taaban na kisaikolojia akionekana mtu anayetamani mahojiano yaishe tu, Lissu akaulizwa ukiwa kiongozi wa upinzani na siku ukiingia Ikulu utafuta sheria zinazoelezwa kuwa kandamizi zinazoufanya ushoga kuwa kosa la jinai?

Maskini, mwisho wa zama ukatimia, baba la watu likajikanyagaaaa mwishowe likaingia kingi eti litafuta sheria zote zinazozuia ushoga nchini.Maweeeee[emoji17]

Rasmi Lissu kaunga mkono ushoga. Hakika ametaabika sana.

Kwa nini utaabike lakini?

Sent using Jamii Forums mobile app
Mzungu kiboko, kamtajia Lawrence Masha na cheo chake enzi za JK!.

Aliyemtuma TL aende BBC alimdanganya vibaya sana. Muingereza mwaka jana katupatia paundi milioni 300 kwa sababu tu ya kupambana vyema na rushwa.

Ilibidi ajipange kweli.
 
true ...hawako pamoja Lissu na wapambe wake.....
Unaelewa maana ya HARD TALK???? Ni hivi They will never, once again Never side with you

All hawataki kukuweka kwenye comfort zone

Ukiona wamekuita kwenye HARD TALK they know you can do it

Lissu did it! Salute you comrade

Huyu mnayemtetea hana kifua cha kukabiliana na haya ndio maana inaitwa HARD TALK -
Language/English (fluent) Confidence Intelligence ndio vigezo vya kuitwa kwenye kiti kile cha Enzi


They will always side na kile unachopingana nacho for you to prove 'your believes/standings'

Msiwe mnasikiliza kama kasuku unless leo kwako ni mara ya kwanza kushuhudia HARD TALK
Wanachotaka ni uanike mapungufu yote ya mtawala na chama chake as much as possible

Nikusaidie kidogo sikiliza HARD TALK za viongozi wa nchi ya Marekani akina Obama Bush Trump ndio uje uandike huu upupu wako.
 
Wapinzani haohao wakakimbia na dereva Hadi Nairobi, wakamtoa Hapo hadi kutibiwa kisaikolojia na Mwisho wakaamua kumsomesha.

Nokia ya kitochi yuzingi jamii foramu
Wapinzani hao hao wakang'oa cctv,wapinzani haohao wakashirikiana na policccm kufuta jarada la uchunguzi?
 
Lissu alikosa kuwa na matayarisho ya kujibu maswali ya Hard Talk
Alitakiwa ajibu kigentleman bila kuonyesha majibu ya uhasama, ila alijikita kwa kupinga kila kitu cha Magufuli akaonekana yupo biased na kuwaambiwa yeye kama mwanasheria alitakiwa aweka proof and not allegations.
Vile vile lugha haikuwa upande wake wa kujinadi.
 
Ndugu zangu,

Kama wazungu wanatambua kuwa tuhuma za akina Tundu Lissu, Zitto Kabwe na wenzao kuwa ni za 'kutengeneza' basi wabadili mbinu.

kitendo cha waandishi wa media za kimataifa kuyaita madai ya Lissu kuwa ni ''base less allegations'' au ''inflamatory statement ni dhahiri wapo uchi.

Huenda Zitto Kabwe naye hajatupa mrejesho wa Mwenyekiti wa jumuiya za madola baada ya kuambiwa ''your allegations against Hon.Ndugai with respect to CAG are utter baseless''

Tuliwahi kusema hapa uongo haudumu na ndicho kilichotokea na zaidi umewaumbua watu mchana.

Ni dhahiri hata ule mpango wa akina Ngurumo kutafuta ''hadi ya ukimbizi'' Finland umeshindwa.

Tanzania yetu sote, tuipende,tuikumbatie.
Tumechoka kusoma vitu visivyokuwa na uzito kama huwezi kuandika kwa nini ujionyeshe ujinga wako hapa. Tumechoka kusoma ujinga huu
 
Wapinzani hao hao wakang'oa cctv,wapinzani haohao wakashirikiana na policccm kufuta jarada la uchunguzi?
Na wapinzani haohao wakakimbia na dereva Hadi Nairobi na Mwisho wakaamua kumpeleka ubeligiji kutibiwa kisaikolojia na kumsomesha

Nokia ya kitochi yuzingi jamii foramu
 
Ndugu zangu,

Kama wazungu wanatambua kuwa tuhuma za akina Tundu Lissu, Zitto Kabwe na wenzao kuwa ni za 'kutengeneza' basi wabadili mbinu.

kitendo cha waandishi wa media za kimataifa kuyaita madai ya Lissu kuwa ni ''base less allegations'' au ''inflamatory statement ni dhahiri wapo uchi.

Huenda Zitto Kabwe naye hajatupa mrejesho wa Mwenyekiti wa jumuiya za madola baada ya kuambiwa ''your allegations against Hon.Ndugai with respect to CAG are utter baseless''

Tuliwahi kusema hapa uongo haudumu na ndicho kilichotokea na zaidi umewaumbua watu mchana.

Ni dhahiri hata ule mpango wa akina Ngurumo kutafuta ''hadi ya ukimbizi'' Finland umeshindwa.

Tanzania yetu sote, tuipende,tuikumbatie.
Anyway nilikuwa sitaki kukujibu maana nilisha weka msimamo kuwa watu fulani just ignore them. Ngoja nijibu kidogo.
Kama umesikiliza kwa weledi, mtu ambaye ana elimu ya sheria kidogo atagundua kuwa Stephen Sucker alikuwa anamuuliza leading questions which are not allowed in examination -in-chief au direct examination! You cause your witness to give answers you want! basi ndicho kilichofanyika leo! kama huelewi tafuta Lumumba mwenzako akueleweshe.
Threfore today's mission is highly accomplished.... to expose the evils of 5th dictatorial regime! Chakaza Salary Slip
 
Back
Top Bottom