Tundu Antipas Lissu on BBC HARDtalk - 21 January 2019

Tundu Antipas Lissu on BBC HARDtalk - 21 January 2019

Kwa nn tumpe public attention hivi? he is fact less, yaani pamoja na kuwa mbobezi wa sheria bado anathamini hisia zake binafsi kuliko facts zenye ushahidi?
Sasa sijui ataenda na marekani? sijui ataongea hivihivi pia..hahahaha
::sasa nataman achukue interview na Mzalendo Shaka wa VOA atambomoa bomoa..
:::::: ya lissu imekwisha sasa, tugeukie siasa zenye tija.
Viva Magufuli Viva Makonda Viva wazalendo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Muasisi wa Taifa la Tanzania , Mwl. Julius Nyerere aliwahi kusema kuwa tumuogope kama ukoma mtu anayetaka kwenda ikulu kwa gharama yeyote. Mtazamo huu wa Mwalimu juu ya watu wa namna hiyo unafikirisha sana na kufanya tutafakari sana na kujiuliza maswali yafuatayo: kama mtu ana ndoto ya kuwa rais, si ataipigania ndoto yake kwa namna yeyote ili aende ikulu kuwa rais? Je, mwalimu aliona nini mpaka kufikia kutoa kauli kama hiyo?

Nimetafakari na kuona kuwa maneno ya Mwalimu Nyerere yalikuwa sahihi ya kwamba tumuogope mtu wa namna hiyo kwa sababu kuna wengine wanapelekeshwa na tamaa ya kuwa Rais kuliko matarajio yao na hivyo kutumia kila njia kutimiza tamaa zao na si matarajio yao. Moja ya watu wenye Tamaa hiyo ni Tundu Lissu, tamaa hiyo inampeleka puta haswa hata kufikia hatua ya kuichafua nchi yake na Rais wake.

Kiukweli kwenye mahojiano aliyofanya kwenye kipindi cha BBC HARDTALK kimeonesha ni kwa namna gani Tundu Lissu akipelekeshwa na tamaa ya urais mpaka kufikia hatua ya kuichafua nchi yake na Rais wake. Ni mara nyingi katika kipindi hicho alikuwa akiulizwa kama ana ushahidi wa yale anayoyasema dhidi ya serikali yake kwa shutuma kama hizo na yeye kusema inafahamika hivyo kama jibu.

Ni aibu na fedheha kubwa sana kwa mtu kama Tundu Lissu ambaye ni msomi wa sheria kuishutumu serikali imehusika na hiki na kile kwa shutuma kubwa za kuhatarisha amani na usalama bila kuwa na ushahidi. Ni vile tu mwandishi hakusema ila angepata nafasi angemwelezea kuwa kwa kosa kama hilo la kuishutumu serikali bila ushahidi kwa hapa uingereza ni kosa kubwa sana na adhabu yake ni kubwa.

Mwandishi wa kipindi kile kasaidia kwa namna kubwa sana kuamsha hisia za watanzania kwa kufichua ubabaishaji wa Tundu Lissu kwa dunia na uhatari wa anayoyafanya kuwa yanaweza kuhatarisha amani na usalama wa nchi. Shutuma anazozipeleka kwa rais wetu ni kubwa na zinahitaji ushahidi wa kutosha kuzitoa kwa sababu zinasababisha wawekezaji na watalii kupungua kutokana na hali mbaya ya kiusalama na uvunjifu wa amani unaoratibiwa na serikali kama Tundu Lissu anavyotaka iwe .

Serikali kama mlinzi namba moja wa usalama na amani ya nchi na raia wake hauna sababu za kueleza sababu za kiusalama kisiasa hasa zile ambazo hawana kithibitisho kuwa zimesababishwa na nini. Katika suala la Tundu Lissu kuna nadharia nyingi juu ya kushambuliwa kwake hivyo Lissu kuishutumu serikali kufanya hivyo moja kwa moja ni kosa na hivyo wenye akili inabidi tujiulize ni kwa nini serikali tu?

Jibu ni kwamba, Tundu Lissu anapelekwa puta na mawazo ya kuwa Rais hivyo ameanza kujipanga taratibu kwa kujenga chuki kwa wananchi kuwa CCM ndio wahusika hivyo wanapata nguvu ya kufanya fujo pale CCM inapowashinda kwenye uchaguzi mkuu wakisaidiwa na wanaowatuma kufanya hivyo.

Tundu Lissu , Dunia nzima sasa inajua lengo lako si zuri kwa nchi yako na waandaaji wa BBC hardtalk wameona aibu kumuhoji mtu ambaye hana data wala ushahidi wa tuhuma anazozitoa kwa serikali ambazo kwao wenyewe wanajua kwa tuhuma kama zile kwa nchi kama uingereza ni makosa makubwa. Umeamua kuichafua nchi yako kwa kupelekwa puta na urais ambao huna hakika utapata ama laaa .

Ushauri

i. Tundu Lissu asinyamaziwe, kwa nguvu ile ile anayoitumia kuichafua nchi kwa shutuma za kuokoteza zisizo na ushahidi ni vyema serikali ikatumia nguvu hiyo hiyo kumjibu . Tundu Lissu ajibiwe kisiasa na kitaalamu.

ii. Tundu Lissu atakapo rudi Tanzania kuandaliwe mdahalo kati ya Tundu LIssu na mwanaCCM mmoja ,watumie jukwaa hilo kumjibu kwa sababu Tundu Lissu hajaichafua serikali katuchafua pia CCM kwa kuwa ndio tunaongoza serikali.

Hitimisho

Tundu Lissu anajiona anajua sana kwa sababu anaamini hakuna mwanaCCM mwenye uwezo wa kumjibu ila akijibiwa atanyamaza kimya. Kila mtanzania mwenye akili timamu anamjua Tundu Lissu anafanya anayoyafanya kwa sababu ya tamaa ya Urais na anatengeneza mazingira mapema ili kushindana na nguvu ya Lowassa ndani ya CHADEMA.

na Karlo Mwilapwa
Hebu Mjibu wewe Kiongoz!!!!?ingekuwa tunaruhusiwa kuwapiga mawe watu wanafiki hadharani sidhani kama kuna mwana CCM angesalimika!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
The guy NAILED IT ............ ndiyo sababu ya thread tofauti tofati kufunguliwa kuja na Propaganda!!

Na mtangazaji amemalizia kwa kusema "Tundu Lisu, we will be watching that story. Thank very Much"
 
Nimesikiliza Hard Talk ya BBC. imethibitisha uwezo mdogo wa Lissu kuelewa mambo. Kinachoshangaza ni jinsi mtu huyu anavyokuwa nje ya maswali. Kila wakati anahangaika kusimulia alivyopigwa risasi badala ya kujibu anachoulizwa.

Anapoulizwa suala la ushoga, alitaka kukwepa kwa kuonyesha eti serikali inaingilia mambo ya bedroom lakini mtangazaji ana uelewa kuliko yeye anamrudisha kwenye swali. Jibu lake anajiuma-uma, anajiuma-uma tena na kujikuta analazimisha kujibu kwamba atatetea haki za kila mtu, akimaanisha hata ushoga ni haki kwa mujibu wa haki zetu. Hiyo iko tofauti na jinsi alivyoanza kukubali kwamba kuna sheria ya miaka mingi inayozuiya ushoga. Jibu hili naamini alikuwa akijaribu kumfurahisha muulizaji badala ya kuisemea jamii ya Tanzania. Je, Kweli Lissu anaamini anachofikilia ndicho wa-TZ wanachokitaka? Au basi ni kiumbe asiyejielewa?
Wewe mwenyewe uwezo wako ni mdogo huwezi kutoa tafhimini ya interview ya Tundu Lisu kwani alivyoongea ndivyo ilitakiwa aongee akiweka akiba ya maneno kwani bado zipo interview nyingi zinakuja
 
Lissu anajiabisha sana kifanya Siasa na kwenye maswala ya data. Hesabu hazidanganyi.. Mzungu anahoji akiwa na data mkononi afu mtu hana hapa data za mapato ya TRA anafuta kwanza swali afu anajibu la kichwani kwake. Nimemuona mweupe sana Leo. Amejitahidi tu kuonyesha nyongo na JPM lakini kwenye data na uongongo mwingi.. Hadi mzungu akaona anataka kutoka nje ya Mazda.
Data gani mkuu maana serikali ya magu si imezifanya data kuwa ni hatimiliki yake?
 
Alitoa mbona,kwamba viroba vyenye miili ya watu inaokotwa kwenye fukwe za bahari na kwenye mitaro ya maji machafu.

Kwamba kuna watu waliuawa kibiti,mkuranga na maeneo mengine

Kwamba wapinzani kila kukicha wao wapo mahakamani kwa kusingiziwa Kesi

Kwamba wale watu ambao walidaiwa kuwa ni wezi wa madini na kamati ya wale maprofesa wazoefu waliotuambia kuwa kila m-tz atapata Noah moja, Mtukufu raisi aliwaita kuwa ni Wanaume na watalipa kifutajasho cha $300 million ambazo hazijalipwa Hadi leo

Kwamba biashara imekuwa ngumu Sana,wafanyabiashara wakubwa na wawekezaji wamefunga biashara zao kwa figisu za serikali hii

Na nyingine kibao. Kama hizi sio evidence kwako, naomba usi-quote comment yangu maana utakuwa hujitambui

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu sheria ina miiko yake,ushahidi wakina ulitakiwa kuwa watu 300 waliodaiwa kuuwawa na kuwekwa kwenye viroba wakielea kwenye pwani ya bahari ya Indi ni wapinzani wa serikali kutoka Kibiti.
Kwa mwanasheria mzoefu kama Lissu alitakiwa awe makini na tuhuma zenye ushahidi na sio allegations.
Lakini jambo muhimu ni kuwa hakujitayarisha vilivyo.Ila kama atapata nafasi nyingine,ameishapata funzo,atatumia nafasi yake vyema.
 
The guy NAILED IT ............ ndiyo sababu ya thread tofauti tofati kufunguliwa kuja na Propaganda!!

Na mtangazaji amemalizia kwa kusema "Tundu Lisu, we will watching that story. Thank very Much"
Mimi nimependa sana yale mahojiano , yalimvua mtu nishai, Tundu Lissu alibaki mtupu kabisa , alikuwa anamung'unya maneno mpaka basi na mara nyingi ameambiwa wewe ni mwanasheria si vizuri kuongea bila ushahidi.
 
Mkuu sheria ina miiko yake,ushahidi wakina ulitakiwa kuwa watu 300 waliodaiwa kuuwawa na kuwekwa kwenye viroba wakielea kwenye pwani ya bahari ya Indi ni wapinzani wa serilali kutoka Kibiti.
Kwa mwanasheria mzoefu kama Lissu alitakiwa awe makini na tuhuma zenye ushahidi na sio allegations.
Lakini jambo muhimu ni kuwa hakujitayarisha vilivyo.Ila kama atapata nafasi nyingine,ameishapata funzo,atatumia nafasi yake vyema.
tatizo ni kufikiri kila saa yupo kwenye mikutano ya kampeni.
 
tengeneza utetezi uwezavyo ila mwishowe aliishia kutoa tuhuma zisizo na ushahidi. Halafu, si kwamba mtu akiongea kiingereza au kujitetea kwa kiingereza ndio kuongea ukweli.
Na hapo ndio bavicha wanapochemka. Wao walikua wanaangaika na kiingilishi wakati mzungu mwenyewe alikua anataka facts.

Nokia ya kitochi yuzingi jamii foramu
 
Kada wa CCM Bollen Ngetti anatoa rai yake.

DAWA YA TUNDU LISSU HII HAPA

Na Bollen Ngetti

YULE Afisa Usalama wa TISS alimwambia Zitto, "dawa yako ni kukuua". Hii maana yake ni kwamba mbinu zote zimefeli na njia sasa inayoonekana muafaka ni kumuua Zitto.

Inawezekana waliopanga na kuratibu mabunduki kwa Lissu nao waliona hakuna namna isipokuwa ni kumuua Lissu jaribio lililoshindwa licha kutumia risasi nyingi. Sitoshangaa kama kundi hilo la watu waovu linapanga Plan C maana kuua kulifeli, kuporwa Ubunge nao umeshindwa. Je, Tundu Lissu ameshindikana? Lakini pia tujiulize kosa hasa la Lissu ni lipi? Kukosoa Serikali? Kuna tofauti gani Kati ya Lissu na Jamal Kashoggy wa Saudia?

Nimefuatilia mahojiano ya Lissu kipindi cha "Hard Talk" cha BBC. Lissu amejitahidi sana kujibu maswali magumu ya BBC. Alichonivutia Lissu ni kwamba alikwepa kuongea uongo. Alisimamia ukweli wa alichofanyiwa na hali halisi ya siasa za Tanzania.

Dawa ya kutibu ugonjwa ws "Lissu" si kuweweseka, si kutapatapa, si kutukanana mitandaoni. Tunakosea sana wana CCM wenzangu. Lissu ajibiwe kwa hoja si vihoja. Mbona ni utamaduni wetu kujibu hoja? Wako wapi kina Nape, Mwigulu nakadhalika kumjibu Lissu?

Lakini pia tuelewe kuwa kutokana na kunusurika kifo, imemwongezea Lissu umaarufu mkubwa wa kisiasa maana sasa anabebwa na "global sympathy" (huruma ya dunia). Hii ni hatari sana. Kama kura ingepigwa Leo ya Urais Kati ya Lissu na Magufuli kuna uwezekano Lissu angepata kura nyingi za huruma kutoka kwa kina mama ni vijana chini ya miaka 35. Kura za huruma huwa ni hatari sana maana watu hawatoangalia mema yote uliyowatendea Bali wataangalia huruma.

Uwezekano wa Lissu kugombea Urais 2020 ni mkubwa na kadri tunavyoweweseka ndivyo tunavyozidi kumpaisha. Ninachoshauri CCM tuwe makini kumpata a very strong candidate kuweza kumvaa Lissu ili tuvuke salama. Tujiulize kwa tutakayemsimamisha je, atatuvusha salama au itabidi kutumia "bao la mkono?" Na je, "bao la mkono" litakuwa na nafasi tena katika mwanga huu ambapo dunia nzima macho yako Tanzania? Baraza la Wazee mtusaidie. Vyombo vya dola muwe "fair" kutenda haki na demokrasia. Ni vizuri JPM ashauriwe kugombea tena maana hajatangaza kufanya hivyo. Na endapo atakataa basi mgombea anayeweza kumuangusha Lissu 2020. Hiyo pekee ndio dawa ya Lissu na si kuweweseka na wito wa kumtaka arudi nyumbani. So what?

Sote tunajua mwezi wa tatu EU na USA watakata uhusiano wa kifedha na nchi yetu kwa mujibu wa taarifa zao. Sasa vijana wa Lumumba tusianze kujipanga kumhusisha Lissu na hili, hapana. Ni sisi wenyewe tumeshindwa kujenga mahusiano mazuri na mataifa haya katika kuheshimu utawala bora na haki za binadamu. Tujiandae kisaikolojia kabla ya kufikiria "kuchapa noti hewa" kuokoa jahazi. Tujibu hoja za Lissu maana zinajibika. Msemaji wa Serikali ajitokeze kumjibu Lissu na si propaganda! Paul Makonda si size ya Lissu maana si mwanasiasa huyu. Hoja za Lissu ni za kisiasa!
#AchaWoga2020
We ni ni mwana CCM kweli? Ƙama ni kweli basi kumbe CCM bado ina watu wenye ufahamu mzuri!
 
Ndugu zangu,

Kama wazungu wanatambua kuwa tuhuma za akina Tundu Lissu, Zitto Kabwe na wenzao kuwa ni za 'kutengeneza' basi wabadili mbinu.

kitendo cha waandishi wa media za kimataifa kuyaita madai ya Lissu kuwa ni ''base less allegations'' au ''inflamatory statement ni dhahiri wapo uchi.

Huenda Zitto Kabwe naye hajatupa mrejesho wa Mwenyekiti wa jumuiya za madola baada ya kuambiwa ''your allegations against Hon.Ndugai with respect to CAG are utter baseless''

Tuliwahi kusema hapa uongo haudumu na ndicho kilichotokea na zaidi umewaumbua watu mchana.

Ni dhahiri hata ule mpango wa akina Ngurumo kutafuta ''hadi ya ukimbizi'' Finland umeshindwa.

Tanzania yetu sote, tuipende,tuikumbatie.

Masikini vibwengo wa ccm hamjaelewa mchezo uliochezwa, Steve yuko well informed na hali halisi iliyopo hapa bongo ila alikuwa ana mprovoke Lissu ili afunguke zaidi na dunia ijue kinachoendelea hapa nyumbani.
 
Watu mbona understanding yenu ndogo, yule mwandishi alikuwa anachokoza mada. Mmezoea waandishi uchwara wa TBC wanaosifia sifia tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
kamanda hakuna kitu kama kuchokoza, suala la mwanasheria kutoa tuhuma bila kuwa na ushahidi ni aibu. Akiulizwa una ushahidi wapinzani wananunuliwa anajibu..''contact them...'' sasa hii ndio kuchokoza mada?
 
Masikini vibwengo wa ccm hamjaelewa mchezo uliochezwa, Steve yuko well informed na hali halisi iliyopo hapa bongo ila alikuwa ana mprovoke Lissu ili afunguke zaidi na dunia ijue kinachoendelea hapa nyumbani.
Kamanda ni dhahiri matusi ni matokeo ya hasira za kushindwa kujenga hoja. Ukweli unao,pole.
 
m

Tundu lissu limejionyesha mbele ya ulimwengu lilivyo jinga. He has been grilled like meat. Chezea hardtalk stephen sackur. Alifikiria atawadanganya hardtalk kama anavyowadanganya nyumb wa cdm. Hardtalk yuko well versed kuhusu mambo ya tanzania. Hapo lissu ni kingereza tu ndio anajua lakini siasa ni kibaraka takataka. Imeacha walimwengu wakijua jpm anapendwa na amefanya makubwa nchini. Sasa hapo lissu limepata nini. Nimefurahi sana huyu mpuuzi kwenda hardtalk.
Wewe mwenyewe ni kilaza hujui kingereza hata huna ulichoelewa wewe ndiyo jinga kubwa na nyumbu kwani mbugani nyumbu ni wengi kama CCM walivyokuwa wengi lakini mbumbumbu zaidi, hujui hata maana ya kibaraka umekariri ujinga wa akina le mutuz umefurahi nini wakati wewe mwenyewe ni mpuuzi mshamba, nani kakuambia furaha yako itakubalika kwa watanzania wenye Akili? Jpm anapendwa na nani? Kafanya makubwa yapi? Kupiga trilion 1.5 kujenga chato Airport kijijini porini? Kupiga 10% kwenye ununuzi wa ndege mitumba wakadanganya ni ndege mpya? Acheni kujidai nyinyi ni watakatifu wakati ni mashetani wakubwa.
 
Back
Top Bottom