Tundu Antipas Lissu on BBC HARDtalk - 21 January 2019

Tundu Antipas Lissu on BBC HARDtalk - 21 January 2019

alisema maendeleo ni vipau mbele vyake mwenyewe kama uwanja wa chato sawa na ule wa mobutu ambao hauna tija kwa nchi wala maendeleo ya nchi
Hajawa mwadilifu kukubali kuwa mapato ya ukusanyaji yameongezeka pamoja vita dhidi ya rushwa

Kuusu nukta ushoga naona kagoma kubeba msalaba huo ijapokuwa mtoa mada kapotosha ktk hili

Lakini naamini angekuwa magu angetepeta yule mwandishi anajua sana kumbana mtu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
inamana wapinzani walisuka mpango wakawatoa walinzi kwenye nyumba za makazi ya wabunge.
wapinzani wakatoa cctv camera.
wapinza wakatumia nafasi hiyo kumtandika mpinzani mwenzao risasi 30.
wapinzani hao hao wakawa bega kwa bega na mtu waliemshambulia huku wale ccm ambao hawakuhusika wakaamua kujitenga kwa jambo ambalo haliwahusu.
basi nafikiri kuna haja ya ccm kuacha kuwashwa washwa na lisu.
 
Sio mzungu,dunia nzima ndo imeelewa kilichotokea,au unafikiri alikuwa Tanzanite Tv.
You're so myopic
Mkuu acha kujifariji mzungu anajua hata kwamba leo umegegedwa au laa!

Ndio maana nakwambia hao jamaa hawaihitaji kelele za Lisu kujua mambo ya Kibiti.

Alafu hamjifunzi. Dah nyumbu ni nyumbu tu.

Ok tufanya Lisu atasababisha mzungu kuja kumtoa Magufuli madarakani basi ili ufurahi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyu ni kada mtiifu kwa ccm,nawashauri wasipokee maoni yake kwa sababu yataisaidia sana CHADEMA.
Hata hoja za kumjibia Lisu hawana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndugu zangu,

Kama wazungu wanatambua kuwa tuhuma za akina Tundu Lissu, Zitto Kabwe na wenzao kuwa ni za 'kutengeneza' basi wabadili mbinu.

kitendo cha waandishi wa media za kimataifa kuyaita madai ya Lissu kuwa ni ''base less allegations'' au ''inflamatory statement ni dhahiri wapo uchi.

Huenda Zitto Kabwe naye hajatupa mrejesho wa Mwenyekiti wa jumuiya za madola baada ya kuambiwa ''your allegations against Hon.Ndugai with respect to CAG are utter baseless''

Tuliwahi kusema hapa uongo haudumu na ndicho kilichotokea na zaidi umewaumbua watu mchana.

Ni dhahiri hata ule mpango wa akina Ngurumo kutafuta ''hadi ya ukimbizi'' Finland umeshindwa.

Tanzania yetu sote, tuipende,tuikumbatie.
Ameambiwa au alikuwa anaulizwa maswali? Hivi huko CCM mnamatatizo gani au wote ndo ma font fent!
 
Huo ushindi autolee wapi acha kujipa matumaini hewa. Hakuna mjinga atampa ridhaa ya kuongoza nchi mtu kama Tundu Lissu. Hapo tu hajapata urais anaanza kuuza nchi kwa wazungu, akipata je si wazungu watashika idara zote nyeti.

Madaraka anapata kwa kura za wananchi na hawategemei hao TISS. Hao wazungu ni marafiki kwani hawakwepeki. Hakuna rais yoyote wa nchi hii ambaye hajawahi au atakaye wakwepa wazungu. Kura zetu tutampata kwa nguvu.
 
Ndugu zangu,

Kama wazungu wanatambua kuwa tuhuma za akina Tundu Lissu, Zitto Kabwe na wenzao kuwa ni za 'kutengeneza' basi wabadili mbinu.

kitendo cha waandishi wa media za kimataifa kuyaita madai ya Lissu kuwa ni ''base less allegations'' au ''inflamatory statement ni dhahiri wapo uchi.

Huenda Zitto Kabwe naye hajatupa mrejesho wa Mwenyekiti wa jumuiya za madola baada ya kuambiwa ''your allegations against Hon.Ndugai with respect to CAG are utter baseless''

Tuliwahi kusema hapa uongo haudumu na ndicho kilichotokea na zaidi umewaumbua watu mchana.

Ni dhahiri hata ule mpango wa akina Ngurumo kutafuta ''hadi ya ukimbizi'' Finland umeshindwa.

Tanzania yetu sote, tuipende,tuikumbatie.
Nimeangalia ile clup ya hard talk zaidi ya mara tatu. Sijaamini kile wazungu wamemfanyia jamaa. Alibaki anajikanyaga kanyaga tu bila kuwa na hoja zilizonyooka. Nasema ile interview imewaumbua sana chadema. Aibu yao wenyewe. Walitehemea maswali direct yenye mrengo wa kuiabisha nchi lakini jamaa alichokutana nacho ni hatari tupu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
ha ha alisema tashinda magufuli ashinde kwao chato labda alisema kati ya viongozi wa africa magufli anaonekana ameweza kuwapambana na watu wa magaharibi kuhakikisha hapoli mali na kuendekeza rushwa Lissu akasema akasema huyu mtu alisema kwamba tumewaweza na tutarudishwiwa milioni 300 us dollars lakini hapa nikizungumza hatujapata hata senti tano(not a single peny) kwa maana hiyo magufuli kashindwa mimi naona magufuli kaatanua midomo mbavu lakini hola na yeye sasa kaamua kuungana na mabeberu anaibia nchi
Ameendeshwa na hisia za kipinzani na siyo facts,akipewa facts anajingata bila ushahidi wowote,kama BBC kama Hardtalk ni test ya kuongea kingereza nampa A+ kama ni mahojiano na hoja zenye points nampa zeroooo.
 
*LISSU ATAABIKA SANA, AISHIA KUAIBIKA LONDON, ABANWA VIKALI NA KUTOA MAPOVU*

_NA Mwamba wa Kaskazini_

Leo ndio msemo kuwa Kiingereza sio maarifa umethibitika.

Tundu Lissu ana uwezo wa kutosha tu kuongea Kiingereza lakini asubuhi ya kuamkia leo kukosa maarifa kujawa na umbea, uongo na uzushi na uzandiki dhidi ya nchi yake kumemtokea puani akifanya mahojiano na Kipindi cha Hard Talk cha BBC.

Sikiliza haya.

*1.Aonesha Chuki Binafsi Kwa Magufuli*

Kosa la kwanza ni kutojadili hoja bali mtu.Kila alipoulizwa aliishia kutaja jina la Magufuli hata asipohusika.

Mtangazaji mzungu akabaki anashangaa na kumbana kwa maswali zaidi akaishia kutoa macho maskini.

*2.Lissu Hakutegema*

Hakika hata mimi sikutegema kama yule mzungu angefanya utafiti kiasi kile na kuyajua mengi ya Tanzania kiasi cha Lissu mwanzoni tu kubabaika na kuanza kuzusha uongo.

*3. Jaribio la kumdanganya Mzungu lakwama*

Baada ya kuzoea kuandika viwaraka vyake na kuwapa akina Martin Malera wa Tanzania Daima au Ibrahim Yamola wa Mwananchi leo Tundu Lissu kakutana na mwanahabari wa level nyingine.

Akajikuta anakosa ushahidi...anaambiwa unalalamika kila siku Serikali imekushambulia, unaushahidi gani anasema niliona gari inanifuatafuata, mzungu akambana kwani gari ziko ngapi na mtu yeyote si anaweza kukufuatilia kwani umeshafanya kazi ngapi za kukuweka katika risk ikiwemo kuwa wakili, Lissu akajikuta anakiri kuwa ni kweli hana ushahidi wa moja kwa moja bali ushahidi wa mazingira.

Asante sana mzungu, huyu Bwana leo baada ya mbwembwe nyingi sasa kakiri hana ushahidi zaidi ya mazingira tu ambayo pia yanaweza kuonesha chama chake kinahusika au hata dereva wake.

*4.Akosa maarifa kwenye madini*

Maskini hapa ndio jamaa alitoa mimacho tu baada ya mzungu kumbana kuwa yeye alipigania sana masuala ya nchi kufaidika na madini haoni kuwa JPM anachukua hatua nzuri?

Kwa hakika na mimi hapa nilipoteza Kiingereza changu[emoji3][emoji3]Sikumbuki hata Lissu alikuwa anajibu nini, aliishia maskini kutaabika na kuruka ruka huku na kule.Mzungu akaona isiwe shida, akahamisha mada!

Kwa kifupi hapa Lissu alijikuta anatamani kumpinga Magufuli, lakini pia akawaza anampinga kwa lipi?Kurekebisha mikataba ili nchi ifaidike? Akabaki anataja taja tu majina mara uwanja wa ndege Chato wakati nchi nzima vjwanja zaidi ya 15 vinajengwa[emoji3][emoji3]

*5.Mtangazaji aamua kutaja mwenyewe mazuri ya Tanzania.*

Baada ya kuona Lissu hana analolikubali katika nchi yake mzungu wa watu akaamua kutaja mwenyewe mageuzi makubwa yanayoendelea Tanzania.

Akataja mapambano dhidi ya rushwa, akataja kuongezeka kwa mapato akataja kutekelezwa kwa miradi mbalimbali ya kijamii na miundombinu.

Usiniulize wakati wote huu mzungu anashusha nondo Lissu alikuwa kwenye hali gani[emoji3][emoji3]Kumbuka mwenyewe kisa cha chura aliyebanwa na mlango[emoji3]


*6. Atoa mfano wa kitoto, wamuumbua*

Akieleza kwa nini wapinzani wenzake wamekuwa wakirejea CCM kuunga mkono juhudi za JPM Lissu aliishia kirusha matuhuma ambayo hadi mtangazaji akamuonya aache kuropoka bil ushahidi.


Lakini yotrme hii ni kwamba alishachanganyikiwa. Sasa sikia hii: akapewa mfano wa Masha aliyetoka CCM na kwenda upinzani (ingawa badae alirudi CCM) kama naye alihongwa huko upinzani? Usiniulize Lissu alikuwa katika hali gani hapa tena[emoji3]

*7.Akata fahamu, aunga mkono ushoga*

Akiwa hoi bin taaban na kisaikolojia akionekana mtu anayetamani mahojiano yaishe tu, Lissu akaulizwa ukiwa kiongozi wa upinzani na siku ukiingia Ikulu utafuta sheria zinazoelezwa kuwa kandamizi zinazoufanya ushoga kuwa kosa la jinai?

Maskini, mwisho wa zama ukatimia, baba la watu likajikanyagaaaa mwishowe likaingia kingi eti litafuta sheria zote zinazozuia ushoga nchini.Maweeeee[emoji17]

Rasmi Lissu kaunga mkono ushoga. Hakika ametaabika sana.

Kwa nini utaabike lakini?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi huyu jamaa ana akili timamu kweli? Maana naona mara nyingi kwenye post zote hana points zinazoeleweka na uwezo wa kujenga hoja kwake ni shida, sana sana ni kebehi, ushabik na matusi tu..!

Kweli Tanzania bado tuna safari ndefu sana ya kutoa elimu ya uraia kwa watu wa sampuli hii.

Namaanisha huyu mtu
Mgonjwa mtambuka
 
Ushindi wa CCM upo katika kuhakikisha kile walichokiahidi kwenye ilani yao kinatekelezeka kwa asilimia 90 na sio chini ya hapo.

Haya mambo ya kwenda BBC na kuhojiwa ni siasa za muda mfupi, ambazo kadri muda unavyozidi kupita ndivyo zinavyogeuka kuwa sehemu ya jana.

Serikali inayohodhi magogoni ikitaka kuendelea kukubalika ni kuongeza pato la taifa kwa kuanzia na pato la mtu mmoja mmoja.

Kuna suala la zile rada nne, zikishafungwa zitaongeza kwa kiasi kikubwa sana pato la taifa. Pia masuala ya kodi kulalamikiwa na wafanyabiashara, pia ni suala muhimu kutazamwa.

Cha muhimu ni serikali kuendelea kutekeleza kulichomo ndani ya ilani, haya mambo ya mahojiano ni umaarufu wa muda mfupi tu.
 
Nimeangalia ile clup ya hard talk zaidi ya mara tatu. Sijaamini kile wazungu wamemfanyia jamaa. Alibaki anajikanyaga kanyaga tu bila kuwa na hoja zilizonyooka. Nasema ile interview imewaumbua sana chadema. Aibu yao wenyewe. Walitehemea maswali direct yenye mrengo wa kuiabisha nchi lakini jamaa alichokutana nacho ni hatari tupu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Wamezoea kuigilizia majibu badala ya kujiandaa kwa kujisomea kabla ya mtihani. kaulizwa maswali ya msingi yeye akang'ang'ana kutunga maswali yake.
 
Back
Top Bottom