TUNDU LISSU AITHIBITISHIA DUNIA CHADEMA KURUHUSU USHOGA NA USAGAJI IKISHIKA MADARAKA
Leo inaweza ikawa na siku ngumu sana kwa mashabiki, wapenzi na wanachama wa CHADEMA ambao hawajui deals/mikataba na makubaliano ambayo viongozi wao huwa wanaifanya kwa siri ili kuungwa mkono na baadhi ya makundi yanayounga mkono ushoga na usagaji ili wajipatie fedha kwa manufaa yao wenyewe kwa kutumia jina la chama chao.
Kwa muda mrefu wamejificha nyuma ya Fatuma Karume, wakimtumia kufanya kazi ya kutetea mapenzi ya jinsia moja kwa kusema hayo ni mambo binafsi ya chumbani (bedroom affairs) hivyo sheria zetu zimepitwa na wakati na tunatakiwa tuziondoe maana zinaingilia uhuru binafsi wa watu.
Maneno hayo hayo ya Fatuma Karume, leo kwa mara ya kwanza baada ya viongozi wa CHADEMA kuyatetea chini ya kapeti leo Tundu Lissu alijikuta hana jinsi ikabidi authibitishie ulimwengu kuwa wao kama CHADEMA pindi wakaposhika madaraka wataondoa sheria zinazozuia ushoga na usagaji, na kuruhusu ndoa za jinsia moja kwa msingi huo.
Tundu Lissu alikuwa katika mtanziko, maana mtangazaji wa kipindi cha Hard Talk (BBC), Bwana Steve alimuuliza wewe kama kiongozi wa upinzani, unauambia vipi ulimwengu kuwa je mkishika madaraka mtabadili katiba na kuondosha hizo sheria kandamizi na kuruhusu mapenzi ya jinsia moja? Kwa kuwa Lissu anajua jambo hilo ni mwiko na aibu kwa watanzania alijaribu kuruka ruka ili asielezee msimamo wake na wa chama chake , lakini mtangazaji alipombana ili aeleze kinagaubaga Tundu Lissu hakuwa na jinsi zaidi ya kusema wao wataondoa sheria hizo maana zinakandamiza uhuru wa chumbani wa watu.
Lissu aliwekewa chaguo kati ya Watanzania na wafadhiri wao ambao ni wanaharakati wanaotetea ushoga, usagaji na mapenzi ya jinsia moja kwa ujumla. Dunia yote leo imethibitishiwa rasmi kuwa sasa CHADEMA wataruhusu ushoga Tanzania. Kwamba Lissu aende jimboni kwake awaambie wana-IKUNGI kuwa ni halali vijana wao wa kiume kuolewa, na pia aende kule TARIME (Kanda Maalum) awaambie kuwa sasa wakurya inatakiwa wawe mashoga, jambo hili halikubaliki kwa jamii yetu na sasa watu wetu wataamua juu ya kuiunga mkono CHADEMA mpya inayotetea vitendo vinavyokiuka maadili ya Kitanzania na imani zetu za dini.
Hivyo ni rasmi sasa katika harakati zao na moja ya sera za CHADEMA kuelekea uchaguzi wa 2020 watakuwa wanatetea mapenzi ya jinsia moja, ndoa za jinsia moja, ushoga, usagaji na mambo ya aina hiyo yaliyokuwa yakifanyika Sodoma na Gomora. Mungu aepushie mbali laana hii katika ardhi ya nchi yetu.
YAANI KUTOKA KUWA MAKAMANDA HADI KUWA MASHOGA? KWELI UKISHANGAA YA MUSA UTAONA YA FIRAUNI.