Tundu Antipas Lissu on BBC HARDtalk - 21 January 2019

Tundu Antipas Lissu on BBC HARDtalk - 21 January 2019

Acha kujitoa ufahamu wewe.,akili yako iko kwenye hesabu tu!!!!? Hata zingekuwa mia.....au unajua idadi ya ulizompiga? Zungumzia issue ya shambulizi la Lisu sio idadi ya risasi.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ukiijadili kwa extremism za kiitikadi tayar utakua na mhuhumiwa, ila ukisimama katikat unakua na illusions zaidi ya 3

Sent using Jamii Forums mobile app
 
TUNDU LISSU AITHIBITISHIA DUNIA CHADEMA KURUHUSU USHOGA NA USAGAJI IKISHIKA MADARAKA

Leo inaweza ikawa na siku ngumu sana kwa mashabiki, wapenzi na wanachama wa CHADEMA ambao hawajui deals/mikataba na makubaliano ambayo viongozi wao huwa wanaifanya kwa siri ili kuungwa mkono na baadhi ya makundi yanayounga mkono ushoga na usagaji ili wajipatie fedha kwa manufaa yao wenyewe kwa kutumia jina la chama chao.

Kwa muda mrefu wamejificha nyuma ya Fatuma Karume, wakimtumia kufanya kazi ya kutetea mapenzi ya jinsia moja kwa kusema hayo ni mambo binafsi ya chumbani (bedroom affairs) hivyo sheria zetu zimepitwa na wakati na tunatakiwa tuziondoe maana zinaingilia uhuru binafsi wa watu.
Maneno hayo hayo ya Fatuma Karume, leo kwa mara ya kwanza baada ya viongozi wa CHADEMA kuyatetea chini ya kapeti leo Tundu Lissu alijikuta hana jinsi ikabidi authibitishie ulimwengu kuwa wao kama CHADEMA pindi wakaposhika madaraka wataondoa sheria zinazozuia ushoga na usagaji, na kuruhusu ndoa za jinsia moja kwa msingi huo.

Tundu Lissu alikuwa katika mtanziko, maana mtangazaji wa kipindi cha Hard Talk (BBC), Bwana Steve alimuuliza wewe kama kiongozi wa upinzani, unauambia vipi ulimwengu kuwa je mkishika madaraka mtabadili katiba na kuondosha hizo sheria kandamizi na kuruhusu mapenzi ya jinsia moja? Kwa kuwa Lissu anajua jambo hilo ni mwiko na aibu kwa watanzania alijaribu kuruka ruka ili asielezee msimamo wake na wa chama chake , lakini mtangazaji alipombana ili aeleze kinagaubaga Tundu Lissu hakuwa na jinsi zaidi ya kusema wao wataondoa sheria hizo maana zinakandamiza uhuru wa chumbani wa watu.

Lissu aliwekewa chaguo kati ya Watanzania na wafadhiri wao ambao ni wanaharakati wanaotetea ushoga, usagaji na mapenzi ya jinsia moja kwa ujumla. Dunia yote leo imethibitishiwa rasmi kuwa sasa CHADEMA wataruhusu ushoga Tanzania. Kwamba Lissu aende jimboni kwake awaambie wana-IKUNGI kuwa ni halali vijana wao wa kiume kuolewa, na pia aende kule TARIME (Kanda Maalum) awaambie kuwa sasa wakurya inatakiwa wawe mashoga, jambo hili halikubaliki kwa jamii yetu na sasa watu wetu wataamua juu ya kuiunga mkono CHADEMA mpya inayotetea vitendo vinavyokiuka maadili ya Kitanzania na imani zetu za dini.

Hivyo ni rasmi sasa katika harakati zao na moja ya sera za CHADEMA kuelekea uchaguzi wa 2020 watakuwa wanatetea mapenzi ya jinsia moja, ndoa za jinsia moja, ushoga, usagaji na mambo ya aina hiyo yaliyokuwa yakifanyika Sodoma na Gomora. Mungu aepushie mbali laana hii katika ardhi ya nchi yetu.

YAANI KUTOKA KUWA MAKAMANDA HADI KUWA MASHOGA? KWELI UKISHANGAA YA MUSA UTAONA YA FIRAUNI.
 
Labda kwa hao wa ccm but me binafsi nimeona kupwaya huko BBC ....cjui CCN itakuwaje mana watangazaji wao ni very smart zaidi ya Steve wa BBC.

Sent using Jamii Forums mobile app
Atakosaje kupwaya..ye alidhani anahojiwa na baruani muhuza..uongo mwingii..jamaa kule wana facts..nilichojifunza ni kuwa steve ni genious sana..ana taarifa za kutosha..nimeamini magufuli ni mpango wa Mungu..unavyotaka kummaliza ndio unamuinua..yaani steve alikuwa anafanya kazi ya kueleza mazuri ya magu kupitia majibu ya tundulissu..kuna umuhimu wa kumuacha tundulissu abaki huko akutane na waandishi kama kina steve ili magu afahamike zaidi na dunia ijue mageuzi anayoyafanya tanzania..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dar es Salaam. Majibizano kati ya Tundu Lissu na Spika Job Ndugai yamezidi kukua baada ya mbunge huyo wa Singida Mashariki (Chadema), kuhoji maswali lukuki kuhusu taarifa za matatizo yake akijibu hoja kwamba hana kibali cha kuwa nje ya nchi.

Juzi, Lissu alitoa waraka alioupa jina la “Baada ya Risasi Kushindwa, Sasa Wanataka Kunivua Ubunge”, ukieleza tuhuma zake dhidi ya Serikali kuwa kuna mpango wa kumvua uwakilishi wake wa Singida Mashariki.

Lakini Spika Ndugai aliiambia Mwananchi juzi madai hayo ya Lissu ni “uzushi”, akieleza kuwa Lissu anapaswa kutambua “hana ruhusa ya Spika ya kuwa huko anakozurura”.

“Yeye ametoka kuugua aache uzushi, arudi nyumbani. Tunamsubiri nyumbani,” alisema Spika Ndugai juzi.

“Kitu muhimu ni kwamba ajue hana ruhusa ya Spika ya kuwa huko anakozurura. Sasa achunge kidogo, maana Spika ana nguvu zake, asimpe sababu.”

Ndugai alisema hawezi kumpangia Lissu mambo ya kusema ila ofisi yake haina taarifa.

Hata hivyo, Lissu, ambaye ni mnadhimu wa kambi rasmi ya upinzani bungeni, alikuwa na maswali mengi wakati alipozungumza na Mwananchi jana kuhusu majibu hayo ya Ndugai.

“Spika anajuaje kwamba nimepona? Anajua masharti niliyopewa na daktari ni yapi? Anajua nimetokaje hospitalini?” alihoji Lissu, ambaye alipelekwa Ubelgiji kumalizia matibabu ya majeraha aliyopata mwaka juzi baada ya kushambuliwa kwa risasi takriban 30 na watu wasiojulikana akiwa nje ya makazi yake, Area D mjini Dodoma.

“Spika hajui. Hajui kwa sababu yeye, tume ya utumishi wa Bunge au maofisa wa Bunge hawajaja kuniona tangu Septemba 7 mwaka juzi niliposhambuliwa.

“Spika Ndugai hajui chochote, hajui nimepona au sijapona. Hajui kwa sababu hajataka kujua, hajataka kunipigia simu kuniuliza kama ambavyo wengine wananipigia simu. Hajataka kuwasiliana na familia yangu, hajui kwa sababu ametaka kubaki asiyejua,” alisema Lissu.

Lissu, mmoja wa watu walioibukia kuwa wakosoaji wakubwa wa Serikali, alisema Spika amesikia tu kuwa yuko Uingereza lakini hajui yuko wapi.

“Ukimuuliza leo Lissu yupo wapi sidhani kama atakuwa na jibu. Hawezi kuwa na jibu kwa sababu yeye na watu wake hawataki kumjulia hali Lissu,” alisema.

Mwanasheria huyo alisema Spika aliwahi kusema kuwa angemtembelea wakati akiwa Hospitali ya Nairobi nchini Kenya au sehemu yoyote ile, lakini mpaka jana hakuwa ametimiza ahadi hiyo.

Lissu pia alizungumzia hoja ya Ndugai kuwa hana kibali cha ofisi ya Spika.

“Hicho kibali kinatolewa katika mazingira gani? Nilishambuliwa mchana kabisa Dodoma na kusafirishwa nikiwa sijitambui. Sasa ni muda gani nilipaswa kuomba kibali?” alihoji.

Alisema suala hilo la kusafirishwa kwenda Nairobi kwa matibabu liliamuliwa katika kikao kilichofanyika Dodoma kilichomuhusisha Ndugai, Dk Tulia Ackson (Naibu Spika), Dk Thomas Kashililah (katibu wa Bunge wa wakati huo, Freeman Mbowe (Mwenyekiti Chadema), Ummy Mwalimu (Waziri wa Afya) na Dk Mwigulu Nchemba (aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani).

“Mimi nikiwa sijitambui, napigania roho yangu,” alisema Lissu ambaye alisema taarifa za kikao hicho alipewa baadaye.

“Katika kikao kile iliamuliwa mimi nipelekwe Hospitali ya Nairobi na nikasindikizwa na daktari wa Dodoma na ndege ikaruhusiwa kuruka saa 6:00 usiku. Sasa hicho kibali ninachoambiwa na Spika Ndugai ni kipi?

“Yeye alikuwepo, aliniona, hicho kibali anachokisema ni kipi? Mtu aliyejeruhiwa vile anaweza kuomba kibali? Au kuniona Uingereza ndio nimepona?”

“Hawajaja kuniona ndio maana wanasema nimepona. Wangekuja kuniona wangejua hicho wanachokisema kina ukweli kiasi gani. Wangejua nimepona au bado, sasa wanabaki kusema nimepona bila kuja kuniona?”

Lissu aliyeshambuliwa mchana wa Septemba 7, 2017 akiwa ndani ya gari, nje ya makazi yake Area D, mjini Dodoma baada ya kuhudhuria kikao cha Bunge, amekuwa akikosoa jinsi Bunge lilivyoshughulikia suala lake, ikiwa ni pamoja na kutogharamia matibabu yake.

Alipata matibabu nchini Kenya hadi Januari 6, mwaka jana alipohamishiwa Ubelgiji alikohitmisha matibabu yake Desemba 31, mwaka jana. Hivi sasa anaendelea na mazoezi yanayolenga kumuwezesha kutembea bila ya magongo.

Lissu ameshasema kuwa siku ambayo madaktari watamruhusu, atapanda ndege siku inayofuata na kwamba ataiachia Serikali jukumu la kulinda usalama wake.

Kuhusu safari yake ya Uingereza, Lissu alisema huwa anaruhusiwa kwa siku chache ambazo anaweza kuzitumia kusafiri nje ya Ubelgiji.

Alisema safari ya London ni takriban saa mbili.

Katika madai yake ya juzi, Lissu alisema hawezi kupuuza taarifa alizoambiwa na watu wake wa karibu kuhusu kuvuliwa ubunge.

“Nimepata taarifa kutoka kwa watu wawili tofauti kwamba kuna mkakati unaandaliwa wa kunivua ubunge wa Jimbo la Singida Mashariki,” aliandika Lissu.

Alisema hoja zinazotumiwa ni kutokuwa na kibali, kutohudhuria vikao na kutotoa taarifa ya maandishi ofisi ya Bunge.

Mwananchi
 
Lissu Jana Akiwa BBC amesema kwamba Alishambuliwa kwa jumla ya Risasi 54, yaani 16 ziliingia Mwilini na 38 zikimkosa.
.....
Sasa Mbona Taarifa ya Lissu inatofautiana na ile ya Chadema Waliyoitoa Mwanzo Kwamba Lisu alishambuliwa kwa jumla ya Risasi 38 kati ya hizo 17 zikiingia Mwilini na 21 zikimkosa?
....
Kwa hiyo Kwa Alichokisema Lisu Jana Ni Kwamba tayari zimeongezeka Risasi zingine 16.

Sent using Jamii Forums mobile app
Leo sikua na ratiba ya kucheka umenichekesha sana kwaiyo 16 hazina shida sindio kwenye mwilini
 
Lissu Jana Akiwa BBC amesema kwamba Alishambuliwa kwa jumla ya Risasi 54, yaani 16 ziliingia Mwilini na 38 zikimkosa.
.....
Sasa Mbona Taarifa ya Lissu inatofautiana na ile ya Chadema Waliyoitoa Mwanzo Kwamba Lisu alishambuliwa kwa jumla ya Risasi 38 kati ya hizo 17 zikiingia Mwilini na 21 zikimkosa?
....
Kwa hiyo Kwa Alichokisema Lisu Jana Ni Kwamba tayari zimeongezeka Risasi zingine 16.

Sent using Jamii Forums mobile app
Utakuwa na Tatizo na kugha iliyotumiwa. Rudi sikiliza Tena.....!!!
 
TUNDU LISSU AITHIBITISHIA DUNIA CHADEMA KURUHUSU USHOGA NA USAGAJI IKISHIKA MADARAKA

Leo inaweza ikawa na siku ngumu sana kwa mashabiki, wapenzi na wanachama wa CHADEMA ambao hawajui deals/mikataba na makubaliano ambayo viongozi wao huwa wanaifanya kwa siri ili kuungwa mkono na baadhi ya makundi yanayounga mkono ushoga na usagaji ili wajipatie fedha kwa manufaa yao wenyewe kwa kutumia jina la chama chao.

Kwa muda mrefu wamejificha nyuma ya Fatuma Karume, wakimtumia kufanya kazi ya kutetea mapenzi ya jinsia moja kwa kusema hayo ni mambo binafsi ya chumbani (bedroom affairs) hivyo sheria zetu zimepitwa na wakati na tunatakiwa tuziondoe maana zinaingilia uhuru binafsi wa watu.
Maneno hayo hayo ya Fatuma Karume, leo kwa mara ya kwanza baada ya viongozi wa CHADEMA kuyatetea chini ya kapeti leo Tundu Lissu alijikuta hana jinsi ikabidi authibitishie ulimwengu kuwa wao kama CHADEMA pindi wakaposhika madaraka wataondoa sheria zinazozuia ushoga na usagaji, na kuruhusu ndoa za jinsia moja kwa msingi huo.

Tundu Lissu alikuwa katika mtanziko, maana mtangazaji wa kipindi cha Hard Talk (BBC), Bwana Steve alimuuliza wewe kama kiongozi wa upinzani, unauambia vipi ulimwengu kuwa je mkishika madaraka mtabadili katiba na kuondosha hizo sheria kandamizi na kuruhusu mapenzi ya jinsia moja? Kwa kuwa Lissu anajua jambo hilo ni mwiko na aibu kwa watanzania alijaribu kuruka ruka ili asielezee msimamo wake na wa chama chake , lakini mtangazaji alipombana ili aeleze kinagaubaga Tundu Lissu hakuwa na jinsi zaidi ya kusema wao wataondoa sheria hizo maana zinakandamiza uhuru wa chumbani wa watu.

Lissu aliwekewa chaguo kati ya Watanzania na wafadhiri wao ambao ni wanaharakati wanaotetea ushoga, usagaji na mapenzi ya jinsia moja kwa ujumla. Dunia yote leo imethibitishiwa rasmi kuwa sasa CHADEMA wataruhusu ushoga Tanzania. Kwamba Lissu aende jimboni kwake awaambie wana-IKUNGI kuwa ni halali vijana wao wa kiume kuolewa, na pia aende kule TARIME (Kanda Maalum) awaambie kuwa sasa wakurya inatakiwa wawe mashoga, jambo hili halikubaliki kwa jamii yetu na sasa watu wetu wataamua juu ya kuiunga mkono CHADEMA mpya inayotetea vitendo vinavyokiuka maadili ya Kitanzania na imani zetu za dini.

Hivyo ni rasmi sasa katika harakati zao na moja ya sera za CHADEMA kuelekea uchaguzi wa 2020 watakuwa wanatetea mapenzi ya jinsia moja, ndoa za jinsia moja, ushoga, usagaji na mambo ya aina hiyo yaliyokuwa yakifanyika Sodoma na Gomora. Mungu aepushie mbali laana hii katika ardhi ya nchi yetu.

YAANI KUTOKA KUWA MAKAMANDA HADI KUWA MASHOGA? KWELI UKISHANGAA YA MUSA UTAONA YA FIRAUNI.

Kwani Tanzania mashoga hakuna? Nenda sinza madukan mtaa unaitwa sodoma utawakuta kibao tu,
 
Tundu Lissu anza kuwavulia nguo hao mabwana zako huko huko wakuhemee kisogoni. Kama unaweza kukubali kuhalalisha ushoga ili upate support ya kugombea urais na kwa akili yako ukasahau kama si mila na desturi za hao unaodhani wanaweza kukupigia kura basi ujue wewe si kiongozi. Kiongozi ni yule anaekumbatia matakwa ya watu wake walio wengi no matter what. Binafsi nimechukia mno na hii interview yako na hawa mabwana zako. Tunafahamu siasa za kimataifa na tunafahamu nini kinatafutwa na hao wazungu. Hatutakupa kura ndugu yangu. Hufai hata ubalozi wa nyumba kumi kumi.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwa nini usijinyonge kama umechukia?
 
Atakosaje kupwaya..
Amepwaya kwenye eneo lipi hasa kama unaweza tuwekee tujue ni dakika ya ngapi na sisi tuangalie alivyopwaya!!

Kumsifia Steve Sakur mwana CCM kama wewe huoni kama unasifia mtangazaji wa chombo cha habari cha mabeberu!?
 
Hapa ninahasira sana
Lissu na wapambe wako nakuuliza ni faida gani umeipata kuichafua Tanzania hii na kumchafua Rais Magufuli?
Kweli umeshindwa kuelezea hata jema moja alilofanya huyu Rais?kweli tunamponda magufuli lakini sio huko mnakoenda huo sii utamaduni wetu watanzania.
Ili pata faida gani serikali baada ya shambulio lá Lissu na kutompa hela za matibabu?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Amepwaya kwenye eneo lipi hasa kama unaweza tuwekee tujue ni dakika ya ngapi na sisi tuangalie alivyopwaya!!

Kumsifia Steve Sakur mwana CCM kama wewe huoni kama unasifia mtangazaji wa chombo cha habari cha mabeberu!?
Fatilia alipoulizwa kuhusu lawrence masha na alichokiongea yeye..
Lakini fuatilia kuhusu Magu kununua ndege na alichokijibu yeye..yaani unamtuhumu mtu kujenga uwanja..kisha unaambiwa kanunua ndege unasema sio kazi yake..wakati ye ndio kasimamia..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mbona unaongea kama vile ni kibaraka wa mabeberu na si Mzalendo!!

Huu ujinga ndiyo watanzania hawataki kusikikia kibaraka vipi? Yaani umetaka kumuua kisha asiongee kisa unakuja na kisingizio cha kishamba kuwa mabeberu mara Uzalendo, hamjui hata maana yake mmekariri Akili za Cyprian musiba, kupigwa Risasi vina uhusiano gani na Uzalendo? au kutafuna trilion 1.5 kifisadi ndiyo Uzalendo? Kujenga chato Airport porini kijijini ndiyo Uzalendo? Kuwabambikia Wapinzani kesi kuwanyanyasa ndiyo Uzalendo? Kula 10% ununuzi wa ndege, ujenzi reli, flyover na miladi kibao ndiyo Uzalendo?
 
Back
Top Bottom