Tundu Antipas Lissu on BBC HARDtalk - 21 January 2019

Tundu Antipas Lissu on BBC HARDtalk - 21 January 2019

Haaa haaah haaaah alifikiri itakuwa ni walk in the park nini,sidhani kama ana hamu naye tena yule interviewer !!!
 
Lissu: Kwa Miaka Mingi Upinzani Na Chama Tawala Tumekuwa Na Vita Ya Maneno, Lakini Hatukuwi, Kufikia Hatua Ya Wapinzani Kupigwa Risasi, Kutekwa Na Kupotezwa, Kama Ilivyo Tokea Katika Uongozi Huu
 
Kumeibuka mjadala mkubwa katika mitandao kijamii kufatia kile kilichodaiwa kuwa ni kauli ya Mh. Spika Ndugai, iliyomtaka arejee nchini na kuendelea na shughuli zake za kibunge vinginevyo sheria itachukua mkondo wake dhidi yake.

Hivi karibuni TAL akihojiwa na moja ya vyombo vya habari huko Uingereza, alisema kwamba kwa sasa amepona na atarudi nchini muda wowote; pia alitumia wasaa huo kuwaweka wazi Watanzania na jumuiya ya kimataifa kuwa yupo tayari kugombea nafasi ya juu kabisa ya uongozi katika nchi yetu hapo mwaka 2020 kama chama chake kitaridhia apeperushe bendera yake.

Kinachoshangaza ni kuwa wapambe wake wamekuwa na wasiwasi juu ya usalama wa Lissu kuliko Lissu mwenyewe. Wakati yeye akisema yuko tayari kurejea nchini wakati wowote, wao wanasema asirejee hata kama atapoteza nafasi ya Ubunge huku wakidai kuwa wanahofia usalama wake na wengine wamesema aombe “Political Asylum” katika moja ya nchi hizo, sijui kwa vigezo vipi. Viongozi wa juu wa CHADEMA bado wapo kimya kabisa katika hili. Kuna siri nzito ambayo Lissu na dereva wake wanajua.

Nilichojifunza hapo ni kuwa wapambe wake wanakubali wazi kuwa TAL anavunja sheria kwa kutojishughulisha na masuala ya Kibunge bila kibali cha Spika wakati akiwa na afya njema kabisa, na badala yake anafanya ziara nje ya nchi zenye malengo hasi kwa nchi yetu. Hivyo wapambe wake hawatashangazwa iwapo Spika ataamua kutomtambua Lissu kama Mbunge, lakini tutarajie malalamiko yao kama kawaida ya kulalamikia kile wasichokiamani.

Lissu bado anaamini kuwa Tanzania ni nchi ya amani tofauti na wapambe wake wanavyoamini na ndiyo maana ameweka wazi mipango yake kisiasa. Tujiulize maswali haya, iwapo ataomba hifadhi nje kama wapambe wake wanavyotaka, “Plan Yake” ya kuwa Rais itakuwaje? Je, atafanya kampeni na kuchaguliwa kutoka huko huko aliko?

Katika hili, Lissu na wapambe wako hamko pamoja kabisa.
Acheni hizo bwana lumumba viongozi waongee nini wana kesi mahakamani wengine wamefungwa mbona mnajitoa ufahamu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna watu humu ni mara yao ya kwanza kusikiliza hiki kipindi ......... tena watakuwa wameambulia 50 % or less ya kilichokuwa kinazungumzwa kutokana na lugha iliyotumika. Wengi wao kwa sasa wanategemea mijadala au michango inayoendelea JF .....!!

Kwa ujumla ni viongozi wachache sana Tanzania wanaoweza kwenda ni kujieleza bila kigugumizi kwenye Hardtalk ..... kama mnabisha mpelekeni Polepole ............!!?
🤣🤣🤣🤣 slow slow bado hajafika level za kuitwa pale yeye Mwisho Milardayo au Lemutz Tv
 
Asante kwa video nimeiangalia yote... Huyu mzungu kafeli kwenye hard talk yake na hayuko neutral, na maswali yake yamebase kwenye takwimu zinazotolewa na serikali na organs zake.... Lissu anaongelea uhalisia wa Tanzania na Mtanzania, point kwa point ana msingi wa kile anachojibu lakini mzungu anauliza vile anavyovisikia bila kuhoji uhalali na uhalisia wake

Jr[emoji769]
umeielewa mkuu? amequote umesikia akirefer independent observer Dann Paget wa Oxford University? Cleaning up of the country amesema we've seen not hear say, sikiliza tena jamaa yuko nondod
 
Back
Top Bottom