Hapana @Jurjani usione ukweli wako kwa mtazamo wako ni ukweli wangu..
Ukweli una tabia moja ya ajabu sana, na juu yake haukaliwi na chochote. Ukweli ni kuwa kama kweli wewe ni mkweli na nafsi yako inashuhuduia,basi ungekiri hili na kuacha kujadili hili sababu liko wazi sana, na hili liko wazi na nilio uandika ni ukweli wa wazi kabisa, ndio maana kuna swali katika nukta moja wapo huko juu hujalijibu.
Pili, nilichokiandika hapa kimemili katika elimu na misingi yake, ndiyo maana nimegusa pande zote, upande wako wangu,wetu na upande ulio dhidi yako.
Tatu, ukweli hauna upande mzee, ndiyo maana huwa mchungu.
Nne, hizi ni falsafa dhaifu za kusema ya kuwa kuna ukweli wa namna unavyojitokeza kwa mtu, yaani wewe uwe na ukweli wako,mimi niwe na wangu tena katika jambo moja. Hapa walio leta hii nadharia walifeli na kuwadanganya watu, ukweli ni MMOJA.
Mimi ni mwadilifu na huwa nikikengeuka nakubali kurelebishwa kwakuwa si mkamilifu na huwa naomba na radhi pia
Kaka usiwe unapoteza muda katika jambo ambalo hata ukipewa miaka na mikaka huwezi kulipinga kielimu, na hapa unadhihirisha hilo. Wewe si muadilifu. Sasa hili iweje linakushinda kwamba umekosea ? Kwanini usikiri hilo ?
Ni wachache sana huwa wanawapa stahiki zao wale wanao wachukia au wale ambao ni maadui zao, hao ni wenye elimu na uchajimungu, sababu huwa wanafanya mambo kwa ajili ya kumridhisha Mola muumba na si kujifurahisha, au kutafuta sifa au mfano wake.
note hii kitu inaitwa ukweli usiegemee sana kwake kwakuwa ukweli hubadilika kulingana na mazingira, imani, hulka na mitazamo...
Kwanza ngoja nikufundishe jambo kuhusu tamko UKWELI, nilichokiona hujui maana ya tamko hili, ndiyo maana linakusumbua na kutoka nje ya mipaka yake.
UKWELI ni kauli au kitendo kinapo afikiana na hali halisi. Maana yake ukweli hauna egemeo, bali unasimama wenyewe popote pale. Ukweli haubadiliki sababu katika ukweli kuna hayo yoyote, yaani itifaki huzingatiwa.
Napenda uhalisia kwakuwa hauna rangi nyingi hivyo haubadiliki wala haubadilishwi
Sasa mbona huu uhalisia wa wewe kumili katika hisia zaidi hutaki kuukiri au kwa sababu uko dhidi yako...?
Waja wema na wenye elimu, walisisitiza sana kutokupendelea kumzungumzia sana yule usiyempenda kwa kuchelea ya kuwa ni rahisi sana kumdhulumu, kumtuhumu na kumfanyia mbaya mengine kisa tu humpendi au mfano wake.