Tunautaabisha mwili kwa manufaa ya nani?

Kuna ratiba ndefu sana ya kuuaga mwili wa aliyekuwa rais wa Tanzania 2015-2021... Kwa ujumla wake ataagwa mara sita maeneo tofauti ya nchi ikiwemo Zanzibar iliyokuja kuchomekwa baadae kwa sababu za kisiasa
Msiba ni gharama kwa kila hatua na ni gharama zaidi kwa kila siku inayoongezeka kila siku ipitiyo bila kuzika...lakini zaidi kiimani ama kiroho si vema kuuhangaisha mwili uliokwisha tengana na roho labda tu iwe kwa maagizo ya mhusika
Safari ya kifo ni ndefu isiyo na kinyume ndio maana wafu hutolewa eneo alilofia, mochwari, nyumbani kisha kaburini... Ni safari ya njia moja... Ni kinyume cha mazoea kuutoa mwili mochwari na kuuanika siku nzima kisha kuurudisha mochwari tena na kuutoa tena na tena...

Watetezi wa hili wana hoja zao kama hizi
Dar kuaga ni mara mbili kutokana na wingi wa wakazi wake
Dodoma ni mji mkuu wa nchi alioupigania katika maisha yake hivyo si vizuri kuwaruka watu wa Dodoma
Mwanza ndio mkoa wa mji alikokulia
Geita na baadae Chato ndio nyumbani
Vipi kuhusu Zanzibar? Ni sehemu ya muungano , japo leo tayari kulikuwa na wawakilishi waliokuja kwa gharama za serikali
Kwa sasa ni matumizi , bajeti wanaijua wachache lakini huko mbeleni huu msiba unaweza kuja kuwa kashfa ya ufisadi
Kwa kila siku ya huu msiba kuna pesa inateketea
Per diem za viwango tofauti
Mafuta ya magari yanayohusika kwenye msiba
Malazi, chakula na vinywaji kwa waalikwa, wahudhuriaji, waombolezaji na wageni mbalimbali
Gharama za majukwaa mbalimbali, viti meza nk
Washereheshaji na watumbuizaji
Gharama za kuhifadhi mwili
Dharura nknk

Tunaweza kufanya mambo bila kujua mtazamo wake lakini isifike mahali tukakufuru kwa kuona kwamba hivi ndivyo inavyopaswa kuwa na zaidi kumbe kuna wapiga dili nyuma yake.

Hali ngumu ya maisha inawafanya baadhi kutumia misiba kama sehemu ya kujazia mashimo yao ya madeni, matumizi na mahitaji mbalimbali

Naweza kupigwa mawe kwenye hii post na wanufaikaji lakini huu... Wale wataosema msiba unabebwa na rambirambi za wapendwa wake. Na bajeti ya kitengo kwa nafasi yake kama mkuu wa nchi..lakini kuagwa mara sita sehemu tofauti za nchi kunaweza kuweka rekodi mpya.
Watasema upelekwe na Mbeya kwa Naibu spika aliye mpigania mpaka akawa mbunge
 
Demi huna haja ya kupanic zaidi nadhani tumeshafunga mjadala kwenye hili...kwakuwa hakuna kitakachobadili uhalisia wa kile nilichoandika
Sijapanic wala, naeleza mtazamo wangu na sidhani kama ulitegemea kila mtu awe upande wako. Kama kupinga hoja yako ni kupanic ni sawa kwa mtazamo wako amini hivyo.
Mjadala umefungwa kivipi wakati bado tunaaccess ya kucomment? Labda ufugwe tusicomment

Sent from my Infinix X5515 using JamiiForums mobile app
 
Kumbe ni mambo ya kisiasa sio tena kuuchosha mwili? Ona sasa hoja yako hata wewe mwenyewe huielewi.
Ungefafanua toka kwanzo kuwa kuna mambo mabaya yanafanyika nyuma ya pazia ambayo sio sahihi. Tungejibu hoja yako katika muelekeo huo.
Unachanganya mambo halafu unatulaumu hatujui kujibu hoja.

Sent from my Infinix X5515 using JamiiForums mobile app
Demi nakushauri tena pumua pumzi ndefu tatu kisha utulie kidogo hiyo panic itashuka ...hii mijadala yenye migongano ya mawazo haitaki panic kabisa
Soma tena nilianza kuzungumzia kiroho kisha maslahi ya wanaohusika ambao kwa vyovyote ni ccm
Kitu ambacho nilikiacha hewani ni hilo swali ... ! Ninini basi maana ya kuwa great thinker kama huwezi kufikiri zaidi ya kufikiri?
 
Tunachojisahaulisha ni kuwa huyu hakuwa tu John Magufuli, alikuwa Rais wa JMT, Tena Rais aliyekufa akiwa madarakani, je tumelifikiria hilo?

Hoja ambayo ningekubaliana na mtoa mada ni kufuja hela, Ila sio "kuuchosha mwili", unachoshaje mtu aliyekufa?
La kufuja pesa hata mimi ningelielewa

Sent from my Infinix X5515 using JamiiForums mobile app
 
Sijapanic wala, naeleza mtazamo wangu na sidhani kama ulitegemea kila mtu awe upande wako. Kama kupinga hoja yako ni kupanic ni sawa kwa mtazamo wako amini hivyo.
Mjadala umefungwa kivipi wakati bado tunaaccess ya kucomment? Labda ufugwe tusicomment

Sent from my Infinix X5515 using JamiiForums mobile app
Hapana hii ni hoja yenye mgongano wa mawazo ndio maana nikaileta huku..lakini nina uzoefu wa kusoma vibe za mtu hata temperature gauge inapoanza kupanda najua
 
Demi nakushauri tena pumua pumzi ndefu tatu kisha utulie kidogo hiyo panic itashuka ...hii mijadala yenye migongano ya mawazo haitaki panic kabisa
Soma tena nilianza kuzungumzia kiroho kisha maslahi ya wanaohusika ambao kwa vyovyote ni ccm
Kitu ambacho nilikiacha hewani ni hilo swali ... ! Ninini basi maana ya kuwa great thinker kama huwezi kufikiri zaidi ya kufikiri?
Panic unaidefine vipi kaka yangu? Haya ngoja ninyamaze waje ambao wanaokubaliana na wewe watakuwa hawajapanic.
Ni kama vile hutaki kupingwa tukubaliane na kila hoja unayoitoa . Haipo hivyo
 
Hapana hii ni hoja yenye mgongano wa mawazo ndio maana nikaileta huku..lakini nina uzoefu wa kusoma vibe za mtu hata temperature gauge inapoanza kupanda najua
Sawa mtabiri
 
Panic unaidefine vipi kaka yangu? Haya ngoja ninyamaze waje ambao wanaokubaliana na wewe watakuwa hawajapanic.
Ni kama vile hutaki kupingwa tukubaliane na kila hoja unayoitoa . Haipo hivyo

Sent from my Infinix X5515 using JamiiForums mobile app
Demi pls nielewe ni wapi niliposema sitaki kupingwa? Nilichokushauri ni tofauti kabisa na ulivyonielewa
 
Kuna ratiba ndefu sana ya kuuaga mwili wa aliyekuwa rais wa Tanzania 2015-2021... Kwa ujumla wake ataagwa mara sita maeneo tofauti ya nchi ikiwemo Zanzibar iliyokuja kuchomekwa baadae kwa sababu za kisiasa
Msiba ni gharama kwa kila hatua na ni gharama zaidi kwa kila siku inayoongezeka kila siku ipitiyo bila kuzika...lakini zaidi kiimani ama kiroho si vema kuuhangaisha mwili uliokwisha tengana na roho labda tu iwe kwa maagizo ya mhusika
Safari ya kifo ni ndefu isiyo na kinyume ndio maana wafu hutolewa eneo alilofia, mochwari, nyumbani kisha kaburini... Ni safari ya njia moja... Ni kinyume cha mazoea kuutoa mwili mochwari na kuuanika siku nzima kisha kuurudisha mochwari tena na kuutoa tena na tena...

Watetezi wa hili wana hoja zao kama hizi
Dar kuaga ni mara mbili kutokana na wingi wa wakazi wake
Dodoma ni mji mkuu wa nchi alioupigania katika maisha yake hivyo si vizuri kuwaruka watu wa Dodoma
Mwanza ndio mkoa wa mji alikokulia
Geita na baadae Chato ndio nyumbani
Vipi kuhusu Zanzibar? Ni sehemu ya muungano , japo leo tayari kulikuwa na wawakilishi waliokuja kwa gharama za serikali
Kwa sasa ni matumizi , bajeti wanaijua wachache lakini huko mbeleni huu msiba unaweza kuja kuwa kashfa ya ufisadi
Kwa kila siku ya huu msiba kuna pesa inateketea
Per diem za viwango tofauti
Mafuta ya magari yanayohusika kwenye msiba
Malazi, chakula na vinywaji kwa waalikwa, wahudhuriaji, waombolezaji na wageni mbalimbali
Gharama za majukwaa mbalimbali, viti meza nk
Washereheshaji na watumbuizaji
Gharama za kuhifadhi mwili
Dharura nknk

Tunaweza kufanya mambo bila kujua mtazamo wake lakini isifike mahali tukakufuru kwa kuona kwamba hivi ndivyo inavyopaswa kuwa na zaidi kumbe kuna wapiga dili nyuma yake.

Hali ngumu ya maisha inawafanya baadhi kutumia misiba kama sehemu ya kujazia mashimo yao ya madeni, matumizi na mahitaji mbalimbali

Naweza kupigwa mawe kwenye hii post na wanufaikaji lakini huu... Wale wataosema msiba unabebwa na rambirambi za wapendwa wake. Na bajeti ya kitengo kwa nafasi yake kama mkuu wa nchi..lakini kuagwa mara sita sehemu tofauti za nchi kunaweza kuweka rekodi mpya.
Kwa Unafiki, haujambo.
 
Angekuwa mwislam wangekuwa washazika.
Sababu imani yao yataka hivyo.

Ila huyu imani yake ni tofauti na kwa mujibu ya imani yake ya kikatoliki si kosa,mwisho wa siku atazikwa kwa misingi ya imani yake ya kiroho ya Roman Catholic.
 
Back
Top Bottom