Tunautaabisha mwili kwa manufaa ya nani?

Tunautaabisha mwili kwa manufaa ya nani?

Wengi wamepotoka sana! Aidha, wengi wanashindwa kuheshimu mawazo tofauti na kushambuliana badala ya kuchambua hoja mbadala. Tunaacha kujadili maudhui na muktadha wa hoja, tunamjadili au kumwelezea mtoa hoja
JF ya sasa uwezo wa kujadili hoja umepungua sana... Hoja hujibiwa kwa hoja..kinyume cha hapo ni mahoka
Kwasasa kwenye hoja nyingi kinzani, malumbano hutoka kwenye hoja na kuhamia kwenye vioja, vijembe na kejeli ama la kumjadili mtoa hoja....!!!
 
Asante kwa bandiko refu lenye ufafanuzi wa yale niliyoandika.. Hitimisho ndio limetoa muktadha wa yote uliyoandika
Bado tunapushana kwenye ukweli na uhalisia... Nitakapopata muda nitakuja na mada inayojitegemea kuhusu ukweli na kuhusu uhalisia..
Usipate shida kushughulika na maneno hayo mawili,sababu moja halikai bila ya mwenzake. Ukweli ndiyo uhalisia wenyewe, ndiyo maana kwenye maana ya Ukweli unakuta ni kuafikiana na hali halisi, uhalisia huanza.
 
Kwasasa hatuongelei tena mtu hai... Bali mwili wa mwendazake ... Sasa kinachotokea hapa ni vitu viwili tofauti kabisa ....Mwili wa marehemu na marehemu! Ukweli ni upi? Uhalisia ni upi? Hapo ndio tunaachana njiapanda
Inaonekana hujaelewa nilichokiandika, maelezo yangu yamejikita kwa Maiti, ambaye kiiamani nimeelezea ya kuwa maisha yanaendelea na yapo ambayo yanaendelea muda huu sisi hatuyaoni.

Kadhalika huwezi kuutenganisha mwili wa mwenda zake na yeye mwenyewe,bali tofauti hapo ni hatua tu za kuelekea katika ukamilifu na lengo la sisi kuwepo duniani.
 
Kuna ratiba ndefu sana ya kuuaga mwili wa aliyekuwa rais wa Tanzania 2015-2021... Kwa ujumla wake ataagwa mara sita maeneo tofauti ya nchi ikiwemo Zanzibar iliyokuja kuchomekwa baadae kwa sababu za kisiasa
Msiba ni gharama kwa kila hatua na ni gharama zaidi kwa kila siku inayoongezeka kila siku ipitiyo bila kuzika...lakini zaidi kiimani ama kiroho si vema kuuhangaisha mwili uliokwisha tengana na roho labda tu iwe kwa maagizo ya mhusika
Safari ya kifo ni ndefu isiyo na kinyume ndio maana wafu hutolewa eneo alilofia, mochwari, nyumbani kisha kaburini... Ni safari ya njia moja... Ni kinyume cha mazoea kuutoa mwili mochwari na kuuanika siku nzima kisha kuurudisha mochwari tena na kuutoa tena na tena...

Watetezi wa hili wana hoja zao kama hizi
Dar kuaga ni mara mbili kutokana na wingi wa wakazi wake
Dodoma ni mji mkuu wa nchi alioupigania katika maisha yake hivyo si vizuri kuwaruka watu wa Dodoma
Mwanza ndio mkoa wa mji alikokulia
Geita na baadae Chato ndio nyumbani
Vipi kuhusu Zanzibar? Ni sehemu ya muungano , japo leo tayari kulikuwa na wawakilishi waliokuja kwa gharama za serikali
Kwa sasa ni matumizi , bajeti wanaijua wachache lakini huko mbeleni huu msiba unaweza kuja kuwa kashfa ya ufisadi
Kwa kila siku ya huu msiba kuna pesa inateketea
Per diem za viwango tofauti
Mafuta ya magari yanayohusika kwenye msiba
Malazi, chakula na vinywaji kwa waalikwa, wahudhuriaji, waombolezaji na wageni mbalimbali
Gharama za majukwaa mbalimbali, viti meza nk
Washereheshaji na watumbuizaji
Gharama za kuhifadhi mwili
Dharura nknk

Tunaweza kufanya mambo bila kujua mtazamo wake lakini isifike mahali tukakufuru kwa kuona kwamba hivi ndivyo inavyopaswa kuwa na zaidi kumbe kuna wapiga dili nyuma yake.

Hali ngumu ya maisha inawafanya baadhi kutumia misiba kama sehemu ya kujazia mashimo yao ya madeni, matumizi na mahitaji mbalimbali

Naweza kupigwa mawe kwenye hii post na wanufaikaji lakini huu... Wale wataosema msiba unabebwa na rambirambi za wapendwa wake. Na bajeti ya kitengo kwa nafasi yake kama mkuu wa nchi..lakini kuagwa mara sita sehemu tofauti za nchi kunaweza kuweka rekodi mpya.
Maraisi wote ni wazanzibar kwahiyo issue yakupeleka Mwili wa JPM ZNZ imekua simple tu
 
Na kwa kum'airlift' tunaweza kuikuta roho huko angani inashangaa, ikiuona mwili wake inaweza ghairi kwenda ikaurudia mwili na kupiga chafya🙏! Uone sherehe itakayofuata! Bado hatuamini kama kweli chuma kimeondoka for good!
Nyie mnaoogopa hiyo possibility pole yenu!
 
Kujaza watu msibani haina maana unapendwa, kuna wabaya wako wanakuja kuhakikisha kweli umekufa au ni maneno ya watu.

All in all Rais wetu amefariki tumuombee huko aendako akapumzike salama
Hao adui zako watakuja kujipiga 🤳, hawa 👇 unafikiri ndio sampuli hiyo?
 
Usipate shida kushughulika na maneno hayo mawili,sababu moja halikai bila ya mwenzake. Ukweli ndiyo uhalisia wenyewe, ndiyo maana kwenye maana ya Ukweli unakuta ni kuafikiana na hali halisi, uhalisia huanza.
[emoji1545][emoji1545][emoji1545]Asante kwa mjadala mzuri nimejifunza mengi kwako ...BARIKIWA....!!!
 
Back
Top Bottom