Ngoja tuwekane sawa katika jambo hili, na tuwe waadilifu.
Hapa nagusia nukta mbili au tatu na nukta ya mwisho itakuwa ni nasaha kwangu na kwenu.
1. Kiimani hasa kwetu sisi Waislamu jambo hili ni jambo baya na limekemewa vikali sana, na kiistilahi tunaita KUOMBOLEZA(Kuomboleza ni miongoni mwa mambo manne ya kijinga,ambayo hayataisha mpaka Kiyama kinasimama). Kiimani tunaamini ya kuwa Mtu ni wa aidha motoni au peponi,na akifa anatakiwa kuzikwa haraka ili akaanze kuishi maisha mapya kaburini, kama mtu wa kheri basi kaburi ni katika bustani miongoni mwa mabustani ya Peponi, na kaburi ni katika mashimo miongoni mwa mashimo ya motoni. Kwahiyo kitendo cha kumchelewesha maiti kumzika ni kuzidi kumpa dhiki na kumtesa kama ni wa motoni, na kama ni wa kheri basi mnamchelewesha kwenda kupata mazuri yake,kama alitoa usia mapema basi mzigo wa madhambi unakiwa ni juu yenu na si juu yake. Hitimisho ni kuwa,ni wajibu wetu na ni jambo jema kuwahisha kumzika maiti,tena huwa bora zaidi kutomsafirisha.
2. Wasia, ni jambo la dharura sana kwa mtu makini, tena ukiacha wasia mzuri juu ya maziko yako yaweje,huwa bora zaidi. Ila si kila wasia hufanyiwa kazi.
3. Hapa lazima tuelezane ukweli, mtoa mada nina hakika hali wa shani (Hii ni dhaa ya hakika kabisa, kwayo inahukumu hili sababu imevuka kiwango cja uzani wa asilimia Hamsini),umeandika uzi huu au haya kwa sababu ya chuki yako juu ya mwenda zake, lakini swali la msingi ni , Je angekuwa amekufa kipenzi chako tena katika wadhifa huo wa mwendazake ungeyaandika haya au na wewe ungekuwa katika kundi la hawa ambao wako dhidi yako na mlengo wako ambao wewe unawaita wapigaji ?
4. Hii ni nasaha ambayo kwayo,nimeigusia hapo awali ya kuwa baada ya kumaliza nukta mbili au tatu inayofata ni nasaha kwangu,kwako mtoa mada na kwa wale wasio kuwa mimi na wewe. Nasema hivi "Hutosha mtu kuwa MUONGO kusema au kuandika juu ua kila anachokiona au kukisikia". kiasili haya si maneno yangu.
Ziada : "Hajutii yule aliyekaa kimya kwenye fitina/fitna au kila wa kala."