Tunautaabisha mwili kwa manufaa ya nani?

Tunautaabisha mwili kwa manufaa ya nani?

Kitu nilicho notice sisi wa Tz Thinking capacity yetu ni ndogo kuliko punje ya haladali. Tunahis kuuzururisha mwili wa marehemu ndo kuonyesha kua tunampenda na kumjali hata tuki muaga mwaka mzima hakuna utofauti wowote tutakao ulete iwe kwa marehemu au kwa taifa zaid zaid ni gharama kuongezeka na maisha kuzi kuwa tight maana baada ya hilo zoezi bidhaa zinawez kupanda bei ili kufidia pesa iliyo tumika but who cares???
 
Mkuu huu ni msiba wa aina yake, unalipata taifa letu kwa mara ya kwanza, kuondokewa na Rais aliyepo madarakani. Hivyo lazima kuwe na sintofaham za hapa na pale.

Lakini pia huyu ni Jemedari aliyekua anaahirisha baadhi ya sikukuu za kitaifa kuokoa matumizi na gharama zisizo na ulazima, sifikirii angekuwepo angeliafiki hili.

Kwangu kubwa na la hatari zaidi ni kutokuona kuzingatiwa kwa tahadhari za Covid kwenye hili zoezi, hasa kwa viongozi wetu...tunasahau mapema sana.
 
Kuna ratiba ndefu sana ya kuuaga mwili wa aliyekuwa rais wa Tanzania 2015-2021... Kwa ujumla wake ataagwa mara sita maeneo tofauti ya nchi ikiwemo Zanzibar iliyokuja kuchomekwa baadae kwa sababu za kisiasa
Msiba ni gharama kwa kila hatua na ni gharama zaidi kwa kila siku inayoongezeka kila siku ipitiyo bila kuzika...lakini zaidi kiimani ama kiroho si vema kuuhangaisha mwili uliokwisha tengana na roho labda tu iwe kwa maagizo ya mhusika
Safari ya kifo ni ndefu isiyo na kinyume ndio maana wafu hutolewa eneo alilofia, mochwari, nyumbani kisha kaburini... Ni safari ya njia moja... Ni kinyume cha mazoea kuutoa mwili mochwari na kuuanika siku nzima kisha kuurudisha mochwari tena na kuutoa tena na tena...

Watetezi wa hili wana hoja zao kama hizi
Dar kuaga ni mara mbili kutokana na wingi wa wakazi wake
Dodoma ni mji mkuu wa nchi alioupigania katika maisha yake hivyo si vizuri kuwaruka watu wa Dodoma
Mwanza ndio mkoa wa mji alikokulia
Geita na baadae Chato ndio nyumbani
Vipi kuhusu Zanzibar? Ni sehemu ya muungano , japo leo tayari kulikuwa na wawakilishi waliokuja kwa gharama za serikali
Kwa sasa ni matumizi , bajeti wanaijua wachache lakini huko mbeleni huu msiba unaweza kuja kuwa kashfa ya ufisadi
Kwa kila siku ya huu msiba kuna pesa inateketea
Per diem za viwango tofauti
Mafuta ya magari yanayohusika kwenye msiba
Malazi, chakula na vinywaji kwa waalikwa, wahudhuriaji, waombolezaji na wageni mbalimbali
Gharama za majukwaa mbalimbali, viti meza nk
Washereheshaji na watumbuizaji
Gharama za kuhifadhi mwili
Dharura nknk

Tunaweza kufanya mambo bila kujua mtazamo wake lakini isifike mahali tukakufuru kwa kuona kwamba hivi ndivyo inavyopaswa kuwa na zaidi kumbe kuna wapiga dili nyuma yake.

Hali ngumu ya maisha inawafanya baadhi kutumia misiba kama sehemu ya kujazia mashimo yao ya madeni, matumizi na mahitaji mbalimbali

Naweza kupigwa mawe kwenye hii post na wanufaikaji lakini huu... Wale wataosema msiba unabebwa na rambirambi za wapendwa wake. Na bajeti ya kitengo kwa nafasi yake kama mkuu wa nchi..lakini kuagwa mara sita sehemu tofauti za nchi kunaweza kuweka rekodi mpya.
Mungu akiamua ataukipanga ata pangua unaweza uka imagine kabisa mtu anaacha hospital ya taifa muhimbili Anaenda kufia Dispensary ya MZENA !!!!!!!......atakama anateseka nimipango ya Mungu huenda adhabu yake ndo imeanzia hapa kabla kuingia kabrini
 
Mshana uliona Moi alivyokuwa anapigishwa safari za Lee funeral na kubadilishwa Suit kila siku? Kuna tofauti y Hayati na hawa marehemu wetu
Nitafuatilia kisha nitatoa maoni yangu[emoji2839]
 
Nakuunga mkono sana! Tunajihangaisha zaidi na mwili-mfu kuliko mwili-hai. Mwili-mfu ni mavumbi tu, ni utupu. Mwenye nao kaondoka, hatuoni, hatusikii wala hahisi chochote!

Mwili-hai unabeba mtu halisi ambaye ni nafsi na roho yake. Huyo ndiye tumjali zaidi, na si mwili-mfu anaouacha.
Kuna ratiba ndefu sana ya kuuaga mwili wa aliyekuwa rais wa Tanzania 2015-2021... Kwa ujumla wake ataagwa mara sita maeneo tofauti ya nchi ikiwemo Zanzibar iliyokuja kuchomekwa baadae kwa sababu za kisiasa
Msiba ni gharama kwa kila hatua na ni gharama zaidi kwa kila siku inayoongezeka kila siku ipitiyo bila kuzika...lakini zaidi kiimani ama kiroho si vema kuuhangaisha mwili uliokwisha tengana na roho labda tu iwe kwa maagizo ya mhusika
Safari ya kifo ni ndefu isiyo na kinyume ndio maana wafu hutolewa eneo alilofia, mochwari, nyumbani kisha kaburini... Ni safari ya njia moja... Ni kinyume cha mazoea kuutoa mwili mochwari na kuuanika siku nzima kisha kuurudisha mochwari tena na kuutoa tena na tena...

Watetezi wa hili wana hoja zao kama hizi
Dar kuaga ni mara mbili kutokana na wingi wa wakazi wake
Dodoma ni mji mkuu wa nchi alioupigania katika maisha yake hivyo si vizuri kuwaruka watu wa Dodoma
Mwanza ndio mkoa wa mji alikokulia
Geita na baadae Chato ndio nyumbani
Vipi kuhusu Zanzibar? Ni sehemu ya muungano , japo leo tayari kulikuwa na wawakilishi waliokuja kwa gharama za serikali
Kwa sasa ni matumizi , bajeti wanaijua wachache lakini huko mbeleni huu msiba unaweza kuja kuwa kashfa ya ufisadi
Kwa kila siku ya huu msiba kuna pesa inateketea
Per diem za viwango tofauti
Mafuta ya magari yanayohusika kwenye msiba
Malazi, chakula na vinywaji kwa waalikwa, wahudhuriaji, waombolezaji na wageni mbalimbali
Gharama za majukwaa mbalimbali, viti meza nk
Washereheshaji na watumbuizaji
Gharama za kuhifadhi mwili
Dharura nknk

Tunaweza kufanya mambo bila kujua mtazamo wake lakini isifike mahali tukakufuru kwa kuona kwamba hivi ndivyo inavyopaswa kuwa na zaidi kumbe kuna wapiga dili nyuma yake.

Hali ngumu ya maisha inawafanya baadhi kutumia misiba kama sehemu ya kujazia mashimo yao ya madeni, matumizi na mahitaji mbalimbali

Naweza kupigwa mawe kwenye hii post na wanufaikaji lakini huu... Wale wataosema msiba unabebwa na rambirambi za wapendwa wake. Na bajeti ya kitengo kwa nafasi yake kama mkuu wa nchi..lakini kuagwa mara sita sehemu tofauti za nchi kunaweza kuweka rekodi mpya.
 
Sawa kabisa
Kusema kweli hii kitu ni pointless kabisa. Uongozi uliobaki wamedhihirisha kuwa nao bado ni malimbukeni tu.

Haiwezekani kufanya mikusanyiko mikubwa namna hiyo bila kujali uhalisia wa janga covid-19.

Watu tungeangalia shughuli kupitia kwenye TV na kusikiliza kwenye radio ingetosha. Hakukuwa na haha ya haya yote. Kwanza ni gharama kubwa tu zinatumika na zinaongeza mzigo kwenye kodi za wanaoitwa wanyonge.

Mimi kwangu haileti tofauti kuwa ameagwa na watu wengi au hajaagwa kabisa. Mtu akishakufa amekufa tu hata akiagwa na dunia nzima haimsaidii chochote.

Wangempumzisha tu tuendelee na maisha.

NB: In the end, all the people you know including you will die.
 
Tena ingependeza kama wangemzungusha kila mkoa ili kila mtanzania apate nafasi ya kumuaga mpendwa wetu. Nimeumia sana na huu msiba yani ni kama naota vile.
Above all kifo chake kimekuja ghafla sana mpaka ni ngumu kuamini.
Raha ya milele umpe ee bwana na mwanga wa milele umuangazie, apumzike kwa amani.

Sent from my TECNO BA2 using JamiiForums mobile app
 
Walificha habari za kuugua kwake ,sasa wanataka kutuaminisha kuwa alikuwa anapendwa ,kwa nini kipindi anaugua msiweke wazi ili wananchi kwa nafasi zao wafanye maombi na dua ajili ya Mgonjwa.

Kwa sasa haileti picha nzuri katika hali ya uwiano ,eti kuuaga Mwili mara huku mara kule, Mwili ushaachana na Roho..
 
Back
Top Bottom