Ni dhambi kuchora tattoo kwenye mwili

Ni dhambi kuchora tattoo kwenye mwili

john achila mukumwa

Senior Member
Joined
Jan 4, 2024
Posts
133
Reaction score
269
Ni dhambi kuchora tattoo kwenye mwili

Maandiko katika kitabu cha Mambo ya Walawi 19: 28: “Msichanje chale yo yote katika nyama ya miili yenu kwa ajili ya wafu, wala MSIANDIKE ALAMA MIILINI MWENU; mimi ndimi Bwana”.

Bwana alikataza watu kuchanjwa chale kwa sababu chale zote zinahusiana na ibada za wafu, au ushirikina.


Bwana hakuwahi kuwaagiza wana wa Israeli wanapopatwa na matatizo fulani au wanapohitaji kinga ya jambo fulani wachanjwe chale. Hizo zilikuwa ni ibada za kipagani, ambazo tunaona hapa Bwana anawaagiza wana wa Israeli wasizifuate hizo desturi. Bwana aliwaagiza kuwa tiba ya magonjwa yao ni kuzishika sheria zake, na siyo kwenda kujichanja mwilini.

Lakini pia aliwaagiza wasiandike alama zo zote katika miili yao (tattoo).

Watu wengi hawajui asili ya tattoo. Watu wa zamani walikuwa hawachori tattoo kwa lengo la urembo kama siku hizi. Watu wa zamani walikuwa wanachora tattoo kwenye miili yao kwa lengo lile lile kama la kuchanja chale, kwa ajili ya ibada ya nguvu za giza.

Ilikuwa ni ibada za miungu, na walikuwa wanafanya hivyo kufuata maagizo ya miungu yao, kuwa wanapotaka kupata jambo fulani, au kujikinga na hatari fulani, ni lazima wachore alama hizo katika miili yao.


Hizo zinaweza kuwa ni michoro ya aina fulani ya wanyama kama vile nyoka, ndege, au wakati mwingine majina fulani ya lugha zisizoeleweka, au alama za jua, au mwezi nk. Kwa sababu shetani ndiye aliyekuwa nyuma ya mambo hayo, basi kila aliyefanya hivyo alikuwa ananufaika kwa namna fulani na mambo ya kishetani.

Ni kama tu mtu aliyechanjwa chale au anayetembea na hirizi leo, anakuwa anatembea na pepo fulani linalomkinga dhidi ya mambo fulani yanayohusiana na anachokiamini.

Lakini miaka ilipokwenda mbele, watu waliwaona watu wanaojichora tattoo kuwa wanapendeza. Hivyo, pasipo kuchunguza asili ya lile jambo ni nini, nao pia wakaenda kuiga mioyoni mwao, wakidhani kuwa wanaweka urembo tu kwenye miili yao, kumbe wanaweka uchawi na mapepo kwenye miili yao, pasipo wao kujijua. Wanajiongezea roho fulani za yule adui katika maisha yao.

Kwa hiyo mwili wo wote wenye tattoo, tayari una pepo fulani ndani yake. Hii ni kwa sababu asili ya tattoo au chale siyo urembo wala fasheni, bali ni kinga fulani za kichawi.


Biblia imetuonya kuwa miili yetu inapaswa iwe hekalu la Roho Mtakatifu.
1Wakorintho 6:19: “Au hamjui ya kuwa mwili wenu ni hekalu la Roho Mtakatifu aliye ndani yenu, mliyepewa na Mungu? Wala ninyi si mali yenu wenyewe;
20 maana mlinunuliwa kwa thamani. Sasa basi, mtukuzeni Mungu katika miili yenu”.

Kumbuka kuwa hapo biblia haijasema miili ya wale wanaomwamini Bwana Yesu kuwa ni NYUMBA YA KAWAIDA, bali ni HEKALU. Hekalu ni tofauti na nyumba ya kawaida.

Kuna nyumba za aina nyingi, zipo za kulala wageni, nyumba za kuhifadhia mizigo, nyumba za kiofisi, nk. Lakini HEKALU ni nyumba maalum kwa ajili ya ibada tu.

Sasa nyumba yenye chale au yenye tattoo itakuwaje hekalu la Mungu? Tunaona hiyo?

Kwa hiyo, usichanje chale yo yote mwilini mwako. Kuchora tattoo ya aina yoyote ile ni kosa.

Kama ulijichora tattoo huko zamani, au ulichanjwa chale udogoni na sasa umempa Bwana maisha yako, hiyo ni vema. Ile roho nyuma ya hiyo tattoo imeondoka, lakini shetani bado atakuwa na visababu vichache vichache vya kukushitaki mbele za Mungu.

Hivyo, chukua uamuzi wa kwenda kuvifuta hivyo vitu ili shetani asipate sababu yoyote ya kukushitaki.

Makampuni yanatumia matangazo mbalimbali kujitangaza pamoja na bidhaa zao. Nawe, kama umejichora tattoo, mwili wako usitumike kuitangaza kazi za shetani, kwa sababu usipofuta tattoo, ni sawa na kampuni fulani ya matangazo inatangaza nembo au biashara yake
.

Hivyo, mpe Bwana maisha yako. Hata kama unapenda tattoo kiasi gani, Mungu hataki (Walawi 19: 28, 1Wakorintho 6:19-20). Usione aibu. Kuwa jasiri. Usiseme watu watakuonaje. Maisha ni yako binafsi, siyo ya hao wanaokuona. Siku ya mwisho, utaulizwa maswali ukiwa wewe peke yako, bila hao wanaokuona kuwepo. Na hukumu itatolewa juu yako wewe, siyo juu ya hao wanaokuona. Kama Mungu amekwishasema kuwa hataki tattoo, unatarajia hukumu gani?

Tafuta kanisa sahihi ya maombezi, ufute tattoo zote mwilini mwako. Alama zitabaki kama alama tu, kama kovu. Lakini hazitakuwa tena na connection yo yote na shetani.

Utakuwa umeuweka mwili wako wakfu kwa Mungu, ili autumie.
 
Makampuni yanatumia matangazo mbalimbali kujitangaza pamoja na bidhaa zao. Nawe, kama umejichora tattoo, mwili wako usitumike kuitangaza kazi za shetani, kwa sababu usipofuta tattoo, ni sawa na kampuni fulani ya matangazo inatangaza nembo au biashara yake.✍🏿
 
Ukiacha masuala ya kiroho, uhalisia wa maisha ni kwamba sekta nyingi rasmi za ajira bado zina miongozo mikali sana dhidi ya tattoo zinazoonekana wazi. Kuchora kunaweza kukufungia milango ya fursa nyingi za kiuchumi baadae.
 
Ninampango wa kuchora...

Ni nadharia tu kudhani tattoo ni dhambi.
 
Ni wapi Bwana aliwaambia wanamakonde au wamatumbi au wachagga wasichore miili yao?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom