Tunautaabisha mwili kwa manufaa ya nani?

Tunautaabisha mwili kwa manufaa ya nani?

Demi Nilikuona wazi kabisa hukufurahishwa na bandiko langu... Hata pamoja na hisia hizi kwamba nilimchukia marehemu ...lakini sasa hatumuongelei Magufuli tena, tunaongelea 'mwili wake' Mada yangu imejikita kwenye mwili uharibikao baada ya roho kuuacha
Nimefanya kazi mochwari mojawapo ya ethics za mochwari ni kuwatendea haki marehemu wote hata kama kati yao kuna adui yako mkubwa kwakuwa kilichopo pale si yeye tena bali ni jumba tupu liitwalo mwili

Kama ni jumba tupu sio mwili hai iweje useme tunautaabisha? Hauna hisia, hauumii popote.
Kuuzungusha watu wamuage ni kujiridhisha matakwa yetu sie binadamu, maiti haitambui chochote. Na kama marehemu anaona kinachoendelea huku duniani naamini hakasirika kwa tunachomfanyia kwasababu ni kwa upendo tu.
 
Mkuu mimi nimewaza nikashangaa watu hawana hata huruma na maiti, kuna haja gani ya kuaga dar mara mbili, dodoma, mwanza geita, mimi nadhani dar wangeaga mara moja, then Zanzibar ingawa sio lazima maana viongozi wote wa zanzibar walikua hapa, mwili usafirishwe kwenda chato ambapo wanafamilia wataruhusiwa kuaga then wazike, sasa ratiba ya kuaga mwili wiki nzima mwishowe maiti yenyewe itaoza jamani, nadhani hili jambo hata ndugu hawajalifurahia sema tu hawana namna
Kuna haja ndo mana watu wanajitokeza kusingemuwa na haja watu wasingeenda, subiri wakifa wanaokuhusu utafanya maamuzi hata ya kuwazika siku hiyo hiyo la huyu halikuhusu kwahyo huna haja ya kujiuliza
 
Kama ni jumba tupu sio mwili hai iweje useme tunautaabisha? Hauna hisia, hauumii popote.
Kuuzungusha watu wamuage ni kujiridhisha matakwa yetu sie binadamu, maiti haitambui chochote. Na kama marehemu anaona kinachoendelea huku duniani naamini hakasiriki kwa tunachomfanyia kwasababu ni kwa upendo tu.
Ok sawa sawa ngoja tukubaliane kutokubaliana ndio njia sahihi ya mjadala
 
Mshana Jr tangu lini na wewe unaanza kuwa na wivu wa kipuuzi namna hii na maiti?

Hii ni sherehe ya Mwisho ya JPM. Ana ndugu, jamaa na marafiki. Waacheni waage.

Unapoongea hivi unawaumiza na kuwakwaza.

Ungefuta huu uzi tafadhari.
JF ya sasa uwezo wa kujadili hoja umepungua sana... Hoja hujibiwa kwa hoja..kinyume cha hapo ni mahoka
Kwasasa kwenye hoja nyingi kinzani, malumbano hutoka kwenye hoja na kuhamia kwenye vioja, vijembe na kejeli ama la kumjadili mtoa hoja....!!!
 
Kuna haja ndo mana watu wanajitokeza kusingemuwa na haja watu wasingeenda, subiri wakifa wanaokuhusu utafanya maamuzi hata ya kuwazika siku hiyo hiyo la huyu halikuhusu kwahyo huna haja ya kujiuliza
Wanasahau kwamba kiongozi ni mtu wa watu, na watu wapo pande mbali mbali wanataka kushuhudia.
Kila mtu ana principles zake linapokuja suala la msiba...serikali haifati imani ya mtu bali inaangalia kile kinachofaa.

Sent from my Infinix X5515 using JamiiForums mobile app
 
Mshana Jr I agree with you
Yaani wameamua kuiba hela na kusambaza Corona huko zenji kwa kina Juse waliovunjwa vunjwa Miguu , ndo wanampeleka!!! Very unfortunate

Sisi tushamsamehe marehemu hila unafiq tusiupe nafasi.
 
JF ya sasa uwezo wa kujadili hoja umepungua sana... Hoja hujibiwa kwa hoja..kinyume cha hapo ni mahoka
Kwasasa kwenye hoja nyingi kinzani, malumbano hutoka kwenye hoja na kuhamia kwenye vioja, vijembe na kejeli ama la kumjadili mtoa hoja....!!!
Hoja yako haiwezi jadiliwa ipasavyo maana mambo ya kiroho kuhusu maiti ni wewe na wachache wenzako mnayaelewa. Yamekaa kichawichawi zaidi.
Usingetaja mwili wa mtu ambae una chuki nae..eti unamuonea huruma.

Sent from my Infinix X5515 using JamiiForums mobile app
 
Kitu nilicho notice sisi wa Tz Thinking capacity yetu ni ndogo kuliko punje ya haladali. Tunahis kuuzururisha mwili wa marehemu ndo kuonyesha kua tunampenda na kumjali hata tuki muaga mwaka mzima hakuna utofauti wowote tutakao ulete iwe kwa marehemu au kwa taifa zaid zaid ni gharama kuongezeka na maisha kuzi kuwa tight maana baada ya hilo zoezi bidhaa zinawez kupanda bei ili kufidia pesa iliyo tumika but who cares???
Wivu hadi kwa maiti???? Yani even after his death bado mnaweweseka nae? Bado mnateseka tu? Kweli hakuna kama JPM RIP
 
Mshana Jr I agree with you
Yaani wameamua kuiba hela na kusambaza Corona huko zenji kwa kina Jude waliovunjwa vunjwa Miguu , ndo wanampeleka!!! Very unfortunate
Mshana Jr angeongelea kuhusu kuiba pesa na kusambaza Corona angeeleweka. Hoja yake imejikita kwenye mwili kuumia, anaona huruma sana.

Unachokubaliana nae sio hoja yake.

Sent from my Infinix X5515 using JamiiForums mobile app
 
Mungu akiamua ataukipanga ata pangua unaweza uka imagine kabisa mtu anaacha hospital ya taifa muhimbili Anaenda kufia Dispensary ya MZENA !!!!!!!......atakama anateseka nimipango ya Mungu huenda adhabu yake ndo imeanzia hapa kabla kuingia kabrini
Adhabu yako wewe itaanza ukiwa bado uko hai
 
Walificha habari za kuugua kwake ,sasa wanataka kutuaminisha kuwa alikuwa anapendwa ,kwa nini kipindi anaugua msiweke wazi ili wananchi kwa nafasi zao wafanye maombi na dua ajili ya Mgonjwa.

Kwa sasa haileti picha nzuri katika hali ya uwiano ,eti kuuaga Mwili mara huku mara kule, Mwili ushaachana na Roho..
Wewe kaa kwako hakuna anakuita wala kukulzimisha kushiriki
 
Tunachojisahaulisha ni kuwa huyu hakuwa tu John Magufuli, alikuwa Rais wa JMT, Tena Rais aliyekufa akiwa madarakani, je tumelifikiria hilo?

Hoja ambayo ningekubaliana na mtoa mada ni kufuja hela, Ila sio "kuuchosha mwili", unachoshaje mtu aliyekufa?
 
Hoja yako haiwezi jadiliwa ipasavyo maana mambo ya kiroho kuhusu maiti ni wewe na wachache wenzako mnayaelewa. Yamekaa kichawichawi zaidi.
Usingetaja mwili wa mtu ambae una chuki nae..eti unamuonea huruma.

Sent from my Infinix X5515 using JamiiForums mobile app
Demi huna haja ya kupanic zaidi nadhani tumeshafunga mjadala kwenye hili...kwakuwa hakuna kitakachobadili uhalisia wa kile nilichoandika
 
Haya ndio majibu kwenye mjadala huu ambao swali hoja kwenye kichwa cha habari halijajibiwa
Iko hivi
Tanzania haijawahi kupata msiba wa kiongozi ngazi ya rais akiwa madarakani tangu uhuru, hivyo ukiachilia mwongozo wa katiba hakuna kingine tujuacho...kwahiyo kwa mara ya kwanza ile practice kwenye vfungu vya katiba ndio inafanyiwa kazi sasa

Hiki kitu kimetokea bila maandalizi ya kutosha(kawaida kifo hakina maandalizi) na hulka ya mwendazake aligeuza mfumo mzima kuufanya ni wake na ndio mwamuzi wa mwisho kwenye kila kitu.. Sasa hapa kuna mambo mengi sana ya kuyaweka sawa, kuna ya lazima na kuna ya muhimu lakini yote yanahitaji muda na muda uliopo hautoshi
Sasa hii ratiba ndefu ya kuaga mwili ni kwa maslahi ya nani? Jibu ni moja tuu... CCM...Ni wakati huu wananchi wakiwa busy na kuaga mwili kwa maelfu huko ndani nyuma ya pazia mambo yanaendelea tena kwa kasi kubwa lakini pia kwa umakini wa aina yake... Wana sacrifice kuuhangaisha mwili ili kudaivate attention ya jamii
CCM inajifahamu position iliyo nayo mbele ya macho ya jamii, IMESHAKATALIWA kitambo.. Uchaguzi huu kama sio wizi mkubwa wa kura ingekuwa Leo hii tunaongea mengine
Sasa ni muhimu sana kupanga timu za ushindi 2025.. Na wakati huo ni sasa, kipindi hiki cha maombolezo...ni katika hili ndio kila timu inajipanga kivyake na kufanya michakato kuwa migumu zaidi

Ni the race against time... Ni kwenye hii kundi lililokabidhiwa msiba linafanya yake pia.. Tutakuja kupeana mrejesho baadae

Kumbe ni mambo ya kisiasa sio tena kuuchosha mwili? Ona sasa hoja yako hata wewe mwenyewe huielewi.
Ungefafanua toka kwanzo kuwa kuna mambo mabaya yanafanyika nyuma ya pazia ambayo sio sahihi. Tungejibu hoja yako katika muelekeo huo.
Unachanganya mambo halafu unatulaumu hatujui kujibu hoja.
 
Mshana Jr usijifananishe naye kakuzidi kila kitu
Ha haa maskini. Nini labda ndugu? Hapa hatupo kwenye mashindano nani kamzidi nani kitu flani.
Ni wewe unayefanana nae maana unakubali chochote anachokisema. Ni kweli siwezi fanana nae kwa chochote kile na sijawahi kutamani kufanana nae.

Ni kama vile unataka kuleta chuki hapa, mimi najadili bango lake. Wewe tamani kufananae nae inatosha.
 
Back
Top Bottom