Tunauomba uongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ukarabati wa uwanja wa Jamuhuri mkoani Morogoro ili mechi za Ligi Kuu zirudi kuchezwa mkoani hapo

ToniXrated

JF-Expert Member
Sep 21, 2022
1,135
2,976
Amani iwe nanyi.

Mkoa wa Morogoro ni miongoni mwa mikoa katika ardhi ya nchi ya Tanzania yenye wapenzi wengi wa Soka. Wachezaji wengi mahiri wametoka katika mkoa wa Morogoro. Ni muda sasa umepita toka dimba la Jamuhuri lilipofungiwa kutumika kwa michezo ya Ligi Kuu nchini Tanzania, kutokana na kushindwa kukidhi ubora wa viwango.

Ni aibu sana kuona uongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kushindwa kukarabati eneo la uwanja (Pitch) kwa kuweka walau nyasi bandia kama ilivyofanywa katika uwanja wa Majaliwa uliopo Ruangwa Mkoani Lindi. Hakika CCM haiwatendei haki mashabiki wa soka mkoani Morogoro.

Aidha niiombe Bodi ya Ligi kuufungia tena uwanja wa Manungu uliyopo Turiani ,ambapo unatumiwa na wakata miwa Mtibwa Sugar kutokana na kuwa na uwanja mbovu. Nashangaa kwanini uwanja wa Mtibwa umeruhusiwa kuchezewa Ligi Kuu ya NBC msimu huu.

Uwanja wa Mtibwa Sugar una matuta matuta na nyasi mbovu kabisa. Ni wakati sasa TFF ikisaidiana na Bodi ya Ligi itaje aina ya nyasi halisia zinazopaswa kupandwa katika viwanja, mfano wa zilizopo uwanja wa Mkapa au Azam Complex.

Kama uongozi wa uwanja utashindwa kupanda nyasi zile, basi iweke nyasi bandia tu kama za uwanja wa Majaliwa uliyopo Ruangwa mkoani Lindi na kama watashindwa kati ya hayo mawili basi uwanja usitumiwe katika mechi za Ligi kuu ya NBC.

Ligi yetu sasa hivi inafuatiliwa barani Afrika na Duniani kwa ujumla, itakuwa aibu sana watu wakiona tunashindwa kuwekeza katika miundo mbinu ya viwanja. Ni bora hata Ligi Kuu ikachezwa kwenye viwanja vitano ila viwe ni viwanja vyenye hadhi ya kimataifa.

Viwanja ambavyo naona vina uwanja mzuri ni uwanja wa Benjamin Mkapa, Azam complex, Liti, Majaliwa na Uwanja wa uhuru tu. Viwanja vingine ni majanga.

Mheshimiwa Rais Mama Samia Suluhu tunakuomba utenge fungu kupitia Wizara yako ya michezo na Serikali yako ya Chama Cha CCM ili ikarabati viwanja mnavyovimiliki. Soka sasa hivi ni ajira kwa vijana na mwamko wa upenzi wa mchezo wa soka ni mkubwa sana. Tafadhali rekebisheni kwanza hivi viwanja tu viwe na hadhi ya kimataifa kisha ndiyo muhamie kwenye majukwaa n.k.
 
Back
Top Bottom