mwanamwana
JF-Expert Member
- Aug 1, 2011
- 1,076
- 4,113
Nianze kwa kumnukuu Hayati Mwalimu Nyerere...
Inapotokea vipindi vya uchaguzi wagombea wakiwa wanatafuta kura, pamoja na sera nzuri za kujiuza wanazokuwa nazo, pia huweza kutumia njia nyingine mbalimbali za kusaka kura. Sababu hizo zinaweza kuwa ukabila, udini, ukanda au jinsia. Wanaweza kutafuta kura kwa kutumia ukabila au kutafuta kura kwa kutumia udini.
Kufatuta uongozi kwa kutumia udini au ukabila unagawa watu. Kazi ya uongozi ni kujenga watu kuwa kitu kimoja ambapo wanaweza kushirikiana kwa shughuli mbalimbali za kimaendeleo bila kuhisi ubaguzi wa namna yoyote.
Kiongozi yeyote anayehubiri ukabila, ukanda au udini ili kupata kura ni mtu hatari sana katika taifa na hapaswi kupewa madaraka yoyote.
Tanzania ina makabila zaidi ya 120, hivyo tunapochagua viongozi tuangalie sera zao kama zinauzika na zinaweza kusukuma gurudumu la maendeleo ya nchi kwa ujumla.
Wakati wa uchaguzi, wagombea wengi hasa nafasi za juu huongeza nafasi za kutumia majengo ya dini na kushiriki shughuli nyingi za kidini ili kuweza kujiuza. Tuwe makini na kile wanachokisema na ku-digest yale yote yasiyo na chembe ya ubaguzi.
Kuna wale viongozi wanaohubiri ukanda, kwamba sasa ni zamu ya labda Kaskazini kutoa Rais etc etc. Hawa lengo lao linakuwa si zuri zaidi ya ubaguzi wa kikanda na kugawa wananchi.
Kuna wagombea wanaohubiri JINSIA, kwamba mkimchagua mwanamke hawezi kutimiza majukumu yake ya kiuongozi kutokana na wanawake wengi labda kuwa na majukumu ya kulea familia etc. Uchaguzi wa Ubunge jimbo la Shinyanga Mjini, Mgombea wa CHADEMA alilalamika kubaguliwa na mgombea wa CCM, Patrobas Katambi kuwa msimchague mwanamke kwasababu anaingia siku zake hivyo hawezi kuleta maendeleo.
Ubaguzi wowote wakati wa uchaguzi ni mwiba mkubwa kwa maendeleo ya demokrasia, huweza kupelekea kutompata kiongozi sahihi na hata kupelekea machafuko kuanzia ngazi ya chini na hata nchi kwa ujumla. Majirani zetu Kenya chaguzi zao tumekuwa tukiona zikiendeshwa kwa misingi ya ukabila, ambapo makabila matatu (Wajaluo, Kikuyu na Kalenjin) ndiyo yenye nguvu.
Ubaguzi ni adui wa utu na unapaswa kupingwa kwa nguvu zote wakati wote na mahala popote
Je, chaguzi ulizoshiriki ni jambo gani mgombea alifanya ukaona ni ubaguzi?