Tunaomba Serikali ipige marufuku kujitolea vijana tupate ajira za kudumu kupitia Utumishi

dav_

Senior Member
Jul 15, 2023
113
389
Husika na kichwa cha habari hapo juu.

TUNAOMBA serikali yetu sikivu ipige marufuku kujitolea ili vijana tupate ajira na pia kujitolea ni upendeleo nafasi hazipo wazi na mpaka uwe na connection.

Pia tunaomba ajira zote za kudumu kwenye mamlaka ya serikali ndogo (local government) wizara, taasisi zote, idara zinazojitegemea na wakala wa serikali, Bunge, mahakama, takukuru, tra, police na ajira yoyote ya serikali zisimamiwe na sekretariet ya ajira katika utumishi wa umma (psrs). Yani kazi yoyote ya kudumu mchakato upitie utumishi ili kuepusha upendeleo na undugu.

Pia tunaomba serikali ifanye maboresho na kushughulikia changamoto za utumishi kama ni kuwaongezea bajeti au rasilimali watu wafanye hivyo ili mchakato uwe rafiki wa haki na muda mfupi.

Pia tunaomba kanzidata(database) ya utumishi itumike ipasavyo na kuhusu matokeo ya usahili wa mahojiano kuwa wazi ili kuepusha mianya ya kupitisha watu. Kama kanzidata ya waliofaulu usahili wakakosa nafasi basi itumike kwa uwazi na kwa haraka sio kazi zinatangazwa Kada zile zile kila siku.

Tumeshuhudia vijana maskin wasio na connection wakipata kazi kupitia utumishi.

Naomba kuwasilisha.
 
Connection muhimu mkuu, tafuta connection

Hayo mawazo unayoyasema hayawezi kufanyiwa kazi yakaleta tija

Hata ajira za ualimu na kada ya afya zimejaa connection, rushwa nk

As long as hiyo kazi ya kuchagua na kutype majina wanafanya watu basi connection is inevitable
 
Naunga mkono hoja
Uhuni wa kujitolea ni kichaka cha watu kupenyezwa kinyemela serikalini
 
Na wale wanaopelekwa na TAESA?
Hivi hapo ukiambiwa ukajitolee pale BOT utakataa kwa kuwa utakuwa umewabania wenzio?
 
Back
Top Bottom