Ombenichelsea

JF-Expert Member
Apr 11, 2013
728
1,014
Haya yakizingatiwa angalau yatasaidia kuboresa mazoezi ya usaili yanayoendeshwa na Utumishi:

1. Katika upande wa mwombaji Waboreshe utoaji wa taarifa kama kuitwa, matokeo, ratiba na mabadiliko yoyote kupitia sms kwa sababu taarifa wanazotoa kwenye website na mifumo inaweza kukwamishwa na mtu kutokuwa na intaneti. Pia kuwe na notifications kwe mfumo ua ajira, notifications zinaonesha kila kinachoendelea.

2. Mfumo uweze kuonesha ajira zinazosubiriwa, zilizopita, n.k. katika majedwali tofauti. Hii itasaidia mwombaji kufuatilia kwa umakini bila kukosea kama ameitwa au la ili asichanganye au kusahau ajira yoyote aliyoomba

3. Usajili ulipaswa kufanyika kila mkoa kulingana na wahusika walioomba kama wanapatikana. Na kama itakuwa ni ngumu, basi saili zifanyike katika kanda zote nchini. Hii itasaidia watu kumudu gharama za kusafiri na kufanya usahili.

4. Kuwe na machine ya utambuzi kwa namba za kutoka NIDA. Kutokana na changamoto mbalimbali za waombaji kutokuwa na vitambulisho au nyaraka za utambulisho, mwombaji anaweza kutumia namba ya NIDA kukamilisha utambulisho wake kwa sababu ni njia ya halali na ya kuaminika itakayo ondoa usumbufu katika zoezi la ukaguzi.

5. Waombaji wajulishwe matokeo ya kila hatua ya usahili hata usaili wa mahojiano kwa wakati. Kuna kipindi usahili unaweza kufanyika lakini matokeo yanatoka kesho yake. Napendekeza matokeo yatoke ndani ya siku moja kwa hatua zote za usahili. Hii itaepusha gharama za kuendelea kusubiri kutokana na wengi wao kusafiri kutoka mbali na makazi yao.
 
Pia Kuna baadhi ya coz zimekosa ajira wajaribu ziunganisha kwenye baadhi ya post za ajira mfano waliosoma rural development Hawa mpk walilalamikaga ndo wakachomekwa kwenye ajira za Maendeleo ya jamii
 
Wakiweza kufanya saili Kila mkoa watakua wamecheza kama Pele magharama ya Kanda yanawakosesha watu haki zao aisee walau kwa Kila mkoa itakua poa sana
 
Back
Top Bottom