SoC02 Tunahitaji majukwaa ya kukuza fasihi ya Kiswahili

Stories of Change - 2022 Competition

MAKA Jr

JF-Expert Member
Nov 17, 2016
256
185
shaaban-books-data (1).jpg

Picha. Chanzo: The Citizen (12/08/2022)

UTANGULIZI

Je, hatuwezi kutumia barua, insha, makala, hadithi, mashairi, tamthiliya, na riwaya za Watanzania katika kufanya utafiti wa masuala kadhaa yenye mustakabali muhimu kwa Taifa letu? Je, mtoto mdogo wa Shule ya Msingi au Sekondari hawezi kutoa wazo jipya kupitia hadithi, insha, au mashairi lenye mchango kwa Taifa?

Kama Taifa tunahitaji kupanda mbegu za Fasihi ya Kiswahili ili tuvune utambulisho wa kuwa Nchi Muasisi wa lugha ya Kiswahili Afrika na duniani kwa ujumla.

Kuna haja ya kuanzisha Majukwaa ya kushindanisha kazi za fasihi ya Kiswahili kuanzia hatua ya chini hadi ya juu kabisa.

Kama Tanzania tunaweza kuwa na 'Bongo Star Search' ya mziki, je hatuwezi kuwa na 'Bongo Star Search' ya uandishi wa hadithi au mashairi nchi nzima ili kukuza fasihi yetu ya Kiswahili?
Shaban Robert mwingine hawezi kuzaliwa kama hakuna maandalizi. Maandalizi ya kuzalisha Shaban Robert wengi yanapaswa kuanza leo.
Nchi zilizopiga hatua kifasihi zilianza kuwa na majukwaa ya kukuza uandishi kazi za fasihi. Nchi kama Marekani na nchi nyingine za Ulaya zina majukwaa kama haya.

Kwa sasa, Afrika na Dunia kwa ujumla zinavutiwa sana na Kiswahili. Na Fasihi yetu inaendelea kupendwa siku hadi siku. Ukuaji huu unahitaji majukwaa madhubuti ya kuendeleza Fasihi ya Kiswahili.

SABABU KUU TATU (03) ZA UANZISHWAJI WA MAJUKWAA YA KUKUZA KAZI ZA FASIHI
Msukumo wa ukuzaji wa Fasihi ya Kiswahili Tanzania kunatokana na maendeleo ya kasi ya Kiswahili barani Afrika na duniani kwa ujumla.

Zifuatazo ni sababu kuu tatu za kuanzishwa majukwaa ya kukuza kazi za Fasihi ya Kiswahili:

01. Kukua kwa lugha ya Kiswahili
Sababu ya kwanza ni kukua kwa lugha ya Kiswahili ambako kunapaswa kwenda sambamba na uzalishaji mkubwa pia wa fasihi utakaokidhi mahitaji ya ndani na nje ya Tanzania. Hali iko wazi kabisa kuwa idadi ya wanaozungumza lugha ya Kiswahili inazidi kuwa kubwa kila kukicha. Hadhira iliyokuwepo wakati akina Shabani Robert na wengine wanaandika, kwa mfano, sio sawa na hadhira ya sasa. Japo kazi zao ni tunu kwa Taifa letu lakini bado tunahitaji uzalishaji mkubwa zaidi ili walaji waliokuwa wengi sasa waweze kutosheka. Ni hadhira kubwa inayohitaji wazalishaji wengi pia.

02. Kuibuka kwa watu, mashirika, taasisi, na nchi mbali mbali zinazotumia Kiswahili

Sababu ya pili ni kuibuka kwa watu, mashirika, na taasisi mbali mbali za kimataifa ambazo sasa zinaanza kutumia Kiswahili kama njia ya kuwafikia wadau wao ama wateja wao kwa kupitia kazi zao mbali mbali. Leo hii, Kiswahili kimetambulika na Umoja wa Afrika (AU) na Umoja wa Mataifa (UN) ambapo sasa kila Julai 07 ni Siku ya Kiswahili duniani. Haya ni maendeleo makubwa ya Kiswahili. Pamoja na Kiswahili kufundishwa kwenye Vyuo Vikuu mbalimbali duniani, pia siku hizi ni jambo la kawaida msanii wa muziki kutoka nje ya Tanzania kuandika nyimbo na kuimba kwa Kiswahili kwa sababu anajua kuna wateja ama mashabiki wengi wa Kiswahili watakaomsikiliza. Hata filamu ni hivyo hivyo. Kuna majirani ambao maigizo yao mengi yalikuwa yamejikita katika kutumia lugha zao za asili au Kiingeraza, lakini sasa wanaamua kutumia Kiswahili kwa sababu hadhiara ya Kiswahili ni kubwa Afrika Mashariki kuliko hadhira ya lugha nyingine yoyote katika eneo hili. Kwa kifupi, kila sekta nje na ndani ya Tanzania inaona Kiswahili kama fursa ya kipekee katika kufanikisha shughuli zao. Redio na Televishenii za Kimataifa nazo haziko mbali na fursa ya lugha ya Kiswahili. Sasa hivi zinazidi kuja kwa kwa kasi tofauti na zamani. Zimefika mbali zaidi na kufungua vituo vyao vya televisheni kwa lugha ya Kiswahili. Je, sisi bado hatuyaoni haya? Haya yote yatatufanya tuonekane ni wenye lugha kwa kujikita zaidi katika uzalishaji mkubwa wa fasihi ya Kiswahili.

03. Ufundishwaji wa Kasi wa lugha ya Kiswahili nje ya Tanzania

Sababu ya tatu ni kufundishwa kwa kasi kwa lugha ya Kiswahili nje ya Tanzania. Hii ni mbali na matumizi tu ya lugha ya Kiswahili, lakini pia uhitaji wa matumizi yanaongezeka kwa majirani zetu kila siku. Kwa mfano, hivi karibuni nchi kadhaa kama vile Uganda na Afrika Kusini zimechukua hatua ya kuanza kufundisha Kiswahili kwenye shule zao. Unapoona nchi zaidi ya tatu au nne zinaitangaza lugha fulani iwe lugha rasmi, ujue huo ndio mwanzo wa kukua kwa lugha yenyewe. Hali hii pia imeambatana na kasi ya kuongezeka kwa walimu wa lugha ya Kiswahili wanaohitajika kwenda kufundisha nchi za nje wakiwemo majirani zetu. Yote haya yanahitaji chombo madhubuti cha kusimamia uendelezaji wa Kiswahili kama lugha ya Afrika Mashariki ikiwemo kazi ya kuzalisha kazi za fasihi kwa wingi na kwa ubora. Ni wazi kuwa jamii isiyo enzi fasihi yake haiwezi kuwa na ubavu wa kupambana na kulinda utamaduni wake. Hatua mbali mbali za wasomi wa jamii husika zikichukuliwa kimadhubuti, bila shaka jamii hii itadumisha utamaduni wake kwa sababu itakuwa kwenye vitabu na kuifanya jamii ipende kusoma vitabu. Kuwepo kwa chombo kitakachowakutanisha waandishi kutaimarisha jamii na jamii na mashirika yake kuamini kuwa kile chombo ndicho msingi wa maisha na utamaduni wetu.
Tunao wahitimu wengi wa fasihi na wana mchango mkubwa, lakini ukweli uliopo hapa ni kwamba bado tuko nyuma kifasihi na jamii yetu inakua kwa kasi kubwa na hatuipi kinachostahili kutokana na kasi yake ya ukuaji.

HITIMISHO
Kwa kipekee, nawapongeza sana JAMII FORUMS kwa kuanzisha mashindano ya 'STORIES OF CHANGE'. Huu ni mwanzo mzuri sana. Tunategemea kuona wadau wengine wanajitokeza zaidi ili kuanzisha mashindano mengi ya namna hii. Kwa mfano, kama mashindano ya 'STORIES OF CHANGE' yana gharama ya shilingi milioni 50, je, hatuwezi kupata wadau wengine wakawekeza shilingi milioni 150 zitakazowezesha kuandaa mashindano kama haya kwa shule za Msingi, Sekondari, na Vyuo? Mimi naona inawezekana. Hata kama yasipofanyika kila mwaka, yanaweza kufanyika kila baada ya miaka kadhaa. Kongole kwa JAMII FORUMS. Hakika njia mmetuonyesha. Kazi iliyobaki kwetu ni kuifuata na kuleta mabadiliko katika fasihi yetu ya Kiswahili na kujidhirisha kuwa sisi ndio Waasisi wa Kiswahili Afrika na duniani. Wakati watu sekta ya michezo wanahaha huku na kule kutafuta vipaji, JAMII FORUMS nao wamefungua njia ya kutafuta vipaji vya uandishi wa fasihi ya Kiswahili kutoka kila kona ya nchi hii. Tuwaunge mkono.

Rejea:
[Picha] ]COVER: Shaaban Robert: Father of Kiswahili literature (12/08/2022)
 
View attachment 2321662

Kazi nzuri sana mkuu! Majukwaa ya kukuza na kutangaza kiswahili yaongezeke, ila lugha ya kufundishia iendelee kuwa kiingereza!
 
Back
Top Bottom