Tumpe Rais Kikwete heshima yake

Tumpe Rais Kikwete heshima yake

Naomba tumsamehe huyu jamaa. Inaonekana bado anaishi enzi za "Zidumu fikra sahihi za mwenyekiti wa ....."!!! Hivi kama ingewezekana, wana CCM wenyewe wangeweza kusema hivyo sasa hivi? Kwani hata fikra zenyewe sizioni, ukiachia mbali hilo suala la usahihi.

Zilizotakiwa zidumu ni "fikra sahihi" na si zinginezo ambazo si sahihi. Ndicho tunachokiona leo zile sahihi zinakumbukwa na kupigiwa mfano na wanazuoni wa ndani na nje ya nchi!!
 
Lakini kama serekali imeshindwa kutimiza ndoto za walioichagua kuna haja gani ya kubaki madarakani pasi kujiuzulu. Maana serikali inaajiriwa na wananchi sasa kama wananchi hawaoni uwajibikaji wake hakuna faida ya serikali hiyo kubaki madarakani Bwana Masoud.
 
Bwana Masoud ni mmoja ya wazee waliompigia makofi kikwete wakati wa mipasho time. Na cha kushangaza hadi sasa hachagundua kuwa rais wake alichemka!
 
Hivi Masoud, unajua maana ya kumvunjia heshima mtu? Unataka kunikumbusha wabunge wa zamani akina Simpasa, waliosema wabunge wasipewe changamoto kwani ni watukufu. Acheni udikteta...ziacheni fikra huru zizungumze.
 
kwangu mimi naamini maneno yale aliyoyatamka JK, ingekuwa ni Rais wa South AFRICA, Kesho yake kusingekalika, kungewaka moto, hata ingekuwa Kenya...anamatusi sana huyu Mkwere, ingekua yeye kaambiwa maneno yale unadhani angevumilia.
 
Mkuu Masoud, Upo right kabisa, heshima kitu cha bure...baadhi ya watu hawana heshima au malezi mazuri, huwezi kumuongelea Mkuu wa nchi kama unaongea na walevi BILICANAS. Licha ya kuwa tunatofautina na wenzetu wa chama tawala, haimaanishi kuwa tuwakosee heshima pale wao tunapohisi wamefanya hivyo, zaidi ya sisi kuonyesha uungwana wetu kwa watu tukausuta ujinga na uongo wao, viongozi wazuri wa upinzani siku zote huwa kama "mbwa wa kipofu", kuelekeza njia sahihi kwa bwana wake na kuokota alichoangusha. Alichotakiwa kufanya Mbowe si kutoa maneno ya kilevi "eti aondoke ikulu", huu wazimu. Angewaambia wafanyakazi na wananchi wamuondoe ikulu Kikwete maana wao ndo waliomuweka eti!
 
Mkuu wa nchi ana haki ya kutukana waliomchagua?
 
Junius
Mkuu wa nchi yupi unayemwongelea yule anaye chekacheka kama ni huyo mbona alishajivua heshima zamani yuko uchi, na wafusi wa CCM siku zote huwa kama 'mbwa koko' wanaookoteleza makombo ya mabwana zao kina Makamba wanaowatuma na kujikomba komba kama unavyofanya, bila kufanya hivi watoto wenu hawaendi choo, this is special respond to your post above.
 
Mkuu wa nchi ana haki ya kutukana waliomchagua?
Unajuwaje kama TUCTA wamemchagua Kikwete?
Wapi "wananchi" wametukanwa na Kikwete?
Kuwaambia ukweli kuwa wanawapotosha wafuasi wao kwa kuwa mazungumzo kati yao na serikali hayajafikia mwisho, na kuwa hakukuwa na haja ya kufanya mgomo,alikosea? acheni ushabiki...ukweli siku zote uwe ukweli tu.
 
Mbona sioni Kikwete alipotukanwa zaidi ya kuambia anayostahili. Hata hivyo hastahili heshima ya ukuu wa nchi
 
Unajuwaje kama TUCTA wamemchagua Kikwete?
Wapi "wananchi" wametukanwa na Kikwete?
Kuwaambia ukweli kuwa wanawapotosha wafuasi wao kwa kuwa mazungumzo kati yao na serikali hayajafikia mwisho, na kuwa hakukuwa na haja ya kufanya mgomo,alikosea? acheni ushabiki...ukweli siku zote uwe ukweli tu.
Sasa hata kama hawakumchagua,lakini yeye ni Rais wao! so,alistahili kuwatukana?
Kuna njia za kistaarabu kwa mkuu wa nchi kuongea na wananchi,hiyo njia aliyetumia ni njia Potofu
 
Nahisi mtoa mada ni mmoja wa wale waliojiita eti ni wazee wa dar es salaam. Rais kikwete alijikosea heshima mwenyewe na asitafute mchawi, huwezi kutukana watu wanaokulipa mshahara alafu useme umekosewa heshima. Tatizo la watawala wa Tanzania wakati wanatafuta madaraka wanyenyekevu kweli lakini once wako ofisini wanageuka mbogo.

Rais kikwete lazima atambue kwamba kaajiriwa na watanzania ambao lazima awatumikie.
 
Ngoja tumfungue kichwa huyu bwana, Hizo sh.315,000. ilikuwa ni siri kati ya kamati husika haikutatiwa kutoka nje kabla ya kukubaliana,yeye alitoa nje kwa hiyo serikari ilikiuka masharti ya vikao vya TUCTA na Serikali.Na aliyesema hadharani ni nani?na nani alaumiwe kama si JK. Je aliongerea swala la MAFAO YA UZEENI?Ambayo ndio kilio kikubwa cha Wafanyakazi hao?Muulize kwa nini hakuongerea hilo? Kwa nini hajawahi kuwakemea mafisadi kwa suraaliyoionesha siku ile ya kuwakemea TUKTA Uongo mwingi aliouonesha wewe unamsapoti kwani wewe ni kibaraka wake? Anavyodai kuwa wafanyakazi tunaodai hakizetu tusimpe kura ,wewe kama muelewa angalia tanzania inawafanyakazi wangapi na wasiowafanyakazi wangapi,ukiangalia hilo pima sentesi hiyo iko sawa kutolewa na mtu kama YEYE.
 
mimi si mmojawao wanaomuona Rais kama mfalme wao au baba yao!
Very good answer, kuna watu wanaona bila CCM hawawezi kuishi, hawawezi kupata kazi, watoto wao hawawezi kwenda shule hawana mawazo mbadala, hufikiri watu wote tuko hivyo wanatushangaa sana wanapotuona tuko tofauti kabisa na wao, wanajiuliza tunawezaje kuishi bila CCM? kwa hiyo hawawezi kuisema vibaya CCM au kusema mabaya ya rais hata kama wanaona wazi anakosea, watajikomba waonekane wema kwa heshima ya woga, mimi naona huo ni utumwa wa kifikra na utumwa wa kifikra ni mbaya zaidi kuliko ule wa wakoloni maana unashambulia nafsi, nashukuru Mungu kuniepusha kwa hilo, na sometimes usikute mimi ninayemkosoa rais nafaidika na CCM kuliko yeye anayejikomba, if you cannot express your own views you are as dead as a slave one.
 
Jana mwenyekiti wa CHADEMA bwana Freeman Mbowe alipokuwa akiwahutubia wananchi wa Wasso huko Ngorongoro alimtaka raisi Jakaya Mrisho Kikwete ajiuzulu na kuondoka Ikulu mara moja. Kisa kushindwa kuwalipa wafanyakazi kiwango cha chini cha sh.315,000!

Kila siku za uchaguzi zinavyokaribia yaonesha watanzania wanazidi kukosa heshima kwa raisi wao. Kumfukuza rais aliyechaguliwa namna hii pia ni kuwakosea heshima mamilioni ya watanzania waliomchagua.

Sababu za kushindwa kuwalipa kazieleza na nyinyi mwawajua wanaofilisi uchumi wa nchi, mbona makucha yenu hamjayakunjua kiasi hicho kwao.

Rais wetu akicheka mwanuna na akinuna kwenu ni nongwa. Nyinyii!

Kamwambie Kikwete heshima ni kitu cha bure. Na ukijiheshimu utaheshimiwa. Ukiwa tayari kusema kweli kwa waliokuchagua bila kujali maslahi yako basi nao watakuheshimu lakini ukiwa unawadanganya kila leo basi hustahili heshima hiyo. Katika ahadi zake za kampeni ya 2005 hadi hii leo katimiza ngapi?
 
Hayo mafuta mnayozidi kumpaka Kikwete yanazidi kumfanya azidi kunuka tu kwani anachotakiwa ni kuoga!....Keshajichafua yule kwa matusi yake kwa wananchi wake, kinachotakiwa aombe radhi la sivyo tutendelea kumwona takataka...
 
Mbowe kama mwenyekiti na kiongozi wa chama cha Upinzani (Chadema) ana kila haki ya kusema aliyosema ktk uringo wa kisiasa. Tujifunze zaidi nini maana ya demokrasia na uwezo wa chama pinzani kusema au kuomba rais aliyepo madakani kujiuzuru ama hata kuitisha Uchaguzi mpya. Malalamiko yako wewe mlalahoi yanaweza kupata nguvu tu yakipitia vyombo hivi vyenye nguvu kisheria ku raise issue kama hii. Ni nguvu hoyi hiyo ya kisheria inayompa Mabavu Mgaya kuzungumza kwa niaba ya wafanyakazi wote nchini na Kikwete asimfanye kitu.

Jambo moja tu ambalo naweza kusema ni kwamba yawezekana kuwa mimi nilimfahamu vizuri Kikwete kuliko watu wengi humu JF pamoja na kwamba sijawahi kulizungumzia hili. Upo uwezekano wa Mgaya kutumiwa na watu kisiasa pamoja na kwamba kuna ukweli mkubwa wa madai yake...Vyama vya Ushirika mara nyingi ndio waanzilishi wa Upinzani wa kweli ktk Utamaduni wa siasa na yawezekana kabisa kuwa Mgaya alitumiwa kuanzisha mjadala wa kima cha chini cha mishahara kwa wafanyakazi kama walivyofanya vyama vya wapinzani ktk nchi nyinginezo. Hoja kama hizi huingia moja kwamoja ktkakili za wananchi na kuleta upinzani mkubwa wa utawala uliopo. Ikumbukwe tu Morgan Tsvangirai wa Zimbabwe alikuwa katika nafasi kama hii na kuanzisha upinzani mpya wa kisiasa through mishahara na maisha duni ya Wazimbabwe kwa sababu shirikisho kama hizi zinawahusu Wafanyakazi moja kwa moja tofauti na vyama vya siasa ambavyo huzungumzia zaidi dira, sera na Ilani za chama kuliko hali halisi.
 
Back
Top Bottom