Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) kufanya uchunguzi wa kifo cha Mwanafunzi wa UDOM

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,308
5,462
Katika kipindi cha karibu wiki mbili, Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) imeona katika vyombo vya habari taarifa ya ajali ya gari iliyomhusu Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Afya), Mheshimiwa Dkt. Festo Dugange iliyotokea katika Jiji la Dodoma na kuthibitishwa na Jeshi la Polisi. Kwa niaba ya Tume, tunapenda kumpa pole Mheshimiwa Naibu Waziri kutokana na madhara aliyoyapata katika ajali hiyo. Mwenyezi Mungu aendelee kumponya na kumpa afya njema.

Tume pia imeona taarifa kupitia vyombo mbalimbali vya habari hususan mitandao ya kijamii kuhusu kifo cha mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma Bi Nusura Hassan Abdallah aliyekuwa mwananfunzi wa mwaka wa kwanza katika chuo hicho.

Kwa mujibu wa taarifa, imedaiwa kuwa Bi Nusura Hassan Abdallah alifariki katika hospitali ya Faraja, huko Himo mkoani Kilimanjaro. Kwa hali yoyote ile taarifa za kifo cha mwanafunzi huyo ni za kusikitisha kwa kuwa kifo hicho, iwe kwa sababu yoyote ile, kimekatisha ndoto ya maisha yake na haki yake ya kupata elimu ya juu. Tume inaungana na wazazi wa marehemu, uongozi na jumuiya ya Chuo Kikuu Dodoma, ndugu jamaa na marafiki katika kumwombea kwa Mwenyezi Mungu ampe pumziko la amani.

Wakati tukimwombea Nusura kwa Mwenyezi Mungu amrehemu na kumwombea Mheshimiwa Naibu Waziri apone haraka, kumekuwa na taarifa katika vyombo vya habari zikihusisha ajali ya Mhe Naibu waziri na kifo cha Bi Nusura Abdallah. Kumekuwepo na taarifa katika vyombo hivyo ambazo kwa tafsiri yake zinaonekana kukinzana. Taarifa hizo zimekaririwa kutoka katika Jeshi la Polisi, Chuo Kikuu cha Dodoma, Hospitali ya Faraja iliyopo Himo mkoani Kilimanjaro na taarifa za wananchi kupitia mitandao ya kijamii.

Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora inatambua kuhusu kuwepo kwa vyombo vinavyoshughulikia masuala ya haki jinai hususan Jeshi la Polisi na Ofisi ya Taifa ya Mashtaka ambapo katika mazingira ya kawaida vyombo hivyo vinahusika kulishughulikia suala hili.

Kwa kutambua hilo, Tume inavipa heshma kubwa sana vyombo hivyo katika utekelezaji wa majukumu yake na kazi kubwa ambayo vinafanya. Hata hivyo, kunapotokea mashaka kutoka kwa wananchi kuhusu jambo lolote linaloashiria uvunjwaji wa haki za binadamu au mashaka ya haki kutokutendeka, Tume inayo mamlaka ya kufanya uchunguzi juu ya jambo hilo kwa mujibu wa Katiba na Sheria ya Tume kwa kuwa inalo jukumu la kutetea na kulinda haki za binadamu nchini.

Kwa mujibu wa Kifungu cha 15(1) cha Sheria ya Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Sura ya 391 Tume inayo mamlaka ya kuanzisha uchunguzi wake yenyewe juu ya malalamiko yanayoashiria uvunjifu wa haki za binadamu na ukiukwaji wa misingi ya utawala bora pasipo kusubiri kuletewa malalamiko. Kwa muktadha huo Tume imeazimia kufanya uchunguzi wake huru kwa madhumuni ya kubaini ukweli kuhusu matukio hayo.
Imetolewa na:
Mathew P. M. Mwaimu (Jaji Mstaafu)
Mwenyekiti
TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA

Mei 10, 2023
Pia soma
 
Msikose kumhojo mke wa waziri. Anaweza kujua waziri alikua wapi siku hiyo in case waziri amesahau.
 
Waziri Dugange na poliCCM waliodanganya kuhusu kifo hiki sasa lazima waumbuke, hakuna namna.
 
Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Jaji Mwaimu amesema Tume yake itafanya Uchunguzi Huru wa Kifo cha Nusura Hassan Abdallah aliyekuwa mwanafunzi wa UDOM

Jaji Mwaimu amesema watafanya Uchunguzi Huru kwa mujibu wa Katiba ya JMT

Source: Mwananchi
 
Back
Top Bottom