Tume ya Haki za Binadamu (THBUB) kuchunguza tuhuma za Pauline Gekul

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,118
Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Tanzania (THBUB), inakusudia kufanya uchunguzi wa kina ili kupata ukweli wa tuhuma za ukatili na udhalilishaji unaodaiwa kufanywa na Mbunge wa Babati Mjini, Pauline Gekul dhidi ya Hashim Phillemon, mkazi wa Babati Mjini.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Novemba 28,2023 mjini Unguja, Makamu Mwenyekiti wa tume hiyo, Mohamed Khamis Hamad amesema taarifa za kitendo hicho zimekuwa zikitolewa na vyombo mbalimbali vya habari ikiwemo mitandao ya kijamii, hivyo tume imeamua kufuatilia kwa kina, kupata usahihi.

Amesema pamoja na hatua zilizochukuliwa na mamlaka mbalimbali wameona kuna haja ya kufanya uchunguzi huo kwa mujibu wa ibara ya 130 (1) (c) na (f) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwaka 1977 na kifuungu cha 6 (1) c, f, g pamoja na kifungu cha 15 (1) (a) vya Sheria ya THBUB sura ya 391 ili kubaini ukweli wa tuhuma hizo.
 
Asante tume Kwa ku respond haraka na kuchukua hatua kuchunguza
 
Uchunguzi kuusu nini hapo,,lakini pia hata vyombo vya habari kwasasa vinapaswa kupangiwa taarifa za kuwafikishia wananchi, taarifa Kama hivi zinazidi kutufanya huku kwenye jamii tunaongeza chuki zaidi lini tutaungana kwa taarifa Kama hizi,, huyo mbunge ilibidi wananchi wake wamuulize yupo wapi amabapo tayari akupaswa kua anahishi
 
Back
Top Bottom