usiue ALBINO
Member
- Aug 14, 2023
- 73
- 64
Kauli iliotolewa hivi karibuni na mwenyekiti wa CCM mkoa wa Arusha imenisikitisha sana. Kauli hiyo kwa upande wangu naiona kama ya ubaguzi kwa baadhi ya Wananchi ambao wanamtazamo totauti na fikira zake,jambo ambalo ni hatari kwa afya ya Taifa letu ambalo kwa muda fulani limepita kwenye kipindi ambacho baadhi ya Wananchi waliona kuwa walikuwa wameminywa katika utekelezaji wa baadhi ya majukumu yao, jambo ambalo waliona kuwa ni ukiukwaji wa katiba na sheria za Nchi.
Naiomba tume ya haki za binadamu kwa kushirikiana na taasisi na asasi mbali mbali,ikukemea kwa nguvu kauli kama hizo zilizotolewa na mwenyekiti wa ccm mkoa wa Arusha.kauli kama hizi zinaweza kupelekea Wananchi hasa wale wanaokosa huduma muhimu kama maji au huduma nyingine,kuichukia serikali iliyopo madarakani wakiamini kuwa ni maagizo ya Mwenyekiti wa ccm Taifa
Natoa wito wangu kwa viongozi waliopewa dhamana ya kuongoza Wananchi kuwa makini na tahadhari katika maagizo na matamshi yao.
Pia soma: Mwenyekiti CCM Arusha: Unachagua upinzani kisha unataka uletewe huduma ya maji?