Tanzania mwenyeji wa Kikao cha 77 cha Kawaida cha Tume ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu

bagamoyo

JF-Expert Member
Jan 14, 2010
21,305
24,200
Arusha, Tanzania

ITIFAKI YA UFUNGUZI YABADILISHWA DAKIKA ZA MWISHO

Tanzania mwenyeji wa mkutano wa 77 wa Tume ya Afrika ya Haki za Binadamu na watu, waziri Dr. Pindi Chana ametangaza mabadiliko baada ya mheshimiwa rais wa Jamhuri ya Muungano Dr. Samia Suluhu Hassan kutingwa na shughuli zingine za kitaifa hivyo kushindwa kuwepo kufungua mkutano huo wa kimataifa na atawakilishwa na Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Dr. Hussein Ali Mwinyi


View: https://m.youtube.com/watch?v=7fcJ96FBoZk

Miongoni mwa shughuli zitakazo kuwepo ktk mkutano huo ni uwasilishaji wa ripoti za nchi wanachama waliosaini mkataba wa kuwepo Tume hiyo muhimu Afrika

Ripoti ya nchi inayowasiliswa na nchi mwanachama lazima iangazie na ieleze yafuatayo:
• Hatua zilizochukuliwa katika kutekeleza masharti yaliyomo katika mkataba
• Maendeleo yaliyopatikana hadi wakati huo
• Changamoto zinazoathiri utekelezaji wa Mkataba na nyaraka nyingine za nyongeza zinazohusika

Nchi zinatakiwa kuwasilisha taarifa chini ya Mkataba wa Umoja wa Afrika kuhusu Ulinzi na Msaada wa Watu Waliolazimika Kuhama Makazi Ndani ya Nchi (ibara ya 14 (4) ya Mkataba wa Kampala).

Nchi ambazo zimeridhia Mkataba wa Afrika na Itifaki ya Maputo zinatakiwa kuwasilisha ripoti yenye sehemu tatu, kila sehemu moja ikihusika na mkataba mmoja.

Nchi inatakiwa kueleza utekelezaji wa masharti ya Itifaki ya Maputo kama imeridhia kulingana na Mwongozo wa Tume wa kwa ajili ya nchi kuwasilisha taarifa chini ya Itifaki ya Maputo.

Faida ya uwasilishaji wa ripoti ya nchi katika Itifaki ya Maputo
• Uwasilishaji ripoti huisaidia Tume kutimiza jukumu lake la uangalizi wa kusimamia utekelezaji wa Itifaki.
• Uwasilishaji wa Ripoti za nchi huipa nafasi nchi mwanachama
kuonesha hatua zilizochukuliwa kutekeleza itifaki, pamoja na sababu na changamoto zinazozuia utekelezaji wa Itifaki wenye ufanisi.
• Mchakato wa kuwasilisha unaiwezesha Tume kukusanya taarifa na uzoefu uliojitokeza katika nchi nyingi kutoka nchi kuhusu haki za wanawake katika Afrika.
• Baada ya kuzingatia ripoti hizi, Tume ya Afrika hutoa hitimisho na mapendekezo ambayo nchi wanachama wanatarajiwa kuyatekeleza ili kuboresha upatikanaji wa haki za wanawake.
• Uwasilishaji ripoti wa nchi hutoa namna ambayo Tume hupata taarifa za kuaminika na taswira ya kuaminika ya hali ya haki za binadamu katika nchi. ..... soma zaidi : source : Mwongozo wa Mfumo wa Haki za Binadamu Afrika - Maadhimisho ya Miaka 40 Tangu Kukubalika kwa Mkataba wa Afrika wa Haki za Binadamu na Watu 1981-2021 - Pretoria University Law Press (PULP)


ACHPR 77th Ordinary Session [Public]: 20 October – 9 November 2023​


View: https://m.youtube.com/watch?v=CYvY3VFdHgs

The African Commission on Human and Peoples’ Rights (the ACHPR) wishes to inform State Parties to the African Charter on Human and Peoples’ Rights, Organs of the African Union, National Human Rights Institutions, International Organizations, Non-Governmental Organizations and the general public that the 77th Ordinary Session of the ACHPR is scheduled to take place in Arusha Tanzania from Friday 20 October to Thursday 9 November, 2023.
 
Nchi zinatakiwa kuwasilisha taarifa chini ya Mkataba wa Umoja wa
Afrika kuhusu Ulinzi na Msaada wa Watu Waliolazimika Kuhama
Makazi Ndani ya Nchi (ibara ya 14 (4) ya Mkataba wa Kampala
).

Mambo magumu, ripoti ya nchi ya Tanzania kuhusu watu waliohamishwa kutoka makaazi yao n.k
 
Naona mama kaamua kula kona!

Kuna mambo mengi kuhusu Haki za Binadamu na Watu kwa upande wa nchi ya Tanzania bado hayajatekelezwa na yanatakiwa nchi husika kusema changamoto ni nini ?

Je Ni kukosekana utashi wa kisiasa kutokana na jeuri ya chama tawala dola kujichimbia hadi mihimili mingine ya dola kushindwa kuwa huru, Je ni rasilimali watu, au rasilimali fedha, kukosekana utawala bora hivyo serikali na wenye mamlaka kukakataa kuheshimu hukumu za maamuzi ya mahakama za ndani, EACJ mahakama ya Afrika Mashariki na ile hukumu ya Mahakama ya Afrika ....

Mtikila vs Tanzania (2013)​


View: https://m.youtube.com/watch?v=Cci-Qtd4BZk
 
Mambo mengi yanaendelea barani Afrika


View: https://m.youtube.com/watch?v=Mvcpk9z1380

The International Commission of Human Rights Experts on Ethiopia, impanelled by the Human Rights Council in 2021, delivered an update to the Council on 21 March 2023 during the Council's 52nd session. Chairperson Mohamed Othman said: "The Commission, pursuant to its mandate from this Council, continues to establish the facts and circumstances surrounding alleged violations and abuses – both in the past and ongoing – and to collect and preserve evidence accessible and usable in support of ongoing and future accountability efforts."
 

ACHRDA represented at the 77th Ordinary Session of the African Commission on Human and People’s Rights by Human Rights Officer.​

17 October 2023
African-Comission.jpg

16-18 October 2023​

The Forum on the Participation of NGOs at the 77th Ordinary Session of the African Commission on Human and Peoples’ Rights (African Commission), also known as the ‘NGO Forum’ is an advocacy platform coordinated by the African Centre for Democracy and Human Rights Studies (ACDHRS) to promote advocacy, lobbying and networking amongst and between human rights NGOs, for the promotion and protection of human rights in Africa.

The NGO Forum shares updates on the human rights situation in Africa with CSOs and the international NGO community with a view of identifying responses as well as adopting strategies towards the promotion and protection of human rights.

At the end of the forum, recommendations will be adopted and forwarded to the ACHPR for examination and adoption. This session is holding within the framework of the African Union theme of the year 2023 “The Year of AfCFTA: Acceleration of the African Continental Free Trade Area Implementation”.

More info :
Honourable Commissioner Prof. Rémy Ngoy Lumbu mwenyekiti wa ACHPR azungumzia vikao vya wiki tatu vya Tume Ya Haki za Binadamu na Watu Afrika mjini Arusha


View: https://m.youtube.com/watch?v=--RgvDRav8c Commissioner Remy Ngoy Lumbu from the Democratic Republic of the Congo, is a professor and respected expert on international justice.
 
Olusegun Obasanjo - Waafrika hasa viongozi ni wepesi wa kusahau maazimio wanayopitisha ktk mikutano


View: https://m.youtube.com/watch?v=FbT4LTgmgBE

Kiongozi huyo mstaafu anatoa mifano mingi ikiwemo azimio la Maputo - The Maputo Declaration, ukiwauliza viongozi waliokwisha hudhuria lina azimia nini asilimia 99 hawawezi kukuambia waliazimia nini ingawa walishiriki mkutano wa Maputo.
 
20 October 2023
Arusha, Tanzania

RAIS DR. HUSSEIN MWINYI KATIKA MKUTANO WA ACHPR

1697788803739.png
 
Back
Top Bottom