Beatrice Kamugisha
JF-Expert Member
- May 18, 2019
- 762
- 6,980
Kwenda kanisani kufanya Ibada Ni haki ya kikataba ndani ya Jamuhuri ya Muungano ya Tanzania. Wanaotaka katiba wamenyimwa kufanya makongamano, bila kuathiri Hali ya usalama wameamua siku ya ibada wavae t-shirt zao za kutaka katiba mpya. Naamu waumini wameamua kufanya t-shirt za katiba mpya kuwa nguo ya kuendea sokoni na kanisani.
Je, dola itazuia haki ya kuabudu? Itatunga sheria kwamba kuvaa tshirt ya katiba mpya ni dhambi? Sidhan Kama dola itqvunja katiba kwa kusukumwa na mavazi, tutaelewana tu kwamba tatizo siyo t-shirt, tatizo siyo mabango na Wala tatizo siyo Mbowe. Tatizo nikukosekana kwa haki.
Tunapoelekea tshirt nyekundu ya katiba mpya itakuwa Ni vazi la Taifa maana naona hata CCM wananunua nakwenda nalo kwenye TV.
Tukutane ibadani, Gwajima akipiga mwingi huko Ubungo sisi tupige mwingi kwenye nyumba zetu za ibada. Wachungaji na wasimamizi wa kanisa sidhani Kama watatii dola wakaacha kumtii Mungu aliesema njooni kwangu nyote msumbukao na kulemewa na dhambi maana ntawapumzisha.
Naamini kuwa na wataka katiba wanaokwenda kwenye nyumba za ibada ni Bora kuliko kuwa na wataka katiba wanaokwenda msituni. Kushuhudia waumini wakitaka mabadiliko ni Bora kuliko kushuhudia makundi ya uasi yakitaka mabadiliko. Tujivunie aina hii ya wanadamu kwenye ardhi yetu.