Tulipokuwa primary,unakumbuka?

Kuna wanaokumbuka 'Someni Kwa Furaha' kitabu cha kwanza mpaka cha nne. Wagagagigikoko, Lizabeta na Bulicheka? Vitabu vya Alfu Lela U Lela, Abdul etc etc??
 
Chang'ombe Primary School Dar 1971/72 - Viatu vilikuwa 'Maklipa','Tiger' na 'Bata', PE ndio kipindi kilichokuwa kikipendwa zaidi kwa vile ilikuwa ni dakika 45 za kucheza mpira!
Nje pale wakati wa mapumziko alikuwa anakuja mzee mmoja na tenga lake lenye mihogo ya kuchemsha tuliyoipa jina la 'Likembe'!
Kitabu cha kumsaidia mwanafunzi masomo ya Darasa la Saba kilikuwa ni 'Mwandani wa Wanafunzi'! kitabu cha kiswahili kilikuwa 'Tujifunze Lugha Yetu-kitabu cha 7' kwenye kiingereza kulikuwa na hadithi za 'Kalagesye' na kadhalika! Wanafunzi tulikuwa tunajisomea wenyewe vitabu vya hadithi kama 'Mashujaa', 'Roza Mistika', 'Visa vya Ajabu', 'Mashimo ya Mfalme Suleiman', 'Hadithi ya Allan Quaterman' na kadhalika na kadhalika...!
Those were really the beautful Days.....!!
 
Bulicheka na mkewe Lizabeta....(unaishaje huu wimbo wa Wagagagikoko?)

Na ule wa 'Makari hodari....yo yo yo '? unaishaje?


Bulicheka na mkewe Eliza, Eliza,
Walikwenda Mombasa kuiona nchi,
Katikati ya bahari chombo cha kikazama,
Wakaogelea wote wakaokokaa,
 
kweli enzi zinapita jameniiii, hayo mafuta ya Rays tena rangi zake zilikuwa zile kali sana kama njanoooooo na nyekundu. Ah tumetoka mbali sana. Na vikopo vile vilikuwa vikiisha mafuta basi vilitumika kama container za kuhifadhi mahindi yaliyokaangwa na kulowekwa na sukari. darasani huko ni kula kwa kwenda mbeleeeeeee.
 
Jamani wengine tunakumbuka enzi zile tunapo rudi shule pale karume tunarudi na kuuza dawa za mbu jioni na kibatari huku wagambo wakitusumbua aah kweli tumetoka mbali hizi dawa zilikuwa za aina mbili kijani na nyekundu lakini kijani ndio zilikuwa mali yaani zinawaka kuliko hizi nyekundu sijuwi zilikuwa zinatengenezwa wapi hizi
Halafu tuna sema tunenda shule kumbe tunaishia sokoni kariakoo au feri mhh makubwa yamepita.
 
Kuna wanaokumbuka 'Someni Kwa Furaha' kitabu cha kwanza mpaka cha nne. Wagagagigikoko, Lizabeta na Bulicheka? Vitabu vya Alfu Lela U Lela, Abdul etc etc??

Hapo umenipata natafuta hivyo vitabu nitapata wapi
 

Ngoja turekebishe kidogo haka kashairi ka kuukaribisha mwenge.



Twakukaribisha Mwenge
Mgeni wetu uringe
na wenyeji tukuchunge
Huku tukishangiria

Nuru yako yatangaza,
kuwa umetoa giza,
nuru umeieneza,
hapa kwetu Tanzania.

Kwetu ukitoka mwenge,
uelekee mahenge,
kila mwaka tuupange,
kuja kututembelea.


Nilidhani hii shairi litasahauliwa nilitoe. NAkumbuka Muhisika hapa alikuwa naitwa Dadi, mwenge ulikaribishwa kijijini Mahurunga! Yaani hadithi za vitabu vile niliamini ni kweli kabisa!
 
Duh, yaani sijui kwa nini nilkuwa sijaipitia hii thread wandugu.

Nakumbuka Simulizi za Allan Quaterman na Bwana Gudi, na Mashimo ya Mfalme Selemani yaani utafikiri ni kweli kabisa.

Vinara wa Allan Quatrman ni Msolopa Gasi na Shoka la Ajabu liitwalo Inskoskazi, Namkumbuka Faulata, na Bibi Gagula
 
Duh, yaani sijui kwa nini nilkuwa sijaipitia hii thread wandugu.

Nakumbuka Simulizi za Allan Quaterman na Bwana Gudi, na Mashimo ya Mfalme Selemani yaani utafikiri ni kweli kabisa.

Vinara wa Allan Quatrman ni Msolopa Gasi na Shoka la Ajabu liitwalo Inskoskazi, Namkumbuka Faulata, na Bibi Gagula

Nilikisoma kitabu hiki miaka mingi sana iliyopita, ila nilikuwa mdogo kuweza kukumbuka kila kitu. Nimesahau yaliyo mengi, ila nakumbuka sana "Mashimo ya Mfalme Suleiman na kadithi za "Twaingia katika nchi ya Wakukuana"
 
Ama kweli huko tulikotoka kulikuwa kutamu,

Nakumbuka shuleni kwetu tulikuwa na mwalimu mmoja mnoko sana, wiki ya zamu yake alikuwa anafika shuleni saa 11 Alfajiri ili agonge kengere ya kuhesabu namba saa 12 kamili. Basi mdogo wangu alikuwa mzembe sana wa kuamka mapema, siku moja akatoa mpya, aliamua kupiga mswaki usiku kabla ya kulala na akavaa uniform kabisa ili akikurupuka asubuhi ni mbio tu ili awahi namba. Kweli siku hiyo alifanikiwa kuwahi namba, lakini bado akapata adhabu maana uniform zake zilikuwa zimekunjamana sana kwa vile alilala amevaa. Mmeipata hiyo!!!!!!!!!!!!!!.

Vile vile nakumbuka enzi hizo tulikuwa hatuvai chupi wengi wetu wavulana kwa wasichana, sasa utamu ulikuwa pale ambapo kiranja unatoa adhabu ya wanafunzi kuruka kichura na wakati huo wewe (mimi) kiranja nimekaa mbele yaani wanaruka kuelekea kwangu nilipo. Yaani tilikuwa tunaona picha za bure kabisa.......

Nakumbuka baada ya muda wa shule au siku za jumamosi tunaenda kuchanja/kutafuta kuni, kama wewe ni kijana mkubwa una ka-demu kako, basi mtawafukuza watoto wadogo ili mcheze mchezo wa baba na mama kwenye kichaka. Basi wakuu, ni enzi hizo wengine tulianza kupata uzoefu.
 
Nakumbuka shuleni kwetu tulikuwa kila siku ya jumatatu kwenye gwaride la usafi tulikuwa tunaimba wimbo huu kabla ya ukaguzi wa Mkuu wa shule.

(1) Sisi ndio vijana wako Mwalimu Nyerere,
Tutakao kilinda chama cha mapinduzi

Kiitikio: Hongera Mwenyekiti wa CCM,
Hongera na makamu wa Mwenyekiti.

(2) Chama kilizaliwa visiwani Unguja,
Na sherehe za mwanzo mkoani Dodoma


Kiitikio: Hongera Mwenyekiti wa CCM,
Hongera na makamu wa Mwenyekiti.
 
Mkuu anayekumbuka huu wimbo auweke sawa basi:

(1) Chama chetu kimetuongoza, hadi uhuru tulioupata,
Kinaendelea kuongoza kufikia lengo ujamaa.
Mwenyekiti Mwalimu Nyerere mwenye hekima na wingi wa sifa, Tanzania

Kiitikio
Ewe chama chombo chetu mathubuti kwa hakika, ndio wewe nguzo yetu muongozi wa Taifa, Mwenyekiti Mwalimu Nyerere mwenye hakima na wingi wasifa, Tanzania.

(2) Ilifika wakati mgumu wananchi walifadhaika, utumwa ukoloni ni sumu sisi sote tuna ............


(?) Na mtu asiyejua kufa mwambieni aone kaburi.........

Mie siukumbuki vizuri
 
Jamani wengine tunakumbuka enzi zile tunapo rudi shule pale karume tunarudi na kuuza dawa za mbu jioni na kibatari huku wagambo wakitusumbua aah kweli tumetoka mbali hizi dawa zilikuwa za aina mbili kijani na nyekundu lakini kijani ndio zilikuwa mali yaani zinawaka kuliko hizi nyekundu sijuwi zilikuwa zinatengenezwa wapi hizi
Halafu tuna sema tunenda shule kumbe tunaishia sokoni kariakoo au feri mhh makubwa yamepita.

Ebwana we wewe utakuwa Alumni wangu unamkumbuka Marehemu Mwalimu motomoto? Sabuni ( soap ) Mwalimu Muhsin?

U made my day mate na story ya kuuza dawa za Mbu na kulangua sigara..
 
Ninakumbuka pia wimbo huu wa kuusifu Ujamaa
na kuupinga ubepari (ukoloni)


Wito umekwisha tolewa,
Njoni tuishi kijamaa,
Sasa twamkomiesha mchawi,
Naye ndiye ubinafsi;
Tulitawaliwa,
na hayo mawazo,
ya ubinasi kama;
Liwe jembe, eti langu,
liwe duka eti langu,
kiwe kiwanda eti changu,
chochote kile eti changu;
Lo! lo! loooooooo!

Hiyo hiyo ni kasumba,
ni makovu ya mkoloni,
ubinafsi,
ni kichochoro cha maendeleo,
chapindapinda,
nao ujamaa,
barabara ya lami,
ukipita hapo,
kichwa mbele haraka.
 
Duh! Mnakumbuka enzi hizo 2kienda shule 2napaka mafuta ya kupikia KORIE? Yaani mguu ulikua unameremeta na uso unawaka mpaka basi. Unajibandika layer ya mafuta.

Ukikosa mafuta hayo unapata
Rays. Yalikua yakiuzwa sh 100 tu.
 
Stori za Juma Rose and Baraka?
Hizi stori zilikuwa zinanikosha ile mbaya, mwanzoni ngeli ilikuwa haipandi kabisaa, ila nilikuwa nikiona picha za Juma,Rose na baraka stori ilikuwa inapanda kwelikweli.ila stori ya mwisho ktk series za stori Za juma and baraka ilikuwa chapter ya mwisho wakati huo tuko darasa la saba, Juma anaaga anasema byebye, it was too emotional, from that moment i was not a kid again!

Halafu kwa Upande wa vitabu vya Kiswahili, nako ilikuwa burudani tupu.
stori kama KIBANGA AMPIGA MKOLONI, SIZITAKI MBICHI HIZI,SIKU YA GURIO KATERERO,BENDERA YA TANZANIA,ANDUNJE(mtoto mdadisi), NGANENEPA ANG'ATWA NA NYOKA,AHADI KUMI ZA MWANA TANU na nyingine nyingi zote ilikuwa burudani tupu.

Kweli wakati ule mtaala ulikuwa umetulia, kwa sasa hivi sifahamu mitaala ikoje lakini nakiri mtaala katika somo la kiswahili, ulikuwa umetulia.

Nimalizie kwa beti ninazozikumbuka(japo sizikumbuki vizuri sana) kutoka katika shairi la sizitaki mbichi hizi

Hadithi inayokuja, ni ya sungura sikia
hadithi uliyongoja leo ninakuletea
Alitoka siku moja njaa aliposikia
njaa aliposikia sungura nakuambia

Siku hiyo akaenda porini kutembelea
akayaona matunda mtini yameenea
sungura akayapenda mtini akasogea
Mtini akasogea sungura nakuambia

SIZITAKI MBICHI HIZI, sungura akagumia
naona nafanya kazi bila faida kujua
yakamtoka machozi matunda akalilia
Matunda akalilia Sungura nakuambia

Usifanye utani mkuu, kile Kiswahili tulichosoma sie enzi hizo kilikuwa kimetulia sana! Siyo sasa, wanetu hawajui tofauti ya "ndiyo" na "ndio" au "Hapa" na "apa" ama "Hicho" na "hiko". Yaani hapa umenikuna kinoma. Kwanza madarasa yale ya mwanzo kulikuwa na vitabu murua sana, kama kile cha Paulo na Selina (darsa la pili), Kuna hadithi za Kinango na Nzige, Heri Mimi sijasema na kadhalika. Ukija darasa la tatu ndio unakutana na akina Andunje, Nondo Mla watu, Twende Tukawinde, Jogoo Aliyesema (hadithi ya Pazi) na Sadiki na Sikiri.

SHAIRI LA SADIKI NA SIKIRI
Sikiri mimi masikini
Uvivu wangu nyumbani
Ukiwa huu wa njiani
Nakufa hapa kwa nini?
.....................>
Pia kitabu hiki kilikuwa na shairi la kuukaribisha mwenge, kama kuna mtu analikumbuka basi si vibaya akatukumbusha

Ukija Darasa la Nne ndio unakutana na Kibanga Ampiga Mkoloni, Ndoto ya Kimweri (chifu wa Wasambaa), Mkwawa Shujaa, Barua Kwa Mjomba Mndolwa na Siku ya Gulio Katerero (hadithi ya Kiiza).
Shairi la kitabu hiki linaanza hivi:

KAMA MNATAKA MALI
Karudi baba mmoja, toka safari ya mbali
Kavimba yote mapaja, na kutetemeka mwili
Watoto wake wakaja, ili kumtaka hali
Wakataka na kauli iwafae maishani

Akatamka mgonjwa, ninaumwa kweli kweli
Hata kama nikichanjwa, haitoki homa kali
Roho naona yachinjwa, Kifo kimenikabili
Kama mnataka mali, mtayapata shambani
........................................>
Darasa la tano napo kulikuwa na mahanjamu yake. Nakumbuka hadithi kama ile ya 'Safari Yenye Mkosi', Vijana Wapiga Kambi Ngulwi, Ukakamavu, Kapulya Mdadisi, na kadhalika.

SHAIRI LA KITABI HIKI LINAANZA HIVI
Tumeizika elimu, elimu ya kizamani
Elimu ile haramu, maana ya kikoloni
Imetuishia hamu, kuiga ya ugenini
Elimu yetu ya sasa yawafaa wananchi
...................................>

Kitabu cha Kiswahili cha darasa la sita sikikumbuki vizuri, tulikuwa na mwalimu bomu sana ila nitajitahidi kukumbuka, nadhani kulkuwa na mada moja inahusu 'walowezi'.

Kwa upande wa darasa la saba mambo yalikuwa poa sana.
Kulikuwa na mada kama, Chuo Kikuu, Brown Ashika Tama, Jiji la Dar Es Salaam nk.
Kulikuwa na mashairi mawili katika kitabu hiki, moja linaanza hivi:

Ninaye ndege mzuri, mrembo wa Kupendeza
Rangi zake mashuhuri, ni nne nawaeleza
Ndizo rangi za fahari, urembo kuutimiza
Ndege huyu ndege gani, hapa Kwetu Tanzania?
..........................................>
NB:
Mkuu Gamba la Nyoka, enzi za mawaziri Mungai na Kapuya, walivuruga sana wizara hii ya elimu, yaani vila vitabu vimevurugwa sana baada ya kuunganisha baadhi ya masomo, yaani vitabu havina mshawasha kama vile vya mwanzo. nilivipitia kidogo mwaka 2001 kuangali yaliyomo, nilisikitika sana. Wanetu wanakosa mambo mengi sana kutoka katika vitabu vile. Sikatai kuwa walifanya vile ili kwenda na wakati, binafsi sikuona ubaya wa vile vitabu vya mwanzo.
Tuendelee na kumbukumbu hizi!

Mkuu IDIMI nashukuru sana mzee kwa information hizi, kwa kweli nimekumbuka mbali sana na najihisi hata machozi kunidondoka mtu wangu.

Nilikuwa dogo enzi hizo napiga soka balaa, begi kubwa mgongoni ndani madaftari kibao,Kuhusu ile Stori ya Twende Tukawinde ,nimeikumbuka majamaa wameenda kuwinda ngedere ,dingi kabeba gobore, dada yao kawaandalia Mabumunda. katika hiyo stori nakumbuka jamaa alivyokuwa akilalamika kwa machungu jinsi ngedere wanavyomaliza mazao shambani, nanukuu "Ni nani aliyekula Matango yetu?, huyu atakuwa ni Mnyonyaji".

Umenikumbusha tena kuhusu sikiri na Sadiki

Sadiki sasa ashiba
Chakula kingi kwa baba
Nirudi tena kwa baba
Nakufa hapa kwa nini?

Halafu kuhusiana Na Bendera ya Tanzania
kulikuwa na shairi pia, nakumbuka ubeti mmoja

wakoloni walifika,huku na dharau zao
Kudharau Afrika,kutukuza nchi zao
Sasa wanaaibika, hawana tena kikao
..........................,,,,>



Nakumbuka kidoogo kuhusiana na shairi hili

Twakukaribisha Mwenge
Mgeni wetu uringe
na wenyeji tukupambe
Huku tukishangiria!

Idimi unaikumbuka ngonjera ya(mimi nimeikumbuka kwa mbaali,nadhani nitakuwa nimekosea ila najaribu kuvuta feeling)

Dada Asha sikilza
Maneno ya kupendeza
Azimio la Arusha
Lilizaliwa Arusha

Arusha unaitaja
sijui inavyokuja
Azimio la arusha
Azimio kitu gani?


Think Pad,

Ulicopy hapa zile posts zako kuleeeeee kwa Kabanga ampiga mkoloni....sawa?
 
I remember kila siku jioni kabla ya kuondoka tunaenda parade then tunaimba wimbo ufuatao:

Bendera ya Tanzania,
ndiyo ya kujivunia
Ilianza kupepea,
mwaka sitini na moja,

Hapo tunashuhudia
Tunavyojitegemea
Hapa kwetu Tanzania,
Uhuru umechanua,
Muumba wetu rabuka,
Zijaze zako fanaka......!

....nimesahau sahau vimaneno vingine.....but was very very emotional aiseee.......!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom