Tulipokuwa primary,unakumbuka?

Gamba la Nyoka

JF-Expert Member
May 1, 2007
7,022
9,286
Stori za Juma Rose and Baraka?
Hizi stori zilikuwa zinanikosha ile mbaya, mwanzoni ngeli ilikuwa haipandi kabisaa, ila nilikuwa nikiona picha za Juma,Rose na baraka stori ilikuwa inapanda kwelikweli.ila stori ya mwisho ktk series za stori Za juma and baraka ilikuwa chapter ya mwisho wakati huo tuko darasa la saba, Juma anaaga anasema byebye, it was too emotional, from that moment i was not a kid again!

Halafu kwa Upande wa vitabu vya Kiswahili, nako ilikuwa burudani tupu.
stori kama KIBANGA AMPIGA MKOLONI, SIZITAKI MBICHI HIZI,SIKU YA GURIO KATERERO,BENDERA YA TANZANIA,ANDUNJE(mtoto mdadisi), NGANENEPA ANG'ATWA NA NYOKA,AHADI KUMI ZA MWANA TANU na nyingine nyingi zote ilikuwa burudani tupu.

Kweli wakati ule mtaala ulikuwa umetulia, kwa sasa hivi sifahamu mitaala ikoje lakini nakiri mtaala katika somo la kiswahili, ulikuwa umetulia.

Nimalizie kwa beti ninazozikumbuka(japo sizikumbuki vizuri sana) kutoka katika shairi la sizitaki mbichi hizi

Hadithi inayokuja, ni ya sungura sikia
hadithi uliyongoja leo ninakuletea
Alitoka siku moja njaa aliposikia
njaa aliposikia sungura nakuambia

Siku hiyo akaenda porini kutembelea
akayaona matunda mtini yameenea
sungura akayapenda mtini akasogea
Mtini akasogea sungura nakuambia

SIZITAKI MBICHI HIZI, sungura akagumia
naona nafanya kazi bila faida kujua
yakamtoka machozi matunda akalilia
Matunda akalilia Sungura nakuambia
 
Usifanye utani mkuu, kile Kiswahili tulichosoma sie enzi hizo kilikuwa kimetulia sana! Siyo sasa, wanetu hawajui tofauti ya "ndiyo" na "ndio" au "Hapa" na "apa" ama "Hicho" na "hiko". Yaani hapa umenikuna kinoma. Kwanza madarasa yale ya mwanzo kulikuwa na vitabu murua sana, kama kile cha Paulo na Selina (darsa la pili), Kuna hadithi za Kinango na Nzige, Heri Mimi sijasema na kadhalika. Ukija darasa la tatu ndio unakutana na akina Andunje, Nondo Mla watu, Twende Tukawinde, Jogoo Aliyesema (hadithi ya Pazi) na Sadiki na Sikiri.

SHAIRI LA SADIKI NA SIKIRI
Sikiri mimi masikini
Uvivu wangu nyumbani
Ukiwa huu wa njiani
Nakufa hapa kwa nini?
.....................>

Pia kitabu hiki kilikuwa na shairi la kuukaribisha mwenge, kama kuna mtu analikumbuka basi si vibaya akatukumbusha

Ukija Darasa la Nne ndio unakutana na Kibanga Ampiga Mkoloni, Ndoto ya Kimweri (chifu wa Wasambaa), Mkwawa Shujaa, Barua Kwa Mjomba Mndolwa na Siku ya Gulio Katerero (hadithi ya Kiiza).
Shairi la kitabu hiki linaanza hivi:

KAMA MNATAKA MALI
Karudi baba mmoja, toka safari ya mbali
Kavimba yote mapaja, na kutetemeka mwili
Watoto wake wakaja, ili kumtaka hali
Wakataka na kauli iwafae maishani

Akatamka mgonjwa, ninaumwa kweli kweli
Hata kama nikichanjwa, haitoki homa kali
Roho naona yachinjwa, Kifo kimenikabili
Kama mnataka mali, mtayapata shambani
........................................>

Darasa la tano napo kulikuwa na mahanjamu yake. Nakumbuka hadithi kama ile ya 'Safari Yenye Mkosi', Vijana Wapiga Kambi Ngulwi, Ukakamavu, Kapulya Mdadisi, na kadhalika.

SHAIRI LA KITABI HIKI LINAANZA HIVI
Tumeizika elimu, elimu ya kizamani
Elimu ile haramu, maana ya kikoloni
Imetuishia hamu, kuiga ya ugenini
Elimu yetu ya sasa yawafaa wananchi
...................................>


Kitabu cha Kiswahili cha darasa la sita sikikumbuki vizuri, tulikuwa na mwalimu bomu sana ila nitajitahidi kukumbuka, nadhani kulkuwa na mada moja inahusu 'walowezi'.

Kwa upande wa darasa la saba mambo yalikuwa poa sana.
Kulikuwa na mada kama, Chuo Kikuu, Brown Ashika Tama, Jiji la Dar Es Salaam nk.
Kulikuwa na mashairi mawili katika kitabu hiki, moja linaanza hivi:

Ninaye ndege mzuri, mrembo wa Kupendeza
Rangi zake mashuhuri, ni nne nawaeleza
Ndizo rangi za fahari, urembo kuutimiza
Ndege huyu ndege gani, hapa Kwetu Tanzania?
..........................................>

NB:
Mkuu Gamba la Nyoka, enzi za mawaziri Mungai na Kapuya, walivuruga sana wizara hii ya elimu, yaani vila vitabu vimevurugwa sana baada ya kuunganisha baadhi ya masomo, yaani vitabu havina mshawasha kama vile vya mwanzo. nilivipitia kidogo mwaka 2001 kuangali yaliyomo, nilisikitika sana. Wanetu wanakosa mambo mengi sana kutoka katika vitabu vile. Sikatai kuwa walifanya vile ili kwenda na wakati, binafsi sikuona ubaya wa vile vitabu vya mwanzo.
Tuendelee na kumbukumbu hizi!
 
Mkuu IDIMI nashukuru sana mzee kwa information hizi, kwa kweli nimekumbuka mbali sana na najihisi hata machozi kunidondoka mtu wangu.

Nilikuwa dogo enzi hizo napiga soka balaa, begi kubwa mgongoni ndani madaftari kibao,Kuhusu ile Stori ya Twende Tukawinde ,nimeikumbuka majamaa wameenda kuwinda ngedere ,dingi kabeba gobore, dada yao kawaandalia Mabumunda. katika hiyo stori nakumbuka jamaa alivyokuwa akilalamika kwa machungu jinsi ngedere wanavyomaliza mazao shambani, nanukuu "Ni nani aliyekula Matango yetu?, huyu atakuwa ni Mnyonyaji".

Umenikumbusha tena kuhusu sikiri na Sadiki

Sadiki sasa ashiba
Chakula kingi kwa baba
Nirudi tena kwa baba
Nakufa hapa kwa nini?

Halafu kuhusiana Na Bendera ya Tanzania
kulikuwa na shairi pia, nakumbuka ubeti mmoja

wakoloni walifika,huku na dharau zao
Kudharau Afrika,kutukuza nchi zao
Sasa wanaaibika, hawana tena kikao
..........................,,,,>

Pia kitabu hiki kilikuwa na shairi la kuukaribisha mwenge, kama kuna mtu analikumbuka basi si vibaya akatukumbusha

Nakumbuka kidoogo kuhusiana na shairi hili

Twakukaribisha Mwenge
Mgeni wetu uringe
na wenyeji tukupambe
Huku tukishangiria!

Idimi unaikumbuka ngonjera ya(mimi nimeikumbuka kwa mbaali,nadhani nitakuwa nimekosea ila najaribu kuvuta feeling)

Dada Asha sikilza
Maneno ya kupendeza
Azimio la Arusha
Lilizaliwa Arusha

Arusha unaitaja
sijui inavyokuja
Azimio la arusha
Azimio kitu gani?
 
Du, wakuu mmenifurahisha sana.

Juzi nememuuliza mwanangu darasa la tano kama anajua jiografia, ananiambia hiyo ndiyo nini. ni kweli kina Mungai wametuvurugia sana elimu yetu. kulikuwa pia na hadithi ya Kana ka nsungu mwelu nadhani hii ilikuwa darasa la nne. halafu kuna mzee mtu mzima hivi alichorwa amekaa chini ya mwembe anamwaga busara zake ingawa sikumbuki title yake. Na vipi ile safari yenye mikosi
 
Mnanikumbusha mbali! Nakumbuka manenge na mandawa primary... hizi hadithi zilinyanua sana fikra zetu.Halafu kulikuwa na vitabu kama 'usiku wa Kiza'.

Tumetoka mbali.
 
Mh imenikumbusha mbali, nakumbuka hadithi ya kwanza ya kitabu cha darasa la kwanza, JUMA NA ROZA

Huyu ni Juma,
Juma ana dada,
Dada yake ni Roza,
Juma anasema,
Tia sukari Roza,
Tia maziwa,
Roza una kiu?
Kunya chai Roza.


Na pia kama sikosei kitabu cha darasa la tatu kilikuwa na hadithi ya Selina na Mariamu walienda msituni, na kuna picha wanaruka kamba, na mwisho kilikuwa kina hitimisha na hadithi ya watu walikuwa wanataka kuchagua kiongozi wao, na kulikuwa kuna picha ya wananchi na mtu mrefu kuliko wote.
 
Du, wakuu mmenifurahisha sana.

Juzi nememuuliza mwanangu darasa la tano kama anajua jiografia, ananiambia hiyo ndiyo nini. ni kweli kina Mungai wametuvurugia sana elimu yetu. kulikuwa pia na hadithi ya Kana ka nsungu mwelu nadhani hii ilikuwa darasa la nne. halafu kuna mzee mtu mzima hivi alichorwa amekaa chini ya mwembe anamwaga busara zake ingawa sikumbuki title yake. Na vipi ile safari yenye mikosi

Huyo Mzee aliyekuwa amekaa kwenye Mwembe anamwaga busara nadhani alikuwa ni Mzee Kaswiga wa Mbalizi Mbeya (hadi mwaka 1994 ule mti ulikuwa bado upo, sijui kwa sasa, na ukoo wa Kaswiga bado wapo)akiongea na Mr Brown wa Uingereza, baada ya Brown kutembelea Tanzania baada ya uhuru. Hadithi ndio ile niliyodokeza inayosema "Brown ashika Tama". Alishika tama kushangaa 'maendeleo' ya Tanzania baada ya uhuru.

Kuhusu safari yenye mkosi ni kwamba gari lile (isuzu) lilipata pancha mara kadhaa njiani kiasi kwamba wale wanafunzi wliokuwa wanaabiri katika basi lile walifika wakiwa wamechoka sana.

Gamba, umenikumbusha "Mabumunda", nimecheka mpaka machozi kunitoka. Sikutarajia kukumbuka kitu cha namna hii, kweli tunatoka mbali
 
Mnanikumbusha mbali! Nakumbuka manenge na mandawa primary... hizi hadithi zilinyanua sana fikra zetu.Halafu kulikuwa na vitabu kama 'usiku wa Kiza'.

Tumetoka mbali.

Rubabi, kwenye hiki kitabu cha Manenge na Mandawa ndio una ile hadithi ya "Heri Mimi Sijasema", "Safari ya Unguja", "Kinango na Nzige" na "Mwizi wa Viazi".

Nikukumbushe usemi wa Manenge na Mandawa--
Tumbo niache....Nimuachie Manenge
Tumbo niache....Nimuachie Mandawa


Wanetu wanamisi sana mambo haya.
 
Du, wakuu mmenifurahisha sana.

Juzi nememuuliza mwanangu darasa la tano kama anajua jiografia, ananiambia hiyo ndiyo nini. ni kweli kina Mungai wametuvurugia sana elimu yetu. kulikuwa pia na hadithi ya Kana ka nsungu mwelu nadhani hii ilikuwa darasa la nne. halafu kuna mzee mtu mzima hivi alichorwa amekaa chini ya mwembe anamwaga busara zake ingawa sikumbuki title yake. Na vipi ile safari yenye mikosi

Sahara,
Ile hadithi ya "Kana ka Nsungu Mwelu" naikumbuka, kwenye kile kitabu kuna hadithi ya "Sizimwa" yule jamaa aliyekuwa anatisha watu, kiasi kwamba kijiji kikalazimika kumdhibiti kwa kumchimbia shimo refu ambamo alitumbukia, kisha wanakijiji wakammaliza kwa mikuki na mishare.
Pia kwenye kitabu hiki hiki kuna hadithi ya yule Jamaa Mkenya aliyefuga simba (inasemekana ni hadithi ya kweli).

Tuendelee kukumbushana.
 
Mh imenikumbusha mbali, nakumbuka hadithi ya kwanza ya kitabu cha darasa la kwanza, JUMA NA ROZA

Huyu ni Juma,
Juma ana dada,
Dada yake ni Roza,
Juma anasema,
Tia sukari Roza,
Tia maziwa,
Roza una kiu?
Kunya chai Roza.


Na pia kama sikosei kitabu cha darasa la tatu kilikuwa na hadithi ya Selina na Mariamu walienda msituni, na kuna picha wanaruka kamba, na mwisho kilikuwa kina hitimisha na hadithi ya watu walikuwa wanataka kuchagua kiongozi wao, na kulikuwa kuna picha ya wananchi na mtu mrefu kuliko wote.

Kweli kabisa. Iliwachukua muda mrefu sana kupata kiongozi watu wale, maana walitaka awe mnene kuliko wote, awe mrefu kuliko wote, awe na kila sifa inayohitajika (kuliko wote), kiasi kwamba hadi mwisho walishindwa kumpata kiongozi sahihi.
Nakumbuka mbali sana, nawashukuru sana wana JF kwa kumbukumbu hii.
Hadithi ya Juma na Roza/Selina na Mariamu imenimaliza sana!
 
Kweli kabisa. Iliwachukua muda mrefu sana kupata kiongozi watu wale, maana walitaka awe mnene kuliko wote, awe mrefu kuliko wote, awe na kila sifa inayohitajika (kuliko wote), kiasi kwamba hadi mwisho walishindwa kumpata kiongozi sahihi.
Nakumbuka mbali sana, nawashukuru sana wana JF kwa kumbukumbu hii.
Hadithi ya Juma na Roza/Selina na Mariamu imenimaliza sana!

IDIMI yote tisa, kumi ni ile Stori ya mzee Tola
Mzee mchoyo anapenda kula gizani, siku ya siku kala konokono!, mwe alikoma ubishi.

Unajua zile stori zilikuwa na falsafa sana, mfano ukiangalia ile stori ya nondo mla watu, inasisitiza umuhimu wa ushujaa na kujitolea, au hii stori ya mzee Tola, inasisitiza kutokuwa mchoyo.

Tuje katika Upande wa namba.
Zile hesabu za pai mara kipenyo, zilikuwa si mchezo zile, watu walikuwa na vidaftari vyao vimejaa kanuni Tupu. ila zile hesabu za umri na Uwiano zilikuwa si mchezo mtu wangu.

unakuta swali limetegwa kwelikweli, mfano unaambiwa umri wa Asha ni mara mbili ya umri wa juma wa sasa, miaka mitano iliyopita umri wa asha ulikuwa Theluthi ya umri wa Juma, je umri wa Asha wa sasa ni miaka mingapi?

Basi hapo mtu wangu watu tulikuwa tunakodoa macho vibaya mno.
 
Si utani Mkuu Gamba, nakumbuka nilikuwa na daftari la kanuni nyingi sana za hisabati. Ilikuwa kabla hatujaanza rasmi mada ya siku hiyo basi lazima mwalimu aanze na chemsha bongo, ilikuwa noma! Pai mara kipenyo nazikumbuka sana, labda tuendelee kukumbushana kanuni hizi kwa maslahi ya vizazi vyetu vijavyo, maana wanetu wanaogopa sana namba miaka hii, kiasi kwamba zinaitwa "UGONJWA WA TAIFA"
Nakumbuka kanuni kadhaa.
Kutafuta nyuzi (degrees)za maumbo mbali mbali tulitumia kanuni hii:
P= (n-2)90, lakini kuna 'wahuni' wakaja na na hii:
P= (2n-4)180
Kimsingi ukitumia kanuni zote mbili unapata jibu moja, sasa hao waliotumia hiyo njia ya pili ambao nawaita 'wahuni' kulikuwa na haja gani kuweka hiyo namba 2 katika kanuni?

Sijamsahau Mzee Tola na uchoyo wake.

Je unakumbuka "Chilunda Apambana na Chui"?
 
Hahahaha mzee umenikumbusha hesabu za nyuzi, mimi nilikuwa nikiona mahesabu ya maumbo ya nyuzi naangalia kwanza kama ndani kuna Umbo Z, nikiliona tu baasi ,swali limekwisha.

halafu nilikuwa na kitabu fulani kinaitwa "HESABU ZA KIKWETU", aisee yule jamaa aliyekiandika kile kitabu nampigia saluti.

Je unaikumbuka kanuni ya kutafuta Eneo la mche duara uliofungwa pande zote?
 
Sikumbuki ni kitabu cha darasa la ngapi, ila Babu janja likataka linywe chai kiujanja ujanja, huku mjukuu wake akiishia kumezea mate tu mezani.

Babu janja: Unaweza kunywa chai ya moto iliyotoka kwenye bilauri bila kupulizia?

Mjuukuu: Siwezi

Babu janja: Ukiweza kuinywa chai hii bila kupuliza na bila kutumia kisosa, nitakununulia peremende sokoni.

Mjukuu: siwezi, na wewe ukiweza kuinywa ya moto nitakununulia ugoro/tumbaku sokoni.

Babu akatia chai kwenye kikombe na akaanza kama ifuatavyo huku akikaribisha mdomo wake milimita chache kutoka kwenye ncha za kikombe:

Mtoto wewe mtifuuuuuuuuuuuuuuuuuuu
Una moyo mkunjufuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuu
Mwalimu anakusifuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuu
Hata mie ninasifuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuu
Chai hii takatifuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuu


Babu janja kwa kuivuta fuuuuuuuuuuuuuuuu kwa kila sentensi aliyosema akawa amefanikiwa kuipooza chai mithiri ya togwa. Matokeo yake mjukuu chai hakunywa na deni la tumbaku akawa nalo.
 
Enzi hizo mtu akifaulu (kuchaguliwa) darasa la saba kwenda form one nyumbani inakuwa bonge la shangwe lakini si siku hizi hamna tena hiyo sherehe maana ni muda wa mzazi kujikuna kumpelekea mamilioni mama Lwakatare (St. Marys) tehe tehe !
 
Enzi za

mabata madogodogo yanaogelea,yanaogelea
katika shamba zuri la bustani
Yanapenda kutembea bila viatuu,bila vaituu
katika shamba zuri la bustani

yanapenda kulia kwakwa kwakwa kwaakwa,kwakwa kwakwa kwaakwa
katika shamba zuri la bustani.

Ebwanae wachawe si mchezo
Kabla sijahamia Town, nilipata kusoma kijijini, darasa la kwanza na la pili, huko ilikuwa tabu tupu, asubuhi mchakamchaka, wakati mwingine hamuingii darasani siku nzima nyinyi ni kulima tu.kama mmelima mahindi, basi siku ya siku mkishavuna mnapikiwa uji kila mtu anaambiwa aje na kikombe,mnakunywa siku hiyo ,halafu ndo imetoka hiyo.hivi siku hizi mambo ya mchakamchaka vijijini bado yapo?
 
Wakuu mmenikumbusha mbali sana, yaani mmeifanya siku yangu iwe nzuri kwa sababu nimekumbuka mbali sana, siyo siri hadi machozi yamenitoka.

Mnaikumbuka Jiografia darasa la nne? Kamwe siwezi kusahau I wish kama nianze kufundisha kama yule mwalimu, alikuwa bado binti enzi hizo, walimu walikuwa wanafundisha bwana enzi hizo. MNAKUMBUKA KILIMO CHA MIHOGO MTWARA, KILIMO CHA KARANGA DODOMA, UVUNAJI WA ASALI TABORA,KILIMO CHA MKONGE TANGA. Hiyo ilikuwa ni jiografia maalumu ya kuijua nchi yetu na mali asili zake.

Mnakumbuka zile hesabu za darasa la Tano VIPEO NA VIPEUO?

Kiswahili darasa la saba sura ya kwanza kabisa ilikuwa ni shairi ambalo ni fumbo "NDEGE HUYU NDEGE GANI" jibulake ni Tanzania, naomba kama kuna mtu anakumbuka anikumbushe.

Jamani enzi hizo ukifaulu kwanza pale kijijini au mtaani unaheshimika, matokeo yalikuwa yanatoka siku moja kabla ya Christimas,yaani ile sherehe ya Christimas inakuwa yako.

Jamani kweli nimekumbuka mbali saaaana.
 
Kwa Ram,
Shairi lile la ndege kwenye kitabu cha darasa la saba lipo hapo juu, mimi nimeanza na ubeti mmoja wa kwanza, kama kuna mwingine anakumbuka nadhani anaweza kuliendeleza.
Ram, umeniacha hoi na yule babu na mjukuu wake, na kisa cha chai. Ule ulikuwa ni uchoyo uliopindukia! Kile kitabu nakikumbuka, ndio hicho chenye hadithi ya akina Juma na Damasi, waliokuwa wanapondana waziwazi. Enzi zetu walimu walikuwa na wito wa kweli wa kufundisha, walikuwa wakijituma sana, na kulikuwa hakuna wizi mkubwa wa mitihani kama ilivyo sasa, kwa sababu wanafunzi tulijiamini kwa kile tulichofundishwa, sio kama sasa, ualimu umekuwa biashara na kimbilio la 'failures' ambao hawana wito.
Kuhusu somo la jografia, ni kwamba wale watunzi wa vile vitabu walikuwa wameenda shule kweli. Vilikuwa bomba sana kwa mazingira yetu. Kitabu cha darasa la tano kilikuwa ni "Wafanyakazi wa Tanzania", darasa la sita ni "Wafanyakazi wa Afrika Mashariki", darasa la saba ni "Wafanyakazi wa Dunia".
Nakumbuka sana mambo ya "Kilimo Cha Mpunga Burma", "Kilimo cha Miwa Cuba", "Kilimo cha Mpira Malaya" na kadhalika.
 
Nakumbuka hadithi za:

Nondo mla watu....I think this was similar to Angela anaconda hehehe

Jogoo na panzi.....jogoo aliwika akisema "hapo ulipoooooooooooooo" badala ya "kokolikoooooooooooooooooooooooo"

Siku ya gulio katelero.......hii hata sikumbuki vizuri

Mshefa karumekenge na jitihada zake ka kukacha shule hehehehehe

Heri mimi sijasema........jamaa aliyezani kwamba kusema hajasema hakumaanishi amesema hehehehehe

Urafiki ni bora kuliko mwanasesere
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom