Tujikumbushe: Sitaki mbichi hizi...

mwakajingatky

JF-Expert Member
May 30, 2018
555
909
SIZITAKI MBICHI HIZI

Hadithi inayokuja, ni ya Sungura sikia,
Hadithi uliyongoja, leo ninakuletea,
Alitoka siku moja, njaa aliposikia,
Njaa aliposikia, Sungura nakuambia

Siku ile akaenda, Porini kutembelea,
Akayaona matunda, mtini yameenea,
Sungura akayapenda, mtini akasogea,
Mtini akasogea, Sungura nakuambia.

Sungura karukaruka, lakini hakufikia,
Matunda hakuyashika, mikononi hakutia,
Hakika alisumbuka, nguvuze zikapungua,
Nguvuze zikapungua Sungura nakuambia.

Mtazame hapo juu Sungura amelegea,
Mtazame na miguu, matunda anarukia,
Atafanya sikukuu, matunda akifikia,
Matunda akifikia, Sungura nakuambia.

Karuka tena karuka, matunda akarukia,
Mwisho Wave akachoka, kachoka hata mk-Ia,
Penye mti akatoka, pembeni akasogea,
Pembeni akasogea, Subgura nakuambia.

“Sizitaki mbichi hizi” Sungura akagumia,
“Naona nafanya kazi, bila faida kujua”,
Yakamtoka machozi matunda akalilia,
Matunda akalilia, Sungura nakuambia.

Sio kama hakutaka, sasa nakupasulia,
Matunda aliyataka, ndiyo kisa akalia
Tunajua hakufika, alichoka kurukia,
Alichoka kurukia, Sungura nakuambia.

Hadithi nimemaliza, nimekwisha simulia,
Jambo moja sikiliza, rafiki yangu sikta,
Usikose kujikaza, mazuri kukazania,
Utamshinda Sungura, utapata mbivu hizi.

UNAKUMBUKA WAPI?
Tunaweza ku-share ili na wengine waje kujikumbusha pamoja nasi.

Kukuletea hii ni Mimi Mwl wa Darasa la tatu isanga Primary School mbeyaa*
 
Bwana weee umesoma weye? mbona kapicha kasungura sikaoni?

weka tuone! nilisoma in advance kwa urahisi kukionea kiswahili sana , tena nilisoma kabla ya kufika mwaka wangu wa darasa kama utamu hivi ulinivutia na kujibu maswali ya mazoezi kabisa hivo mwalimu wangu Mrs Benigna, hakupata shida kabisa,

But lilipokuja swala la kana ka sungu mweru ee bana ee ilikuwa ni kitonga, Mwalimu wa somo aliitwa Mangaru korofi hilo
 
siku niliyonunuliwa hicho kitabu nilifurahi sana, furaha yangu ilikuja kuisha bandi ya kibanda cha msonge ktk kitanda changu cha kamba na godoro la sufi, nikiwa ninatumia mwanga wa kibatari kujisomea niliumwa tandu kwa yale maumivu nilitupa mkono kibatar kikaangukia kitandani mafuta yakasambaa godoro likashika moto kibanda kikaungua, nililia sana kwa maumivu niliyoyapata na ghetto langu kuungua pamoja na nguo za shule, moka mbili, chacha mbili na suti zangu za mchelemchele
 
Hahahahahahah hyo ni 90s
 
Haha muhenga 😀
 
Bwana weee umesoma weye? mbona kapicha kasungura sikaoni?
weka tuone! nilisoma in advance kwa urahisi kukionea kiswahili sana , tena nilisoma kabla ya kufika mwaka wangu wa darasa kama utamu hivi ulinivutia na kujibu maswali ya mazoezi kabisa hivo mwalimu wangu Mrs Benigna, hakupata shida kabisa,
But lilipokuja swala la kana ka sungu mweru ee bana ee ilikuwa ni kitonga, Mwalimu wa somo aliitwa Mangaru korofi hilo

Mkuu picha najaribu kuweka zinagoma....(sijui mods wamenipiga ban ya kuweka attachment)
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom