Mimi na pikipiki tu[emoji3][emoji3][emoji3]
1. Kuna siku nilikuwa nachota maji kwa pikipiki, sasa kuna mshkaji wangu akaja nyumbani akanikuta ndo nafunga ndoo za maji kwenye pikipiki ili niende kisimani. Kumbe mshkaji alikuwa anataka kuendesha pikipiki sema akawa anamgwaya mshua, sasa tulipo toka nyumbani tukiwa njiani jamaa akaanza kuomba nimpe naye aendeshe, ila nikawa nakataa kwa kuwa nilikuwa namjua jamaa ni mpenda sifa sana na kwa kuwa njia ilikuwa inapita hadi mtaani nilijua wazi angetaka kuonyesha kuwa yeye ni mtabe wa kukimbiza na usalama wetu ungekuwa mdogo. Ila akazidi kunisumbua nikaona isiwe tabu nikamwachia ila nikamsisitizia awe makini.
Bwana bwana, jamaa akapanda mimi nikapanda nyuma, akang'oa chuma. Nikawa naona jamaa anapandisha gia tu kila baada ya mita chache. Ndani ya dakika chache jamaa akawa ameshaikamata gia namba 5 huku spidi ikiwa ni kali sana. Mimi nikaanza kutoka na kijasho nimsihi jamaa apunguze mwendo lakini wapi.
Sasa tukafika sehemu kuna kona kali sana, na ukinyooka kwa mbele bila kukata hiyo kona kuna ka bonde halafu unakutana na reli iliyoinuliwa na kokoto. Sasa jamaa alivyoona kuwa hawezi kupiga kona ikabidi anyooke. Kwanza pikipiki iliruka na tukapita katikati ya miti ya vichaka vichaka, ilipokwenda kutua jamaa bado alikuwa na wenge akazidi kuvuta mafuta, nikaona tunaanza kupanda mlima wa kokoto za relini ikabidi niruke na kamaa akaenda kumamia juu ya makokoto. Cha kushukuru hatukuumia sana, ila pikipiki ilikuwa nyang'anyang'a.
2. Mimi na mshua tulikuwa tunatoka kwa bibi kuwasalimia, tukawa tunarudi nyumbani kila mmoja anaendesha pikipiki yake tukiwa tunapita kwa ile barabara ya dom-singida. Sasa mshua akawa anaendesha slow, nikaambua kumuacha mimi nikatangulia. Sasa likaja semi kwa nyuma likanipita nikasema wewe sikuachi, nikaanza kulifukuzia kwa nyuma ili nami nilipite. Tukaenda wee, baadayr nikasema sasa huu ndo muda wa kuovatake na nikaamua kuovateke kwa kushoto. Bwana wee, ile nakaribia kulipita nikaanza kuona semi linakuja kuande wangu kwa kasi, sijui ndo dereva alikuwa ananifanyia kusudi. Ikabidi nitoke barabarani nikaingia machakani huku nikijitahidi nisidondoke maana nilikuwa kasi sana. Kwa hofu iliyonikumba nikawana naendesha huku nalia kwa kupiga mayowe. Nikaenda kusimama kwa mbele kabisa nikiwa nimechubukachubuka. Niliwatukana sana wale jamaa.
3. Nikiwa na pikipiki yangu ile ile nikiwa nimetoka misele narudi nyumbani nikakuta mto umejaa maji japo hayakuwa mengi sana kiasi cha kutisha, nikasema hapa ntapita tu.
Mzee baba nikajitosa, kufika katikati ya mto ngoma ikazima. Ilipozima maji yakaingia kwenye dude la kutolea moshi, kwa hiyo hapo pikipiki kuwaka tena ni mtihani. Nikiwa sijui nifanyeje nikaona naanza nasombwa mimi na pikipiki yangu. Ikabidi nitoke nikaicha pikipiki ikaanza kubebwa baadaye nikawaza nikiiacha inaweza kwenda mbali na ikaharibika, ikabidi nijitose mtoni ili niitoe. Maji yaone kwenye glasi tu, shughuli iliyonipata pale mtoni nilianza kuwaona akina eskarioti na washkaji zake.