Tuliambiwa pesa za tozo za simu ndio zitatumika kwenye miradi ya afya na elimu sasa fedha za IMF je?

Mung Chris

JF-Expert Member
Sep 12, 2017
3,367
3,778
Waziri wa Fedha awe mkweli maana kama kajisahau vile anaendelea kutoa hotuba, alituambia fedha za tozo zitahusika kwenye Ujenzi wa madarasa na huduma za afya, leo hii fedha walizopewa na IMF anataja miradi ile ile kwamba ndio itakayo tekelezwa, huenda labda mm sijaelewa vizuri pamoja na kuwa nina experience ya ufadhili wa miradi kwamba mnaweza mkawapa wafadhili 3 ripoti ya mradi 1 ila kila mtu akawa alitoa peza za mradi huo huo.

Huenda sijaelewa kwamba fedha za tozo zitafanya kazi gani vile na hizi za IMF zitafanya kazi ipi vile.

Wakumbuke Wastaafu HAWAJALIPWA MAFAO yao sasa ni miezi 12 na zaidi kwa wengine.
 
Lol nchi ngumu hii
 
Ilikuwa ni mwanzoni mwa mwaka huu, serikali ilisema ilipokea mkopo kutoka benki ya dunia kwa ajili ya kujenga shule mpya 1000 nchi nzima.

Je, huko ulipo zimejengwa shule mpya ngapi?

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
Wanasiasa bhana sijui huwa wanatuchukuliaje sisi raia...mambo yao huwa hawanyooshi alafu wanajisahaulisha kama hawakuongea wao..
 
Waziri wa Fedha awe mkweli maana kama kajisahau vile anaendelea kutoa hotuba, alituambia fedha za tozo zitahusika kwenye Ujenzi wa madarasa na huduma za afya, leo hii fedha walizopewa na IMF anataja miradi ile ile kwamba ndio itakayo tekelezwa, huenda labda mm sijaelewa vizuri pamoja na kuwa nina experience ya ufadhili wa miradi kwamba mnaweza mkawapa wafadhili 3 ripoti ya mradi 1 ila kila mtu akawa alitoa peza za mradi huo huo.

Huenda sijaelewa kwamba fedha za tozo zitafanya kazi gani vile na hizi za IMF zitafanya kazi ipi vile.

Wakumbuke Wastaafu HAWAJALIPWA MAFAO yao sasa ni miezi 12 na zaidi kwa wengine.
mwana siasa si wa kuamini maneno yake, anaongea macho makavu na hapepesi. hakuna mwana siasa mkweli. uliambiwa tozo ni kwa nia njema (maneno toka kinywani mwa mh rais), leo mawaziri 8 wanazunguka na helicopter nchi nzima wakitatua kero za ardhi (walipa tozo?).
 
Yule aliyepaishwa mawinguni alikopa na kufadhiliwa miradi na mabeberu lakini alidai miradi yote inatekelezwa kwa fedha za ndani lakini mlikuwa mnashingilia tu bila kuhoji inakuwaje deni linazidi kukua wakati miradi yote tunajenga wenyewe kwa fedha za ndani.
 
Kunafedah za world bank zaodi ya trillion 1 zinakwenda kubolesha elimu..sasa mbona hatumabiwi tofauti ya hizi fedha..Naona kunaupiganji sana
 
Wanasiasa na watu waongo sana na was hovyo sana, bahati mbaya sana wao ndio wanaendesha nchi na kufanya maamuzi ya kisiasa na kiuchumi.
 
Kunafedah za world bank zaodi ya trillion 1 zinakwenda kubolesha elimu..sasa mbona hatumabiwi tofauti ya hizi fedha..Naona kunaupiganji sana
Hizi fedha sidhanimkama zimefika bot/hazina!!! Kuna kiswahili kingi sana kinapigwa juu ya fedha hizi za elimu!
 
Kunafedah za world bank zaodi ya trillion 1 zinakwenda kubolesha elimu..sasa mbona hatumabiwi tofauti ya hizi fedha..Naona kunaupiganji sana
Zile trilion moja walisema watajenga shule mpya elfu moja nchi nzima. Huku napoishi sijaona hata shule mpya moja, hata msingi tu, sijui huko!

Baadae wakasema, tozo za miamala zitatumika kuboresha afya, elimu, barabara za mijini na vijijin etc.

Leo wamekuja na taarifa kwamba, watajenga madarasa elfu 15 kwa fedha za IMF.

Nani atusaidie kuhoji huko mamlakani ili tupate ufafanuzi kati ya fedha zile kutoka World Bank na hizi za IMF?

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
pesa zote za IMF ni mkopo hivyo basi tozo zinatumika kulipa huo mkopo,na mikopo mingine iliyokuepo
 
Mwanasiasa ni Kama mwanamke anaweza kukuomba hela ya kitu cha mhimu kumbe ana hesabu zake

Siyo wa kuwaamini hawa
 
Back
Top Bottom