Mbunge Esther Malleko aeleza Kilimanjaro ilivyonufaika na fedha za miradi ya maendeleo

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,897
942
MBUNGE ESTHER MALLEKO AELEZA KILIMANJARO ILIVYONUFAIKA NA FEDHA ZA MIRADI YA MAENDELEO

"Mheshimiwa Rais ametupatia fedha kwaajili ya ujenzi wa kuimarisha vituo vya afya na utoaji huduma katika Zahanati 35 katika Mkoa wa Kilimanjaro ambapo ametupatia Shilingi Bilioni 2.59 na Shilingi bilioni 4 katika ujenzi wa vituo vya afya katika Halmashauri za Moshi Mjini, Mwanga, Hai na Rombo" - Mhe. Esther Edwin Malleko, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Kilimanjaro

"Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ametupatia fedha kwaajili ya ujenzi wa Majengo ya Hospitali za Wilaya zote Saba ambapo ametupatia Shilingi Bilioni 7.9" - "Mhe. Esther Edwin Malleko, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Kilimanjaro

"Kwenye Sekta ya Elimu, tumeweza kupatiwa Shilingi Bilioni 21 ambazo zimetumika katika ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya Elimu na uhifadhi wa Mazingira kwa shule za Msingi na Sekondari na Shilingi bilioni 6.3 kwaajili ya mpango wa Elimu bila malipo" - Mhe. Esther Edwin Malleko, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Kilimanjaro

"Katika sekta ya Maji tunampongeza sana Mheshimiwa Rais, ameweza kutupatia Shilingi Bilioni 6.29 ambazo zimeenda kwenye ukarabati na kuhakikisha zinatumika katika kuongezeka kupatikani kwa Maji Safi Vijijini" - Mhe. Esther Edwin Malleko, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Kilimanjaro

"Katika kupambana na Umasikini na uwezeshaji wananchi kiuchumi katika Mkoa wa Kilimanjaro Kaya Masikini 41,108 wameweza kugawiwa Ruzuku. Tunashukuru kwasababu walengwa 27,472 wamepewa ajira za muda katika miradi 604 ambayo inaendelea katika Halmashauri Saba za Mkoa wa Kilimanjaro" - Mhe. Esther Edwin Malleko, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Kilimanjaro

"Ninawashukuru sana viongozi wangu wa Chama na Serikali katika Mkoa wangu wa Kilimanjaro na Wanawake wa Mkoa wa Kilimanjaro kwa namna ambavyo wananipa ushirikiano ili kuweza kutimiza Majukumu yangu kila siku kama Mbunge. Ninawaahidi nitaendelea kushirikiana nao hatua kwa hatua ili kuweza kutimiza wajibu wetu kama wawakilishi katika Mkoa wa Kilimanjaro" - Mhe. Esther Edwin Malleko, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Kilimanjaro.
WhatsApp Image 2023-10-05 at 16.08.18.jpeg
 
Back
Top Bottom