Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) Lafikia Makubaliano ya Ngazi ya Wafanyakazi na Serikali Kuhusu Mapitio ya Pili ya Mpango wa Ukopeshaji wa ECF

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,987
Washington, DC - Novemba 3, 2023: Wafanyakazi wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) wakiongozwa na Charalambos Tsangarides, ambaye ni mkuu wa ujumbe wa IMF kwa Tanzania, walifanya mikutano Dodoma na Dar es Salaam kuanzia Oktoba 23 hadi Novemba 3, 2023, ili kujadili maendeleo ya mageuzi na vipaumbele vya sera za serikali katika muktadha wa mapitio ya pili ya mpango wa ukopeshaji wa ECF wa muda wa miezi arobaini kwa Tanzania.

Mpango huo uliidhinishwa na bodi tendaji ya IMF mnamo Julai 18, 2022, kwa jumla ya SDR 795.58 milioni (sawa na dola za Marekani bilioni 1.046 wakati huo) Mwishoni mwa ziara yake, Tsangarides ameitoa taarifa ifuatayo:

“Ninafurahai kutangaza kwamba mamlaka za Tanzania na wafanyakazi wa IMF tumefikia makubaliano ya ngazi ya wafanyakazi kuhusu sera za kiuchumi ili kuweza kuhitimisha mapitio ya pili ya mpango wa ukopeshaji kwa Tanzania chini

Makubaliano ya ngazi ya wafanyakazi yatategemea kuidhinishwa na uongozi na Bodi Tendaji ya IMF wiki zijazo.

Baada ya kukamilika kwa mapitio ya Bodi Tendaji, Tanzania itapata SDR113.37 milioni (kama dola za Marekani milioni 150), na kufanya jumla ya msaada wa kifedha kutoka IMF chini ya mpango huu kufikia SDR342.1 milioni (kama dola za Marekani milioni 452.7).

Mpango wa mageuzi wa Serikali unalenga kuimarisha ufufuaji wa uchumi, kulinda uthabiti wa jumla wa kifedha, na kusaidia ukuaji wa uchumi thabiti, endelevu na shirikishi.

“Baada ya ahueni ya kukua kwa wastani wa asilimia 4.9 mwaka 2021, ukuaji halisi wa Pato la Taifa ulipungua hadi asilimia 4.7 mwaka 2022, ukiakisi athari za mazingira mabaya ya uchumi wa dunia na ukuaji duni wa kilimo kutokana na mvua chache.

Ahueni hiyo inatarajiwa kuimarika kuanzia mwaka wa 2023, lakini itakabiliwa na misukosuko itakayotokana na uchumi wa dunia, ikijumuisha kuyumba kwa bei za bidhaa, ukuaji duni, na hali ngumu ya kifedha duniani.

Mfumuko wa bei ulipungua hadi asilimia 3.3 (mwaka kwa mwaka) mwezi Septemba kutoka kwenye kiwango cha juu cha asilimia 4.9 mwezi Januari 2023. Matarajio ya muda wa kati yatategemea utekelezaji thabiti wa ajenda zilizopo kwenye mpango wa mageuzi wa serikali, unaoungwa mkono na mpango wa ECF.

"Nakisi kubwa kwenye mauzo na manunuzi ya bidhaa na huduma nje ya nchi (kama asilimia 6 katika mwaka wa fedha 2022/23) ikiambatana na hali ngumu ya kifedha duniani imesababisha shinikizo katika soko la fedha za kigeni.

Benki Kuu ya Tanzania iliongeza kasi cha mauzo ya fedha za kigeni ili kuongeza ukwasi kwenye soko, huku ikiruhusu viwango vya ubadilishaji fedha za kigeni kuongezeka kwa kasi zaidi kuliko hapo awali tangu mwezi Julai.

Benki Kuu ya Tanzania imesisitza dhamira yake ya kufufua soko la fedha za kigeni baina ya mabenki, kuhakikisha viwango vya ubadilishaji fedha za kigeni vinatokana na nguvu za soko, na Benki Kuu ya Tanzania kuingia kwenye soko pale tu inapogundulika kuna msukosuko kwenye soko. Kuendelea na sera ya fedha inayolenga kupunguza ujazi wa fedha kwenye uchumi kutasaidia pia juhudi za kupunguza shinikizo katika soko la fedha za kigeni.

"Kwa upande wa sera ya mapato na matumizi ya serikali, serikali imesisitiza kuendelea kutekeleza mpango wa kubana matumizi kama ulivyoainishwa katika bajeti ya mwaka wa fedha 2023/24, ambayo imejikita katika makadirio halisi ya mapato na matumizi. Juhudi za sera za kodi na usimamizi wa ukusanyaji wa mapato zitasaidia kuongeza nafasi ya matumizi zaidi ili kushughulikia mahitaji makubwa ya wafanyakazi na uwekezaji kwenye miundombinu.

Aidha, Serikali imedhamiria kusawazisha muundo wa matumizi kwa ajili ya kipaumbele cha matumizi ya huduma za kijamii ili kupunguza mapungufu katika utoaji wa huduma za elimu na afya na kuimarisha ulinzi wa kaya maskini.

Maboresho ya mazingira ya biashara na utawala bora ni muhimu katika kufungua fursa zilizoko kwenye uchumi wa Tanzania.

Katika suala hili, Serikali itaendelea kutekeleza Mwongozo wa Maboresho ya Udhibiti (Blueprint for Regulatory Reforms), kwa kuzingatia uboreshaji wa kanuni na kuimarisha utawala bora. Juhudi za kupunguza hatari za mabadiliko ya tabianchi kwa kuwekeza katika sera za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi zitasaidia kujenga msingi imara wa ukuaji wa uchumi thabiti na endelevu.

“Ujumbe wa wataalam kutoka IMF ulikutana na Waziri wa Fedha Mwigulu Nchemba, Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Emmanuel Tutuba, viongozi wengine waandamizi wa serikali, washirika wa maendeleo, na wawakilishi wa sekta binafsi.

Ujumbe wa wataalam kutoka IMF unapenda kuzishukuru mamlaka za Tanzania kwa ushirikiano wao, ukarimu na mijadala yenye kujenga.”
 

Attachments

  • PDF.pdf
    127.4 KB · Views: 3
Watupe hela kumalizia SGR hali mbaya sana Serikali imeshindwa kuwalipa Yepi muda mrefu sana sasaaa.....
 
Back
Top Bottom