Tukumbushane miiko ya mila zetu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tukumbushane miiko ya mila zetu

Discussion in 'JF Chit-Chat' started by Kitty Galore, Jul 10, 2011.

 1. Kitty Galore

  Kitty Galore JF-Expert Member

  #1
  Jul 10, 2011
  Joined: May 24, 2011
  Messages: 347
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Wadau najua kila mmoja ana mila za kwao. Hebu tukumbushane kidogo miiko yetu ili hata ambao hawazijui waweze kufahamu kwamba zilikuwepo. Hapa haijalishi ni kwa kabila, koo n.k
  Mfano:
  1. Mwanamke akiwa anasonga ugali mwiko ukivunjikia sufuriani ni mbaya (sijui ubaya wake ni nini)
  2. Mtoto akianza kuota meno ya juu, akija kuoa/kuolewa mwenza wake atakufa,
  3.
  4.
  Tuendelee
   
 2. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #2
  Jul 10, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  1. Mtoto wa kike akikaa katikati ya mlango hatoolewa. 2. Mtu akikuruka hutorefuka. 3. Ukijiangalia kwenye kioo usiku sikumbuki utafanya nini ila inatisha.
   
 3. Preta

  Preta JF-Expert Member

  #3
  Jul 10, 2011
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 24,113
  Likes Received: 3,036
  Trophy Points: 280
  Ukipiga mluzi usiku nyoka anakuja
  Ukisimulia hadithi mchana, unaota mkia
   
 4. D

  Derimto JF-Expert Member

  #4
  Jul 10, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 1,305
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Ukimsemea ndege jikoni hautamkamata tena.

  Usiku ukiingia usiende kuomba chumvi kwa jirani nk.
   
 5. Preta

  Preta JF-Expert Member

  #5
  Jul 10, 2011
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 24,113
  Likes Received: 3,036
  Trophy Points: 280
  Hii inanikumbusha.....ukienda kununua chumvi usiku usiseme chumvi sema dawa ya mboga
   
 6. Babuu blessed

  Babuu blessed JF-Expert Member

  #6
  Jul 10, 2011
  Joined: Oct 14, 2010
  Messages: 1,340
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 145
  Ukikojoa kichakani tema tema mate ili mama asivmbe matiti,
  mtoto wa kiume aruhusiwi kukaa jikoni! Firigis ni ya baba na maini! Ila mjin kilamtu anakula ni pesa yako lol!
   
 7. A

  Apta Kayla JF-Expert Member

  #7
  Jul 10, 2011
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 326
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mtoto mchanga akiangalia kioo haoti meno, ukimuona zeru zeru usipojitemea mate kifuani nawe utazaa zeru zeru.
   
 8. bombu

  bombu JF-Expert Member

  #8
  Jul 11, 2011
  Joined: Jun 8, 2011
  Messages: 1,134
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145
  1. binti akipika huku aimba, ataolewa mbali
  2. kijana wa Kiume akipigwa na mwiko, hatooa
   
 9. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #9
  Jul 11, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,089
  Likes Received: 6,555
  Trophy Points: 280
  nitarudi, mmenikumbusha mambo makuu ya kale.
   
 10. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #10
  Jul 11, 2011
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  kuku akichinjwa na nyama yake kupikwa FIRIGISI ni ya baba hahaaa. huruhusiwi kupiga mluzi nyumbani ni baba peke yake anaruhusiwa. ukipiga mluzi usiku unaita nyoka.
   
 11. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #11
  Jul 11, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,247
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180
  1. usikalie kinu mwanamke hutajaaliwa kuzaa
  2. usitupe nguo yako ama kitambaa chochote chenye hedhi for mbaya wako akitupia jicho huzai...
  3. Ukiona zeru zeru temea mate kwenye blouse ili nawewe usizae zeruzeru (THIS IS DELICATE I KNOW) Natoa ili tuweze ona ni jinsi gani imani nyingine zilikua za kijinga kabisaa!!
  4. Mwanaume asilie kwenye sufuria la sivyo siku ya ndoa yake mvua nzito itanyesha...
   
 12. kinyoba

  kinyoba JF-Expert Member

  #12
  Jul 11, 2011
  Joined: Jun 2, 2011
  Messages: 1,238
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  ni mwiko kwa mwanamke kumwambia mumewe ana hamu ya kukazwa! Ni mwanaume tu ndo mwenye ruhusa ya kuanzisha game usiku.
   
 13. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #13
  Jul 12, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,089
  Likes Received: 6,555
  Trophy Points: 280
  Unamdanganya, siku akikugundua utashangaa.
   
 14. Mentor

  Mentor JF-Expert Member

  #14
  Jul 12, 2011
  Joined: Oct 14, 2008
  Messages: 18,707
  Likes Received: 8,250
  Trophy Points: 280
  Jamani...naomba tu tuseme hii miiko tulifundishiwa wapi maana zote zinakaa za uchagani uchagani...ama ndo miiko meingi ya kitanzania inaendana!??
   
 15. Mentor

  Mentor JF-Expert Member

  #15
  Jul 12, 2011
  Joined: Oct 14, 2008
  Messages: 18,707
  Likes Received: 8,250
  Trophy Points: 280
  Hao ni wababa wa wapi hawajui mambo...
  Kwetu uchagani...KIDARI ni baba...damn, natamanije ningeishi miaka hiyo!!!!
   
 16. Ms Judith

  Ms Judith JF-Expert Member

  #16
  Jul 12, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 2,569
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  1. singles wakila chakula wamekaa kitandani hawataoa katu

  2. wavulana wakikojia mtoni siku ya kupashwa tohara watavuja damu itiririke hadi pale mtoni walipokojoa
   
 17. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #17
  Jul 12, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  Kwa watoto wa kike wakiwa wanajifunza kupika wakiungua ndio dalili ya kujua.
   
 18. First Born

  First Born JF-Expert Member

  #18
  Jul 12, 2011
  Joined: Jul 11, 2011
  Messages: 5,315
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 145
  Mwanamke hahusiki na urithi wa chochote, yeye ni wa kuolewa tu.
   
 19. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #19
  Jul 12, 2011
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Ashadii dadaa, mbona unaniangusha, yaani uoni hikma yake kwenye hizo taboo?

  Kabla sijadadaua, inakupasa utambue kwanini waliweka hiyo miko, kwenye jamii. Kwanza ili kutunza kuheshimiana, kutodharauliana na dhana nzima ya usafi wa mwanamke na vitendea kazi.

  Kila mtu anaelewa kazi ya kinu, ni kutwanga/kukoboa nafaka, iki ni kifaa muhimu sana na kinatakiwa kupewa hishma yake ili kibakie kwenye hali ya usafi, na ndio maana miko mingi ipo kwenye dhana ya kutishana ili watu waifuate. Ebu mwenyewe fikiria umkute mtu kakalia kitu upande ule wa kutwangia, kisha akipumulie, na kesho atwangie humo humo.
  Mf: Ukitaka kuwatisha wanaume wasinywe/kula kinywaji/chakula fulani basi waambie kuwa kula/kunywa kutawapunguzia nguvu za kiume. Ni rahisi sana kuacha kuliko wangeambiwa kutawapelekea kupata saratani (cancer) japo ndio ukweli.

  Sasa hapa ujui kuwa wanawake wanatakiwa kuwa wasafi, wao na mazingira yao, hivi kila mwanamke kijijini au mjini au uko mitaani akitupa hizo Space Shuttle za kuendea mwezini, ujui kuwa ni kueneza maradhi kwenye jamii inayo wazunguka.

  Hapa tuaelekezwa kuonyesha kuheshimiana, kama wewe unamuona zeruzeru ni mchafu au anakuchefua kwa arufu yake basi temea mate kwenye brouse yako (kama unaweza).

  Mwanaume kulia kwenye sufuria ni dalili ya ulafi, kinachokufanya mpaka ule kwenye sufuria ni nini? Ndio wakatishwa kwa kuambiwa hayo waliyo ambiwa.

  Kuna lingine dadangu!?
   
 20. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #20
  Jul 12, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,247
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180

  Bora nimekukuta hapa for now i remember deni... Aalafu XP
  nakubali hio misemo ila tu huo wa zeru zeru ndio niliosema haufai....
  Ndio maana nikasema mila zingine (note sio yooote...)
   
Loading...