Jinsi ya kujenga Familia imara Karne ya 21

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,340
51,900
JINSI YA KUJENGA FAMILIA IMARA KARNE 21

Anaandika, Robert Heriel

Kila mtu duniani anapenda angezaliwa kwenye familia ya Baba na Mama, yenye upendo. Hakuna kama tabasamu lenye upendo ndani ya Familia. Malezi na makuzi ya Watoto ndani ya familia imara humjenga mtoto kuwa mtu Bora mwenye manufaa.

Baada ya kuzaliwa na Kukua kila mtu hufikiri na Kuota ndoto ya kuanzisha familia yake, kuwa na MKE au Mume WA ndoto yake, na watoto wazuri wenye adabu na utiifu.

Familia imara ni nini na ikoje?
Familia imara ni familia yenye kufuata misingi na Maadili ya kifamilia katika kulinda na kutekeleza Haki, wajibu na Majukumu ya wanafamilia.

Familia imara inamambo makuu yafuatayo:

1. UPENDO
2. Sheria, Haki na Hukumu.
3. Maadili, Dini, miiko, Mila na desturi
4. Mali

Sheria za familia ndizo zitaelezea muundo, wajibu na Majukumu ya wanafamilia Kwa kusaidizana na Maadili, miiko, Mila na desturi. Dini ya familia lazima ifungamane moja Kwa moja na asili ya wanafamilia, mfano Kama Wanafamilia ni Wazungu, dini yao inatakiwa iwe yenye asili na uzungu. Mzungu hawezi kuabudu katika dini au miungu ya Waafrika au Wachina au Waarabu. Halikadhalika na Muafrika hapaswi kuabudu katika miungu isiyo na asili na Uafrika, Kwani Kwa kufanya hivyo moja Kwa moja itahesabika kama kuangusha ngome yake (asili yake mwenyewe) na huo utaitwa mmomonyoko wa maadili.

Muundo wa Familia uzingatie Akili, maumbile, utashi, majukumu na wajibu wa wanafamilia. Kwa mfano kama Mwanaume ndiye mwenye nguvu na Akili basi yeye ndiye atapaswa awe Mtawala/mfalme wa familia. Na endapo MKE ndiye atakayekuwa na nguvu na Akili zaidi ya mwanaume basi Mwanamke ndiye awe Mtawala/mfalme katika familia.

Nguvu itahusisha, nguvu ya kimwili, Kiroho, kihisia na Kiakili. Yeyote atakayekuwa na Robo tatu ya hayo mambo Matatu kumzidi mwenzake ndio awe Mtawala. Familia imara inajengwa na Mtawala imara, mwenye nguvu na Akili nyingi.

Lazima ujue unataka kujenga familia imara ya namna ipi, hiyo itakusaidia kumchagua mwenza mtakayefanya wote Maisha.

Karne ya 21 inahitaji kizazi kinachotumia zaidi Akili kuliko nguvu lakini haimaanishi nguvu hazihitajiki, nguvu zinahitajika kwenye dharura.

Jinsi ya kujenga Familia imara Karne ya 21 ni kama ifuatavyo:

1. JIIMARISHE
Jiimarishe kifikra, kihisia, kiroho, Kimwili, kiuchumi na kijamii.

a) Hakikisha unakuwa imara kimwili
Kwa Kula vizuri vyakula vya asili, fanya mazoezi kama wewe sio mtu wa kazi ZENYE nguvu. Lakini kama kazi zako unatumia nguvu, usifanye mazoezi. Hakikisha unakuwa na afya ya mwili imara. Hii itakufanya uwe na nguvu za kiume na pia uwe na Mwili wenye kuvutia.

Kisha imarisha mwonekano wako, kuwa mtanashati kama kijana au Baba au Babu, kuwa Mrembo kama ni Binti au Mama au Bibi. Hiyo itakufanya uwe na familia imara, Watoto na Mwenza wako watazidi kukupenda sio Kwa kujilazimisha bali Kutokana na Mvuto wako.

Familia nyingi huanguka ikiwa mmoja wa wanafamilia endapo hatakuwa imara kimwili, Nani atajivunia MTU mchafu. Nani atavumilia MTU asiye na nguvu za kiume au zakike Wakati wa tendo.

Mwili ni pamoja na vile unavyotembea, tembea kama MTU imara mwenye kustahili heshima, usitembee upande upande kama Gari Bovu, au usipinde mgongo kama MTU dhaifu. Kaa mkao wa kujiamini na MTU mwenye kutumainiwa, kama ni Mwanamke kaa na tembea kama Mwanamke kulingana na umbo na umri wako. Kama ni Mwanaume kaa na tembea kama Mwanaume, sio unalegeza mwili na Matako kama Mwanamke. Jikaze.

Ongea kama Mwanaume, pangilia Sauti na maneno yawe imara yenye kuvutia kiasi kwamba Watoto wakikusikia ukizungumzia wanasema This is my Father, Sauti na maneno yako yaonyeshe heshima, utukufu, Akili na hekima lakini pia mara moja moja yaonyeshe wewe sio mtu unayependa ujingaujinga na kamwe sio MTU wa kukaribiwa na watu wa hovyohovyo.

b) Jiimarishe Kiakili
Itunze Akili yako ikutunze, itumie Akili yako ikusaidie. Imarisha Akili yako Kwa kujifunza vitu vipya vizuri vitakavyokujenga kiheshima. Akili inajengwa Kwa kuona, kusikia, kuhisi na kutafakari. Namna Bora ya kujifunza ni kuyatazama mazingira na Maisha yanayokuzunguka, jifunze Tabia za viumbe, jifunze habari za nyakati, wakati, siku na miaka, jifunze Tabia za nchi na Hali ya hewa. Kuwa MTU wa kutafakari vitu Kwa kina.

Jifunze namna ya kuifanya Akili yako isizoee, isiwe na mazoea na kuamini vitu kirahisi. Jifunze kujua mipaka ya vitu, Maeneo na viumbe(ikiwemo Watu).

Akili ndio itaamua ndoa na familia yako iwe imara yenye furaha au iwe familia dhaifu yenye majuto na mteso

c) Jiimarishe kiuchumi
Fanya kazi, zalisha Mali, kufanya Mali za muda na zakudumu. Mali za muda lengo lake kubwa ni kukurahisishia Maisha na kukufanya uwe na furaha mathalani, kununua magari, au Mashine zozote zile vyote hivyo utavihitaji. Na ili uvipate ni lazima ufanye Kazi. Mali za kudumu hizi zimelenga zaidi HATMA yako ya uzeeni na vizazi vyako, Mali hizo ni kama Nyumba za kuishi, mshamba, viwanja n.k.

Mali hizi ni muhimu kuzipigania, kuna namna mbalimbali ya kukusanya utajiri/Mali Kwa lengo la kujiimarisha na kujenga familia imara; chache Kati ya hizo:

I) Miliki Mali upate Mali zaidi
ii) Miliki Watu upate utajiri na muda zaidi
iii) Tatua tatizo linalosumbua Watu upate Mali.
iv) Anzisha janga/tatizo ukiwa na suluhisho upate Mali.
v) Tengeneza hofu na ugumu baina ya Watu na fursa. Au wafanye Watu vipofu alafu wewe uwe kiongozi wa vipofu lakini uwe unaona. N.k.

Ukishajiimarisha kiuchumi, hakikisha unayeenda kumuoa au kuolewa naye awe naye yupo imara kama wewe au mnakaribiana, ni lazima kuwe na Uwiano unaokaribiana baina ya wanafamilia katika masuala mengi ikiwemo suala la uchumi. Hii itawasaidia sio ninyi tuu Bali hata Watoto mtakaowazaa watakuwa imara na spirit kama ya ninyi wazazi wao.

Uchumi unahitaji Akili ya kuona fursa, kuona siku zijazo lakini pia inahitaji Uthubutu wa kuzifuata fursa hizo na kukabiliana na changamoto. Hayo yote yanamhitaji mtu jasiri na hodari katika kuyakabili.

Uchumi pia unahusu zaidi uses of resources "Utumiaji wa Rasilimali" ikiwemo Mali za MTU mwenyewe kama Nguvu, Akili na Roho. Kisha Kutumia mazingira.

d) Jiimarishe Kiroho na Kihisia
Ni lazima uwe imara na sugu Kiroho na Kihisia. Lazima ujifunze kuvumilia maswahibu ya kidunia, ujifunze tiba za majanga ya Kiroho na Kihisia.

2. TAFUTA MWENZA MNAYEFANANA NA KUENDANA
Familia ni kama serikali, Familia ni ishu ya kiutawala zaidi. Inahusu uongozi, wajibu na Majukumu.
Unapoenda kuanzisha familia sio ishu ya kuenda kwenye igizo la Telemundo, sio ishu ya maonyesho.
Hapo ni ishu ya kiutawala, mamlaka, Serikali. Ni Mwanadamu mjinga tuu asiyejua Jambo hili. Ikiwa wanyama kama kina Simba Bob Junior anajua kabisa ishu ya kuanzia familia ni ishu kiutawala sembuse Sisi binadamu?

Unapomzungumzia familia hapo unazungumzia Kingdom"ufalme". Ni lazima uteua na kuchagua mwenza ambaye hataiangusha falme yako. Sio ujiokotee hovyohovyo Kwa Kutumia hisia kuliko Akili.

Vigezo vya kuchagua mwenza mnayefanana na kuendana;
a) Ni lazima ujiangalie wewe ni mtu wa Aina gani, kuanzia Maumbile yako, Akili yako, hisia zako, Roho yako na Hali yako ya kiuchumi. Yaani utamchagua mtu kulingana na wewe ulivyo. Bahati nzuri kila MTU anajijua.

Hakikisha msipishane Sana kimaumbile, kizuri na muonekano. Sio kijana mfupi unataka kuoa Mwanamke mrefu, au unajijua unamboo ndogo alafu unataka kuoa Mwanamke mwenye Uke mkubwa, hakunaga upendo Kwa Watu wasiofanana au kuendana, hakunaga kitu kama hicho.

Angalia ndoto ya huyo unayetaka kumuoa au kuolewa naye zinafanana, sio mwenzako anataka kuwa Maarufu alafu wewe unataka familia yako iwe Low Key, mtapishana.

Je, mnafanana kitabia? Kikawaida Duniani hakuna Tabia Mbaya au chafu, isipokuwa Tabia Mbaya ni pale Watu Wawili wasipofanana tabia au kimaadili wanapoamua kuwa pamoja. Hiyo ndio Tabia Mbaya.
Ulevi kwako ni Tabia Mbaya, je Kwa mwenzako Ipo hivyo?
Umalaya kwako ni Tabia Mbaya, je Kwa mwenzako Ipo hivyo?
Au yeye atakukubalia tuu ili akupate kisha baadaye akusumbue?
Wanasema Dunia ni moja lakini kila binadamu ana Ulimwengu wake.
Walevi Kwa walevi
Wachawi Kwa wachawi
Watakatifu Kwa watakatifu.

Kamwe usifanye kazi ya kumbadilisha MTU, Huko ni kupoteza Muda wako tuu.
Kama MTU anatabia ambazo haziendani na wewe ni Bora uachane naye mapema Kabla hamjaingia kwenye ujenzi wa familia. Kwani sio kwamba utakwama wewe Bali hata kizazi chako kitakwama.

Kwa leo Taikon niishie hapa. Nipumzike sasa.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
 
Back
Top Bottom