Tukubali au tukatae, lipo tatizo kubwa sana katika sekta ya nishati ya umeme hapa nchini kwetu Tanzania

Uzima Tele

JF-Expert Member
Jan 20, 2023
1,099
2,342
Hili la umeme kwangu mimi Uzima Tele ndilo pekee hunifanya nimkumbuke kwa uzuri hayati Rais John P. Magufuli kuwa alifanya vyema chini ya u - Rais wake.

Honestly, katika kipindi cha uongozi wake ni kama aliona tatizo lilipokuwa, akachukua hatua na kulidhibiti na kukawa na hali ya utulivu ya upatikanaji wa nishati hii muhimu katika kujenga uchumi wa nchi..

Katika kipindi cha u - Rais wake huyu mwamba (Jiwe), hali ya upatikanaji nishati ya umeme hapa nchini ilikuwa very stable. Hata kama kulikuwa na kukatika umeme, basi ilikuwa na mara moja moja sana tena kwa sababu maalumu.

Tangu kutokea kwa kifo cha John P. Magufuli na huyu mama Samia Suluhu (Rais wa kigeni toka nchi jirani ya Zanzibar)kupokea kijiti, tukarudi nyuma hatua nyingi tulikotoka kwenye enzi za giza la mgawo na kukatikatika ovyo kwa umeme.

Hapa ninvyoongea huku kwetu, leo hii pekee (jumapili ya leo tarehe 30/4/2023), umeme upo lakini hauko stable na umekatika zaidi ya mara 20 kwa interval ya chini ya saa moja Kila mkatiko. Hii imekuwa hivyo siku zote tangu tangu huyu mama achukue uongozi wa nchi hii...!!

Hivi shida ni nini? Huyu mzee, Hayati John P. Magufuli (CCM) alifanya nini ambacho serikali chini ya Rais Samia Suluhu (ambaye naye ni WA chama kilekile yaani CCM) inashindwa kufanya?

Kuna nini katika sekta hizi; ya nishati ya umeme, mafuta ya jamii ya petrol na madini..? Je, ndiko dili za kifisadi za upigaji hela za wananchi (umma) za viongozi wa serikali hii ya CCM zilipo?

Je, hata wewe Rais Samia Suluhu tunayeambiwa kuwa u - mwislamu safi unahusika kwenye dili hizi za kifisadi Kwa gharama ya maisha ya watu wako unaowaongoza...? Kama huhusiki, kwanini umenyamaza kimya kana kwamba huluoni tatizo?

Inakuwaje kuwe na tatizo lilelile miaka yote, miezi yote na siku zote na wahusika (serikali) wakitoa majibu yaleyale bila ufumbuzi wowote?

Kiukweli, lazima tukubali leo kuwa, katika sekta hii ya NISHATI YA UMEME na PETROL na MADINI lipo tatizo kubwa linalohitaji ufumbuzi nje kabisa ya watu hawahawa chini ya CCM waliolitengeza tatizo hili. Kwa sababu tatizo hili haliwezi kuondolewa na watu wenye akili hiyo hiyo iliyosababisha ...!!!
 
Nakubaliana nawe kuwa sekta ya NISHATI na MADINI lipo tatizo kubwa. Sekta ya madini ni fursa ya kudhoofisha uzalishaji wa bidhaa za ndani na ya madini ni kuruhusu wachimbaji wa nje nchi ikiachiwa mashimo na kuifanya shamba la bibi (ona kiambatanisho)
20230430_230550.jpg
 
Mwanzo waliingia madarakani kwa mbwembwe wakata kuonesha kila alichofanya mwendazake alikuwa anakosea.

Wakapewa muda watuoneshe ujuzi wao, baada ya hapo tukaanza kuona sarakasi za kila aina, waziri kuunda bodi, mara akatengeneza dili la maintanance $30 mil, ukitazama haya yote ni upigaji tu, wala hakuna lolote lililowezesha kuimarisha upatikanaji wa umeme.

Ndio maana sishangai ulipoandika kwako unakatika zaidi ya mara ishirini kwa siku, na hauko stable, hakuna utendaji wowote wa maana unaoendelea wizara ya Nishati kwa sasa zaidi ya porojo, ujuaji, na upigaji, huku ukisindikizwa na Rais asiyetaka kuhangaisha kichwa chake.
 
Nenda kazikwe naye, bado Kuna nafasi kubwa pale, tafuta tu shuka jeupe, wakukuchimbia utawakuta huko
 
Kuongoza nchi ni science sio siasa. Waliingia na siasa kibao. Ooh ukame, ooh mitambo chakavu, ooh bodi ya tanesco kikwazo, ooh inahitajika forklift..wamedemadema wee sasa wanaishia kujipaka kinyesi tu.
 
Hili la umeme kwangu mimi Uzima Tele ndilo pekee hunifanya nimkumbuke kwa uzuri hayati Rais John P. Magufuli kuwa alifanya vyema chini ya u - Rais wake.

Honestly, katika kipindi cha uongozi wake ni kama aliona tatizo lilipokuwa, akachukua hatua na kulidhibiti na kukawa na hali ya utulivu ya upatikanaji wa nishati hii muhimu katika kujenga uchumi wa nchi..

Katika kipindi cha u - Rais wake huyu mwamba (Jiwe), hali ya upatikanaji nishati ya umeme hapa nchini ilikuwa very stable. Hata kama kulikuwa na kukatika umeme, basi ilikuwa na mara moja moja sana tena kwa sababu maalumu.

Tangu kutokea kwa kifo cha John P. Magufuli na huyu mama Samia Suluhu (Rais wa kigeni toka nchi jirani ya Zanzibar)kupokea kijiti, tukarudi nyuma hatua nyingi tulikotoka kwenye enzi za giza la mgawo na kukatikatika ovyo kwa umeme.

Hapa ninvyoongea huku kwetu, leo hii pekee (jumapili ya leo tarehe 30/4/2023), umeme upo lakini hauko stable na umekatika zaidi ya mara 20 kwa interval ya chini ya saa moja Kila mkatiko. Hii imekuwa hivyo siku zote tangu tangu huyu mama achukue uongozi wa nchi hii...!!

Hivi shida ni nini? Huyu mzee, Hayati John P. Magufuli (CCM) alifanya nini ambacho serikali chini ya Rais Samia Suluhu (ambaye naye ni WA chama kilekile yaani CCM) inashindwa kufanya?

Kuna nini katika sekta hizi; ya nishati ya umeme, mafuta ya jamii ya petrol na madini..? Je, ndiko dili za kifisadi za upigaji hela za wananchi (umma) za viongozi wa serikali hii ya CCM zilipo?

Je, hata wewe Rais Samia Suluhu tunayeambiwa kuwa u - mwislamu safi unahusika kwenye dili hizi za kifisadi Kwa gharama ya maisha ya watu wako unaowaongoza...? Kama huhusiki, kwanini umenyamaza kimya kana kwamba huluoni tatizo?

Inakuwaje kuwe na tatizo lilelile miaka yote, miezi yote na siku zote na wahusika (serikali) wakitoa majibu yaleyale bila ufumbuzi wowote?

Kiukweli, lazima tukubali leo kuwa, katika sekta hii ya NISHATI YA UMEME na PETROL na MADINI lipo tatizo kubwa linalohitaji ufumbuzi nje kabisa ya watu hawahawa chini ya CCM waliolitengeza tatizo hili. Kwa sababu tatizo hili haliwezi kuondolewa na watu wenye akili hiyo hiyo iliyosababisha ...!!!
Tanesco ni kibatari.
 
Kijana aliepewa dhamana amekabidhiwa sio kwamba ni mjuzi wa hio fani bali ni kwamba baba yake alikipigania chama kwahio wakaona nae wampe cheo kama fadhila kwa baba yake. 😀
 
Nenda kazikwe naye, bado Kuna nafasi kubwa pale, tafuta tu shuka jeupe, wakukuchimbia utawakuta huko
Mimi sina ushirika na wafu wala na kifo. Siwezi kufa kwa neno lako Hilo☝️☝️☝️ na badala yake kufa kukurudie wewe na uzao wako sawasawa na matamshi ya midomo yako!

Tunajadili hali ya upatikanaji wa umeme hapa nchini ukilinganisha wakati wake hayati Rais John P. Magufuli na sasa chini ya Rais Samia Suluhu..

Kuna shida gani sasa? Kwanini yeye aliweza ku - stabilize Hali ya upatikanaji wa nishati hii muhimu kwa uchumi wa nchi? Kwanini mara baada ya yeye hali ikabadilika na kurudi kwenye mgawo na kukatikakatika hovyo??

Ni hilo tu. Toa maoni na mtazamo wako. Mimi siwezi kufa na kwenda kuzikwa naye Kwa sababu sina ushirika na wafu wala kifo..!!
 
Nasema hivi, kachukue shuka jeupe, mbao, lakini wa kukuchimbia na kufukia utawakuta hukohuko
 
Kwa kweli hii awamu haikustahili kabisa kutuongoza.yote haya yametokana na katiba mbovu iliyotungwa na watu wabovu.watu hawafanyi kazi kwa weledi na hakuna hatua yeyote inayochukuliwa na wanaendelea kutujibu kwa dharau.
 
Wewe jamaa ningekuwa mods ningekupigaga pini mapema sana .unakauli za kijinga sana
Unampiga Pini mwanahisa? Ukiendeleza undezi ntachukua nyuki,niwaweke kwenye kiroba,niwatupie pilipili kichaa halafu niwaelekeze kwako
 
Back
Top Bottom