Tujaribu Mawaziri wahandisi umeme na watalaamu wa sekta ya umeme Wizara ya Nishati

Yoda

JF-Expert Member
Jul 22, 2018
37,620
46,264
Wizara ya nishati tangu naijua na kuisikia sijawahi kuona ikipewa waziri mtaalamu wa umeme, watu wa electrical engineering au power systems engineering.

Tofauti na Profesa Muhongo ambaye angalau alikuwa mwanasayansi wa miamba(na alijikita zaidi katika madini) sijawahi kuona kabla au baada yake wizara hii ikiongozwa na Waziri mwanasayansi achilia mbali mtaalamu wa masuala ya umeme.

Wizara wamekuwa wanapewa zaidi wanasheria na wengine waliosoma sanaa ambao sayansi ya umeme kwao huenda wanaona nyotanyota tu. Japo pia imekuwa inaongozwa na wanasheria kwa muda mrefu bado ni mojawapo ya wizara ambazo tumepigwa sana katika mikataba ya ajabu.

Sasa labda ni wakati wa kuwapa wataalamu manguli wenye sekta yao katika nafasi zote za waziri na naibu wake tuwajaribu nao, huenda kuna mambo wanaweza kuyaona kwa jicho la tatu ambao sio rahisi mtu maamuma wa umeme kuyafahamu.
 
Walishapeewa Professor Matthew Luhanga Toka chuo kikuu Cha Dar es salaam kama mkurugenzi Mkuu Tanesco na Waziri wa Nishati professor Mark Mwandosya

Wote wataalamu wa umene lakini Hali Ile Ile tu
 
Matthew Luhanga na Mwandosya walikuwa mawaziri wa nishati miaka ipi?
 
Ni kweli hii sekta inahitaji watu kama sisi , lakini shida IPO kwa Wana siasa ambaye amekuteua labda ingekuwa nafasi za kuomba ambazo hazina magumashi.
Lakini kwa mfumo wa nchi yetu ya upigaji wanasiasa watataka wafanye wanavyotaka wao,
Kidogo tu utasikia siongei na mbwa naongea na mfuga mbwa.
Hafu mfuga mbwa nakuona maagizo ambayo ni non technical
 
Matthew Luhanga na Mwandosya walikuwa mawaziri wa nishati miaka ipi?
Umeelewa nikichoandika Luhanga alikuwa mkurugenzi Mkuu wa Tanesco sio Waziri na mbobezu wa umeme Mwandosya alikuwa na uwaziri kipindi Cha Mwinyi akihusika na nishati
 
Wizara ya nishati tangu naijua na kuisikia sijawahi kuona ikipewa waziri mtaalamu wa umeme, watu wa electrical engineering au power systems engineering.

Tofauti na Profesa Muhongo ambaye angalau alikuwa mwanasayansi wa miamba(na alijikita zaidi katika madini) sijawahi kuona kabla au baada yake wizara hii ikiongozwa na Waziri mwanasayansi achilia mbali mtaalamu wa masuala ya umeme.

Wizara wamekuwa wanapewa zaidi wanasheria na wengine waliosoma sanaa ambao sayansi ya umeme kwao huenda wanaona nyotanyota tu. Japo pia imekuwa inaongozwa na wanasheria kwa muda mrefu bado ni mojawapo ya wizara ambazo tumepigwa sana katika mikataba ya ajabu.

Sasa labda ni wakati wa kuwapa wataalamu manguli wenye sekta yao katika nafasi zote za waziri na naibu wake tuwajaribu nao, huenda kuna mambo wanaweza kuyaona kwa jicho la tatu ambao sio rahisi mtu maamuma wa umeme kuyafahamu.
Prof Mark Mwandosya
 
Inahitaji mtu mwenye uwezo wa kuelewa mauzauza ya management ya TANESCO. Kama sio electrical engineer hao jamaa watakudanganya kama mtoto.
Uongo Dr Idris Rashid alikuwa mkurugenzi Mkuu Tanesco mchumi ndie alileta mifumo hii ya luku ya kutoenda kupanga foleni Tanesco
Tanesco ilikuwa na madeni balaa haitoi gawio serikalini kutwa inategenea ruzuku Dr Idris Rashid akabadilisha mainjinia ilikuwa hamna Kitu labda Raisi amteue Dr Idris Rashid mbunge na ampe uwaziri Sio huyo. Proffessior Muhongo wa geology sitaki fisadi huyo loo

Muhongo aisee arudi chuo kikuu tu kule Yuko vizuri serikalini na wizara hakumfai kibaka huyo mwizi mwizi mwizi
 
Umeelewa nikichoandika Luhanga alikuwa mkurugenzi Mkuu wa Tanesco sio Waziri na mbobezu wa umeme Mwandosya alikuwa na uwaziri kipindi Cha Mwinyi akihusika na nishati
Mwandosya alikua Waziri wa Maji...na Ewura by the Time ilikua chini ya wizara yake but kwenye vita ya urais Ewura ikachomolewa na kuperekwa wizara ya nishati na madini....I stand to be corrected.
 
Walishapeewa Professor Matthew Luhanga Toka chuo kikuu Cha Dar es salaam kama mkurugenzi Mkuu Tanesco na Waziri wa Nishati professor Mark Mwandosya

Wote wataalamu wa umene lakini Hali Ile Ile tu

Prof .Mark Mwandosya hajawai kuwa Waziri wa Nishati ila alikuwa katibu mkuu Wizara ya Nishati,Madini na Nishati.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom