Tukio la kutisha: Tuweni makini na mafuta ya kupikia. Kuna mtoto kaharibiwa sura

Melki the Storyteller

JF-Expert Member
May 3, 2022
5,701
9,779
Sambamba na hilo:
• Nimeambulia kipigo ndoige kutoka kwa mwananchi mwenye hasira kali kwa kuwa nimeshuhudia tukio

• Nimepoteza mpenzi papo hapo

Somewhere in Dar es salaam
Pembezoni mwa fremu moja ambayo hutumika kwa ajili ya wateja wa mama ntilie x kupata msosi, kuna mwanamama ambaye hukaanga vitafunwa. Mwanamama huyo yuko opposite na kijifrem changu cha biashara ya Ganga Njaa

Basi bhana, mwanamama huyo kamuacha mwanae mrembo sana, umri 16 yrs mwenye chuchu ndoige na rangi ya mlima Kilimanjaro, labda tumuite Sarah. Kwenye jiko lake alibandika karai lenye mafuta ya kupikia kisha kusikika akizungumza kuwa wacha aendee vitendea kazi nyumbani kwake, ambapo hapakuwa mbali na eneo la kazi

Ndani ya kama dakika 20 mbele, twalimsikia yule Sarah akipiga mikelele kuonesha kuwa mafuta yametaradadi jikoni, nilikuwa mtu wa kwanza kufika eneo la tukio na kumshauri Sarah aondoke mara moja, asogee mbali na eneo, Sarah aliishia kusema eti mama yake atamuadhibu. Nilikaripia kwa kadri niwezavyo, lakini sikuambulia nilichokirenga

Basi bhana, dakika chache zilizofuata, alijitokeza binti ambaye tayari nilikwisha mfungukia hisia zangu, ambaye kwa malengo nalipanga atakuwa msaidizi wa mke wangu kwenye suala zima la mizagamuo kwa kuwa mke wangu hataki tena kushiriki tendo zaidi ya kunipiga vipepsi kila nimgusapo

Baada ya binti kusogea pale, nalimuuliza kama kuna uwezekano wa kuipuka karai, muda ule binti anajongea mbele hatua moja, moto ukaripuka kutoka kikaangoni humo, kwa bahati mbaya ukamnasa Sarah. Uso wote umegeuka tumbua la mafuta, jumlisha ugonjwa wa macho uliokuwa ukimsumbua Sarah, hali imekua mbaya sana. Uzuri wake wote umepotea
__________________

Kipigo nilichoambulia ni kutoka kwa kijana mwenzangu, mtu wa Gym aliyepanda hewani, ambaye pia anamtaka yule binti wa ndoto zangu kimapenzi, japokuwa hakuna hata mmoja kati yetu aliyefanikisha jibu la kuridhisha. Jamaa kapandwa na hasira akidai kuwa kwanini nilimshauri huyo binti akaepue mafuta yale? Je kama angeliungua sura? Ningemuoa?

Japo tumezichapa, lakini kusema ukweli nimepasuliwa vikali hasa hasa maeneo ya mdomo. Mpaka sasa nahisi tayari nimeshamkosa huyo binti
---------------------

Tuachane na binti, turudi kwenye tukio la Mwanamama na mwanae, Sarah. Hilo ndo la msingi, mambo yangu mniachie mimi...
 
Mpee polee yakee mkuu huduma ya kwanza hapo n kumwagia maji baridi yakutoshaa Ili yapooze hayo maumivuu ,
 
Back
Top Bottom