Tujiunge na kuanzisha JAMII FARM

anzisha shamba lako sisi utakuwa mfano mzuri ... au unataka kuingiza watu chaka hapa?
 
Halafu iwe kama ile hadithi ya Animal Farm; ubabe wa moderators uendelee, ushabiki wa members pale pale, halafu na hizi ID za a.k.a. zibakie lakini members waruhusiwe kuvaa kininja ili wasijulikane.

View attachment 18388
attachment.php
i think you are right on this,ID zetu za kijamii forums itabidi tuanze upya au ??:)
 
Malila nakushukuru kwa mchango wako; inaonekana tayari nyinyi mmeshajiunga na kuanzisha hiyo estate. Naweza kupata details za hicho kikundi ili nami niweze kujiunga.

Ni kweli, tumeunganisha nguvu na tunataka kupanuka zaidi, tuna estate hapa Dsm/Pwani na mkoani. Lengo ni wote tuweze kushiriki ktk uchumi wa nchi yetu. Detail za kikundi chetu utapata bure, kwa sababu kujiunga ni bure kama jf na kutoka ni bure kama jf. Karibu sana, unaweza kuni-Pm ili kama uko Dar tunaweza kuonana na kuzungumza. Nitakuwa nje ya dar kuanzia january

Yote yanawezekana chini ya jua.
 
Kazi ya JF kuanzisha mijadala yenye lengo la kukuza na kuelimisha uelewa wa wana jf. Ukipata elimu hapa jf unaweza kwenda kulima wewe mwenyewe
 
kazi ya jf kuanzisha mijadala yenye lengo la kukuza na kuelimisha uelewa wa wana jf. Ukipata elimu hapa jf unaweza kwenda kulima wewe mwenyewe
wanaotaka umoja wajiunge! Jamani tuseme sasa kuonana ni rahisi sana!
 
wanaotaka umoja wajiunge! Jamani tuseme sasa kuonana ni rahisi sana!

Raha ya JF ni hizi a.k.a.
Ya Jamii Farm yatafanya tuwajue wanaomwaga sera za 'UJAMAA' hapa kisha kumbe huko mtaani wanashindana kujilimbikizia mali.
 
Raha ya JF ni hizi a.k.a.
Ya Jamii Farm yatafanya tuwajue wanaomwaga sera za 'UJAMAA' hapa kisha kumbe huko mtaani wanashindana kujilimbikizia mali.
mkuu huo ni woga tuu! kunawatu tunajua mpaka sasa kuwa ujamaa ndiyo ukombozi wetu!
 
Haya si ndiyo mambo ya Mashamba ya Ujamaa yaliyisababisha mpaka Mwamwindi akamtwanga Risasi Dk Kleruu
 
Asante ndugu Mgombezi,

Hilo ni Jambo Nyeti sana ambalo umeongelea ambalo litatoa ajira kwa vijana wa Kitanzania, WAKE kwa WAUME. Pia ndo njia pekee ya kupunguza mfumuko wa bei na kukuza uchumi wa kila Mtanzania.

Kila siku tunakula, na tunavaa. Tunakula Mpunga,Ngano, ugali, alizeti, ndizi, matunda na mengine useme..

Tunavaa Pamba,

Kondoo wa Hariri - Njombe

Bia - Shayiri west kilimanjaro, Mbulu, Nyanda za juu

Mafuta - Palm (Kigoma), Alizeti Singida

Mahindi yanaliwa na pia yanatengenezea cooking oil.

Kitimoto inaweza kuuzwa Ulaya

Sasa kwa nini watanzania tunakalia uchumi halafu tunakuwa masikini???

LIPO TATIZO

Tatizo ni utashi wa Kisiasa na Ulimbukeni.

Kila kitu hatuwezi, kila kitu mwekezaji.

Mfano kuna mashamba makubwa yaliyokuwa RANCH na NAFCO.

Hayo mashamba yamekuwa usingizi kwa muda mrefu na mengine wamegawana vigogo, mengine wamepewa wawekezaji (wakoloni).

Sasa hao wawekezaji wamewageuza watanzania watumwa ndani ya nchi yao. Imagine watu wanaajiriwa kama kibarua katika mashamba.

Ingekuwa vipi kama hao watanzania wangegaiwa kila mtu kuanzia heka 5 mpaka 10. Sidhani kama mtu anaweza kuhudumia heka 5 au basi sema heka 2 basi aidhuru.

Sasa kama mtanzania mmoja akigaiwa heka 5, akapewe hati miliki, anaweza kupata mkopo benki, akalima kwa tractor na pia akapata pembejeo. Kama hakuna mvua, kilimo cha umwagiliaji kifanye kazi. Hapo mavuno ni lazima, masoko ya mazao watafutiwe.

KASORO

Viongozi wengi wa Kisiasa ni wabinafsi, na 10% zinawanufaisha. Masilahi ya wananchi hayaangaliwi.

Wanawapa wawekezaji au wao wanajigawia mahekari kwa mamia wakati wananchi wanakosa angalao heka moja.

TUFANYEJE?

Haya mazungumzo tunayojadili hapa, tunayaandike kwenye magazeti na pia tuyawasilishe wizara ya kilimo, wizara ya ardhi, wizara ya uwezeshaji. na hata wanaharakati na taasisi kama kituo cha haki za Binadamu, haki elimu na vyama vya siasa.

Pia tuanze kujiandikisha, kiwilaya, kimkoa na kitaifa. umoja ni nguvu.

Asanteni, nawasilisha!!
 
Asante Sana Mpadmire.

Binafsi naamini sana katika UMOJA; nafahamu moja kati ya tatizo linalotukabili WAAFRIKA wengi ni ubinafsi. UFISADI ni matokeo ya Ubinafsi, kwani kila mmoja anaangalia maslahi yake binafsi.

Hivyo basi tuunganishe nguvu zetu na kutumilia raslimali zilizopo kwa ajili ya vizazi vyetu vijavyo. Tukishangaa tutakuta ardhi yote imechukuliwa na wawekezaji toka nje.

Naamini hapa JF kuna michango mingi sana, kwani nimeona Mpadmire amelekeza maeneo ambayo tunaweza kuanzisha mashamba.

Michango zaidi inahitajika katika kilimo husika pamoja, taratibu za kupata shamba, gharama za uendeshaji na mgawanyo wa hisa.
 
kwa wale walio serious!! tuanze .. tusikatishwe na wale ambao hawajawahi kufanya juhudi zozote za kwenda kukabiliana na changamoto za kilimo na ufugaji.. mimi nafahamu watu wengi ambao wamewekeza nguvu zao na rasilimali fedha katika kilimo. naamini watafanikiwa..
so kwa wale ambao wana dreams na vision zinazofanana tuungane!!
 
Asante Kanyagio kwa ushauri wako.

Kila jambo halikosi changamoto zake, lakini ni vyema kujaribu. Ninapendekeza mchakato huu kwenda live hapa jukwaani ili tuweze kupokea mawazo ya wengi katika kufanikisha hili. Hatua za awali ambazo tunaweza kuanza nazo ni pamoja na:
  1. Upatikanaji wa ardhi (shamba) - utaratibu utakaotumika na gharama zake.
  2. Mazao yatakayozalishwa kulingana na eneo husika - gharama za uzalishaji
  3. Maandalizi ya Shamba - Kulingana na ukumbwa na mazao husika
  4. Jinsi ya uchangiaji wa gharama kwa washiriki
  5. Mgawanyo wa Faida na Mwendelezo wa Shamba
 
thanks Mgombezi..
kikubwa kushinda chote katika step ya kwanza ni kupata the RIGHT people!! then ifuatiwe na hivyo vingine..
 
Wakubwa kuanzisha shamba la Jamii forum si kazi ndogo, kwanza kuna watu humu hata hawajawahi kushika jembe wala hawajui mazao yanafananaje na yanalimwa vipi - yaani ni waoga sana ku invest kwenye kilimo.

Kitu rahisi nachoona mimi ni kuanzishai Jamii SACCOS ambapo sisi wote tutakuwa wanachama, michango ikusanyewe walau ikifika 100m basi tunaanza investments

Tutachagua kamati nyingi tu kutokana na elimu na wanachama mfano
1. Kamati ya uwekezaji kwenye Ardhi na Kilimo - Mwenyekiti Mlila
2. Kamati ya Fedha na Uchumi ---
3. Kamati ya Uwekezaji kwenye soko la Hisa ---
4 Kamati ya uwekezaji kwenye Ujenzi wa Nyumba (Real estates)

Haya na mengine yataenda kwa awamu kutokana na mapendekezo ya kamati husika.

Hili linawezekana kabisa, mfano wanachama 200 kila mmoja akitoa 500,000/- basi tunapta Tshs 100,000,000 - Hapa tunaweza kuanza kazi ya kutengeneza Katiba yetu na mambo mengine yakafuata, Uaminifu na Uchapa kazi ndiyo nguzo kamili ya muungano wetu huu, - kuna watu wataajiriwa baadaye kutokana na mahitaji yatakayojitokeza.

Kinachotakiwa ni watu kujitolea - humu JF tuna Wanasheria, Wataalamu wa Kilimo na ufugaji, Wachumi, Ma engineer ambao wanaweza kusadia kuandika michanganuo kwenye fani zao.

Tukiamua hili jambo sasa hivi na kuanza hii SACCOS naamini after 5 years tutakuwa mbali sana kama si mfano Africa mashariki.

Wazo langu tu.
 
Asante Elnino

Nd

Wazo lako ni zuri sana; ndiyo maana ninaamini kupitia JF tunaweza kufanya makubwa kwa ajili ya Taifa letu na kutoa mwongozo kwa vizazi vijavyo.

Naamini huu utakuwa mwanzo mzuri; hapa JF tuna wataalamu wa vyama vya Ushirika nafikiri wanaweza kutusaidia hatua zipi tunaweza kuanzia. Tuchukue hatua.....!!!
 
Mgombezi,

Tatizo huwa ni mtaji, Man power ni kibao kwa vitu vyovyote ambavyo mtu anataka kufanya - tatizo linakuja uhamasishaji - haya mawazo yataishia hapa hapa JF believe me, Kuna baadhi ya watu wachache tu ambao wako serious, sasa inabidi wewe mtoa hoja uanze kuwatafuta ili kuwakutanisha na kuanza jambo hili live.

Kuna wana JF wengine hadi waone kitu kimeanza na kimefanikiwa ndipo watafumbuka macho, na kuna wengine wanaamini vitu kama DECI yaani pesa haraka haraka kitu ambacho kwa dunia ya leo hakipo.


Bila Mtaji kusema ukweli huwezi kufanya jambo lolote kwa dunia ya leo, lazima utakaa pembeni uangalie wenzako wanavyotegeneza pesa sababu wana mitaji.

Watanzania hatuna moyo wa umoja, leo hii mimi nitafurahi sana nikiona Mwana JF analia lia njaa wakati mimi nimeshiba, sijajua hii tabia ni ya kuzaliwa au ni asili ya sisi waafrika yaani kusaidiana ni zero.

Hata hapa JF kuna watu wanamiliki makampuni makubwa na wengine wanaishi kwa kima cha chini lakini kusaidiana kupitia forum hii ni zero, tutaishia kuandika then mwisho wa siku kila mtu anajijua mwenyewe.

Tubadilike, tuunganishe nguvu tufanye kitu kwa pamoja, leo hii wahindi, wachina, wakorea wamejaa nchini as if watanzania hatupo - sisi kazi zetu ni kufungua Bar, Kaanzisha shule ambazo hazina ubora na kufungua saloon ya kike na kiume, kununua bajaji, taxies, daladala - aaa Tuamke wa TZ together we can do more than this.
 
mfano mdogo tu jamaa kasema tuanzishe Gazeti la JF, hebu angalia michango ilivyo mingi? hakuna mtu anataka kilimo na ufugaji - ha ha ha
 
Back
Top Bottom