Nifanyeje ili kuikinga mifugo yangu dhidi ya mlipuko wa magonjwa?

Mwalimu Truth

Member
Feb 15, 2015
57
62
Habarini wana Jf.

Shamba langu la Mifugo lina Mbuzi, kondoo, kuku, kanga, bata, Mbwa wa kisasa, njiwa na ngombe wawili ambao wanafugwa wakiwa ndani muda wote.

Lengo langu ni kuwa na wanyama wa kufugwa aina zote kwenye shamba langu, ili kuepuka magonjwa, wanyama wote wanafugwa pasipo kuingiliana eneo yaani eneo nimeligawa katika sehemu kulingana na mifugo husika.

Lengo la uzi huu ni kwamba, bado nahofia mlipuko wa magonjwa shambani ambao unaweza kutokea na kusababisha vifo kutokana na aina mbalimbali za mifugo ninazofuga.

JE, NIFANYE NINI ILI KUBORESHA KUWAKINGA MIFUGO YANGU DHIDI YA MRIPUKO WA MAGONJWA?KINGA NI BORA KULIKO TIBA.
 
Watenge wanyama kulingana na Aina yao mfano ng'ombe ,mbuzi, kondoo , mbwa n.k hawa wote wanaweza pata ugonjwa wa kimeta yaani 'anthrax' usipo kuwa kuku hivyo watenge wanyama.
 
Maji safi
Chakula kisafi
Sehemu ya kulala safi
Mazingira ya Banda yawe safi
Ukizingatia ayo mengine yatafuata kama vile
Chanjo na Dawa
 
Kuwatenga tu tayari umeishazuia mlipuko wa magonjwa

Hapo kilichobaki zingatia lishe, maji, chanjo na matibabu mapema kwa watakaonyesha dalili za maradhi
 
Back
Top Bottom