Tujikumbushe vitabu vya zamani

Tujikumbushe vitabu vya zamani

hiki ndio kitabu bora Tanzania Hakijapata Kutokea Mpaka Leo ``HOFU`` kimeandikwa na A.E.MUSIBA muhusika mkuu katika kitabu hiki anaitwa WILLY GAMBA,kilichapishwa 1988 ni kizuri sana kwa wale wanaokijua na kama hauna naweza kukupa ukitoe copy ukakisome maana hakipatikaniki

Nilimuheshimu sana E. Musiba baada ya kusoma vitabu vyake takriban vyote lakini nilipoteza imani baada ya kugundua hakua anatunga bali alikua anatafsiri kazi JAMES HARDLEY CHASE na kubadilisha majina na maeneo na wahusika mfano, WILLY GAMBA badala ya MARK GILAND!!
 
Mambo ya ajabu yaliyompata Allan Quterman na wenzake,,kuiendea nchi ya watu weupe.Bonge la kitabu japo kwa kiwango fulani kinamdhalilisha mwafrika

Umenikumbusha "Umuslopaas" mkuu. Kitafute pia "Mashimo ya mfalme Suleiman" "Dunia rangirangile"
 
Ama zao ama zangu, nimempa achume, kusadikika,
 
hiki ndio kitabu bora Tanzania Hakijapata Kutokea Mpaka Leo ``HOFU`` kimeandikwa na A.E.MUSIBA muhusika mkuu katika kitabu hiki anaitwa WILLY GAMBA,kilichapishwa 1988 ni kizuri sana kwa wale wanaokijua na kama hauna naweza kukupa ukitoe copy ukakisome maana hakipatikaniki

Mkuu sijawahi kusoma hofu hila nimesoma njama kikomo
 
Nilikisoma zamani sana, naweza pata copy nikisome tena? Natanguliza shukrani Mkuu.
 
Kwakweli vilikuwa vizuri. Hakukuwapo haja ya television na social media.
Vilivuta hisia kiasi kwamba mtu hudhani ya kwamba tukio limetokea kweli.
Mtu ukiwa na kitabu kila akuitaye waona msumbufu akusumbua bureeee
vyangu nivikumbukavyo ni hivi
1. Mazungumzo ya alfu lela ulela
2. Kisiwa chenye hadhina
3. maajabu ya mlima kolelo
4. Jamaaa hodari kisiwani
5. Hekaya za Abunuwasi
5. Safari za juma MA Sungura
6. Tunguli ya Ajabu
7. Bulicheka
8. Mahugri mtoto aliye lelewa na nyani
9. Simba wa Tsavo
10.???
Njoooni hapa tukumbushane uzuri huuu ambao kizazi hiki kimeukosa
Karibuni

Rose Mistika
 
Rosa mistika, kifo kisimani, mfalme edipodi,uhuru wa watumwa, nagona , mzingile, hofu, njama,wasifu wa siti bint saad, maisha yangu na baada ya miaka hamsini...
Miongoni mwa vitabu bora sana hivi
 
Naomba kama unacho cha HOFU cha jembe willy gamba naomba ndg nicheki kwa 0712905393 hii namba plz

Mkuu kweli una hamu na hicho kitabu mpaka umeanika namba yako ya simu JF jamaa asipokupa atakuwa hajakutendea haki namsihi kwa jina la Yesu akuonee huruma na akidhi haja ya moyo wako. NAAMINI ATAKUPA
 
Mkuu sijawahi kusoma hofu hila nimesoma njama kikomo

Elistabulus Elvis Musiba ameandika; Njama, kikosi cha kisasi, Kikomo, Hofu n.k ni vitabu ukisoma utataka kurudia hata mara mia!
 
Elistabulus Elvis Musiba ameandika; Njama, kikosi cha kisasi, Kikomo, Hofu n.k ni vitabu ukisoma utataka kurudia hata mara mia!

Nilisoma Njama mwaka 1986 nilikuwa naona km movie hv, najitisha, naogopa, nazima taa nalala jamani
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom