Simu ya kifo mtunzi nimemsahau jina
katalambula
Simu ya kifo mtunzi nimemsahau jina
Ushauri wa bureeee, tafuta hivyo vitabu kama mtu anaweza fanya kazi hiyo, kisha toa copy chache kwa majaribio, tafuta kijana apite mtaa kwa mtaa atakutana na sisi wa zee wa zamani, na kisha piga pesa unaweza Shangaa
kwakweli vilikuwa vizuri. Hakukuwapo haja ya television na social media.
Vilivuta hisia kiasi kwamba mtu hudhani ya kwamba tukio limetokea kweli.
Mtu ukiwa na kitabu kila akuitaye waona msumbufu akusumbua bureeee
vyangu nivikumbukavyo ni hivi
1. Mazungumzo ya alfu lela ulela
2. Kisiwa chenye hadhina
3. Maajabu ya mlima kolelo
4. Jamaaa hodari kisiwani
5. Hekaya za abunuwasi
5. Safari za juma ma sungura
6. Tunguli ya ajabu
7. Bulicheka
8. Mahugri mtoto aliye lelewa na nyani
9. Simba wa tsavo
10.???
Njoooni hapa tukumbushane uzuri huuu ambao kizazi hiki kimeukosa
karibuni
mzimu wa watu wa kale, roza mistika na kusadikika cha shaaban robert mnavikumbuka?
haha WEZI wa mifugo ilikua dodoma hiyo walivamiwa na kupigwa mishale ma mikuki
Uko vizuri Chief... Waziikumbuka fikiri na Uledi, Mzee marebeto na mapambano dhidi ya Malaria, Mpapai na mitete?
kweli BRN imetushushia hadhi ya elimu yetu
mkuu, elimu ilikua zamani sasa hivi naona kila mtu mwandishi wa vitabu ubunifu kwisha kabisa!.
Kweli mkuu. Hapo Karl Marx angetwambia ni 'ubidhaishaji wa elimu' au 'commodification of Education' kwa lugha ya Malkia. Kwa sasa uandishi ni kibidhaa zaidi na si kutoa huduma
daah...akina Gadi bula, mama mlole, Dania, Bi Hanuna....ninacho kopi yake...
Mkuu nipo Mwanza nina shida sana na kitabu hiki, nisaidie nakipataje?