Tujikumbushe vitabu vya zamani

Tujikumbushe vitabu vya zamani

Kuna hii hadithi;
USIKU WA BALAA
Nilikua kadogo hata la kwanza sijaanza ila najua kusoma, basi kitabu hiki kilikua moja ya kipenzi.
Tatizo nilikua nakisoma jioni baada ya kutoka madrasa, baada ya hapo giza likiingia ni kujitisha tu hasa ile picha ya mtu aliyekatwa kichwa.

Vitabu ni hazina kubwa sana.
Nimejaaliwa kusoma 95% ya vitabu vilivyotajwa humu.
Hivi sasa naendelea kuvikusanya hivi na nimevipata vya kutosha tu.
Vya musiba ndio tabu kuvpata.
 
Ushauri wa bureeee, tafuta hivyo vitabu kama mtu anaweza fanya kazi hiyo, kisha toa copy chache kwa majaribio, tafuta kijana apite mtaa kwa mtaa atakutana na sisi wa zee wa zamani, na kisha piga pesa unaweza Shangaa
 
Simulizi za Agoro Anduru,Dibwela nk hizo ni za magazeti ,Enzi hizo gazeti la ukweli lilikuwa MFANYAKAZI
 
Kwakweli vilikuwa vizuri. Hakukuwapo haja ya television na social media.
Vilivuta hisia kiasi kwamba mtu hudhani ya kwamba tukio limetokea kweli.
Mtu ukiwa na kitabu kila akuitaye waona msumbufu akusumbua bureeee
vyangu nivikumbukavyo ni hivi
1. Mazungumzo ya alfu lela ulela
2. Kisiwa chenye hadhina
3. maajabu ya mlima kolelo
4. Jamaaa hodari kisiwani
5. Hekaya za Abunuwasi
5. Safari za juma MA Sungura
6. Tunguli ya Ajabu
7. Bulicheka
8. Mahugri mtoto aliye lelewa na nyani
9. Simba wa Tsavo
10.???
Njoooni hapa tukumbushane uzuri huuu ambao kizazi hiki kimeukosa
Karibuni
Namba 5 nakitafuta sana. Mwenye kujua nitakakokipata anielekeze
 
Simulizi za Agoro Anduru,Dibwela nk hizo ni za magazeti ,Enzi hizo gazeti la ukweli lilikuwa MFANYAKAZI

Kwa kweli maelezo yenu yanasikitisha sana, mnanikumbusha enzi za zamani, mmenipelka mbali sana jamani.

pia kuna zile. Stori za Pimbi na MADENGE . Noma sana.

kitabu cha "ARABIAN NIGHT' ulikuwa ukisoma vinakupeleka mbali sana.

jamini " KUSADIKIKA " CHA SHK SHAABAN ROBERT. hiki kitabu ni hazina kwa sasa.
 
Jamani tusisahau na magazeti ya wakati ule maana kulikuwa hakuna TV wala radio nyingi kama sasa wakati ule ilikuwa RTD na idhaa zake mbili yaani idhaa ya taifa na biashara ambazo ikifika saa 6 zinafungwa. Sasa magazeti ya wakati ule
1. mfanyakazi
2. sani (sio kama hili la sasa linalochapishwa kama gazeti la kila siku)
3. Busara
4. Misakato
5. Tabasamu
6. Radi
7.....
 
Kibanga ampiga mkolon
Ha ha ha mkuu acha fujo bhana,hiyo ni moja ya sura/topic katika kitabu cha darasa la nne,zingine ni Lindu amwokoa Kapilima,siku ya gulio katerelo,na nyinginezo daaah kitambo...
 
Jamani tusisahau na magazeti ya wakati ule maana kulikuwa hakuna TV wala radio nyingi kama sasa wakati ule ilikuwa RTD na idhaa zake mbili yaani idhaa ya taifa na biashara ambazo ikifika saa 6 zinafungwa. Sasa magazeti ya wakati ule
1. mfanyakazi
2. sani (sio kama hili la sasa linalochapishwa kama gazeti la kila siku)
3. Busara
4. Misakato
5. Tabasamu
6. Radi
7.....
Mfanyaazi kila jumamosi ukurasa wa burudani Kuna Hemedi Kimwanga,michezo Kuna James Nhende Yanga wa kutupwa kutupwa...Sani hapo sasa Lodi lofa,Sukunnu,Madenge na babake,Zena na Betina...funga kazi ilikuwa booonge la mechi Bush stars VS Born Town ....kitambo.
 
Wakati ule ilikuwa hamna namna lazima usome UHURU na MZALENDO. Mimi kwenye mzalendo nilikuwa navutiwa na katuni za CHAKUBANGA na kwenye uhuru ni matangazo ya sinema ODEON, EMPIRE, wakati ule za akina AMITA BACHANI na kina CHAKRABOTI na dansi ... dansi dansi dansi. UHAMIAJI JAZZ, MLIMANI PARK, DAR INTERNATIONAL OSS, MAQUIZ, BIASHARA JAZZ, PANASONIC JAZZ, BUGURUNI SOUND, URAFIKI JAZZ, POLISI JAZZ, MWENGE PASELEPA, TOMA TOMA, WASHIRIKA TANZANIA STARS, VIJANA JAZZ, JUWATA JAZZ, ..... Sasa hivi michosho tu ya mabongo flava wanaimba lakini hawana wapigaji wanaweka CD halafu wanaanza kuimba wakati ule vijana wanaoimba sasa ilikuwa marufuku ni watu wazima tu wao wawe shuleni. Sheria ziklikuwa kali hakuna under 18 kuonekana sehemu za starehe. Sasa hivi vitoto vidogo utakuta viko baa au kilabuni. Disco kila kona na wakati ule hakuna UKIMWI watu watu wanajirusha kwa kwenda mbele wanategemea rangi 2 kutibu mafua. Ilikuwa raha tupu!
 
Jamani mi natafuta kitabu kiitwacho USHINDI WA MAHABA. Nipo tayari kutoa hata Sh.50,000 kwa mtu atakayenipa hicho kitabu. Ni cha zamani sana, miakaya 80 hivi, nakumbuka nilisomanikiwa form 1.
 
Ah mkuu! baba! makumazahn! mzee mwindaji! akeshae! hodari mwepesi! ambae risasi zake hazikosi shabaha! muuwaji wa simba mla tembo! rafiki muaninifu!ile methali ya kikwetu isemayo milima haikutani ni ya kweli kabisa na tena yenye busara. tazama alikuja tarishi kutoka natal akalia na kusema makumazahn amefariki! na nchi haitamuona tena! lakini tazama leo baba yangu katika nchi ngeni tena yenye harufu mbaya kama hii namuona tena makumazahn! hakika ndie yeye bila shaka! manyoya ya mzee mbweha yamekwisha ingia mvi lakini meno na macho yake bado ni makali vilevile kama zamani! mkuu baba unakumbuka namna ulivyopitisha risasi kwenye jicho la nyati aliekuwa anashambulia?

Kitambo!! unanikumbusha swaiba wetu akishakula shada, anaanza kutililika mistari ya hicho kitabu hadi raha. inkosikazi kama sijakosea maana kitambo mzee. dah!
 
Ila naona style ya uandishi ya Musiba (mwandshi wa Njama na hofu), unafanana na ule wa James Hadley Chase. Kwa mtazamo wangu mwandishi bora kabisa kwa Tanzania alikuwa Ben Mtobwa. Style ya uandish wake ni kama Mario Puzzo au Sydney Sheldon.
 
Uko sahihi kiongozi jamaa anataka kutudanganya! Ni yule Mzee aliyewekewa sumu kwenye sigara na yule binti!!

Jamaa gani,,??nilivisoma siku nyingi mkuu hata kumbukumbu zinapotea
 
Hivi Zawadi ya Ushindi kwa Sikamona ilikuwa ninini?
 
Wakati ule ilikuwa hamna namna lazima usome UHURU na MZALENDO. Mimi kwenye mzalendo nilikuwa navutiwa na katuni za CHAKUBANGA na kwenye uhuru ni matangazo ya sinema ODEON, EMPIRE, wakati ule za akina AMITA BACHANI na kina CHAKRABOTI na dansi ... dansi dansi dansi. UHAMIAJI JAZZ, MLIMANI PARK, DAR INTERNATIONAL OSS, MAQUIZ, BIASHARA JAZZ, PANASONIC JAZZ, BUGURUNI SOUND, URAFIKI JAZZ, POLISI JAZZ, MWENGE PASELEPA, TOMA TOMA, WASHIRIKA TANZANIA STARS, VIJANA JAZZ, JUWATA JAZZ, ..... Sasa hivi michosho tu ya mabongo flava wanaimba lakini hawana wapigaji wanaweka CD halafu wanaanza kuimba wakati ule vijana wanaoimba sasa ilikuwa marufuku ni watu wazima tu wao wawe shuleni. Sheria ziklikuwa kali hakuna under 18 kuonekana sehemu za starehe. Sasa hivi vitoto vidogo utakuta viko baa au kilabuni. Disco kila kona na wakati ule hakuna UKIMWI watu watu wanajirusha kwa kwenda mbele wanategemea rangi 2 kutibu mafua. Ilikuwa raha tupu!
Mkuu home ni mission quarter kariakoo,jumapili Sikinde wakiwa DDC,nilikuwa nasiliza domo la Bata la King Maiko Enock na gitaa la Abel Batazar nikiwa barazani burudaaani..
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom