Tujifunze kidogo kuhusu ndege (airplane)

Tujifunze kidogo kuhusu ndege (airplane)

Asante sana Shebbydo....shule kubwa unaitoa kwa lugha rahisi sana mtu kuelewa....ingekuwa ni tuition ungekusanya pesa nyingi sana kwani madarasa ya physics huwa haya masomo kwa asilimia kubwa yanafundishwa bora liende wanafunzi wanameza ili wafaulu mitihani. Asante sana kutoa shule kubwa bure....
 
Leo nitaongelea Flight Data Recorder (FDR) Al-maarufu BLACK BOX kwa sababu nimeona watu wengi wanakisikia sikia habari zake lakini hawakijui kwa undani

Mkuu asante kwa shule, shule mujarab kabisa shukran sana.

Mimi nina maswali kadhaa pia mkuu; 1. Nini maana Air speed na True Air speed? 2.Ni namna ipi hufanya ndege kusoma speed yake ikiwa angani? Mfano Gari hutumia Speed meter, vp kuhusu ndege? Na ili speed iweze kusomwa kifaa chake hufanyaje kazi?
Huwa kinakuwa ndani ya ndege au nje?

Na kifaa kipi husoma umbali kutoka ardhini? Mfano mpo futi elfu 40 kutoka usawa wa bahari, kipi hufanya ndege kuelewa ipo umbali ule kutoka chini?
Shukrani.
 
Habari Wanajukwaa

Ni matumaini yangu kuwa mu wazima bukheri.

Kuna tangazo moja la redio la malaria huwa linanivutia sana, mtoto anamuuliza baba yake kuhusu ndege inavyoweza kupaa angani. Mzee kutokuwa na elimu hata kidogo tu ya aviation anajitetea kwa kumwambia mwanaye hayo ni maarifa ya juu sana.

Ndege nini! Ndege ni chombo ambacho kinasafiri angani kwa kutumia kani mnyanyuo (Lift force) inayozalishwa hasa kwenye mabawa kutokana na uhusiano wa mwendo kati ya hewa na ndege yenyewe.

Ndege ina sehemu kuu tano, yaani; Injini (Power plant), bodi la ndege (fuselage), mabawa (wings), Mkia (Empennage) na Mfumo wa matairi (Landing gear).

1: POWER PLANT; hii ni sehemu ya ndege inayohusika na uzalishaji wa kani msukumo (Thrust force). Hii ndiyo kani (force) inayoisogeza ndege kutoka point A kwenda point B ikiwa angani.

2:FUSELAGE; Hii ni sehemu ya ndege ambapo sehemu zingine zimeunganishwa kwayo. Pia nyiyo sehemu ambapo abiria, wafanyakazi wa ndege na mizigo hukaa.

3:MABAWA; Hii ni sehemu ya ndege yenye umbo la "aerofoil" ambayo inahusika na kuzalisha kani mnyanyuo (LIFT FORCE). Hii ndiyo kani inayoifanya ndege ielee angani.
Aerofoil ni umbo ambalo huzalisha kani-mnyanyuo kutoka na tofauti ya mgandamizo wa hewa wa chini na juu ya umbo hili. Hii ni kutokana na utofauti wa ukubwa wa eneo la chini na juu. Eneo la juu huwa kubwa zaidi ya lile la chini, hivyo kusababisha hewa ya juu kusafiri kwa kasi zaidi ya ile inayopita chini ili kuweza kukutana pamoja katika muda ule ule (LAW OF CONTINUITY). Kasi ya hewa ikiongezeka basi mgandamizo wake hupungua (PRESSURE)

Hiki ndicho kinachotokea kwenye mabawa ya ndege. Mgandamizo wa hewa chini unakuwa mkubwa kuliko juu, hivyo kani-mnyanyuo kuzalishwa. Ikumbukwe kwambo umbo zima la ndege lipo katika aerofoil. Hivyo nalo huchangia kani-mnyanyuo japo kwa kiasi kidogo ikilinganishwa na ile inayozalishwa kwenye mabawa.

4:EMPENNAGE; Hii ni sehemu ya ndege kwayo kunapatikana maumbo yanayoipa ndege "U-stable" katika mihimili yake na vifaa vinavyoifanya ndege iweze kutembea (move) katika mihimili yake. (Tutaangalia huko mbele mihimili ya ndege ni nini). Katika sehemu ndipo kuna "horizontal na vertical stabilizers".

5:LANDIND GEAR; Huu ni mfumo mzima wa matairi ambao unaohusika na kuisaidia ndege kutembea juu ya njia ya kurukia (RUNWAY) wakati wa kuruka na kutua, vilevile wakati wa kwenda sehemu ya matengenezo (HANGAR)

Kwa leo tuishie hapo, sehemu itakayofuata tutaangalia kan (FORCES)i zilizopo kwenye ndege na mihimili ya ndege (MOTION ALONG AIRCRAFT AXES). Mwenye swali lolote kuhusu ndege unakaribishwa.
Mkuu hebu nieleweshe namna engine ya ndege inavyochoma mafuta ktk high altitude ambako hakuna oxygen ya kutosha.au moto sio kwamba lazima oxygen iwepo ndio uwake! Naomba kuunga mkono hii thread uliuoianzisha mkuu
 
hivi uzito wa juu kabisa kubebwa na ndege ni uzito gani? Na kwanini wakati wa kuruka au kutua cabin crew wanaomba madirisha yafunguliwe ndani ya ndege na viti viwe upright?je speed ya ndege angani ni constant au pilot anaweza kuamua kwenda slow au speed?
Shebbydo please tusaidie majibu.
 
Sidhani kama kuna nchi ambayo imezuia kabisa anga lake lisipitwe na ndege ya Kiraia. Kwa mfano hiyo China unayosema, jiulize ndege zinazokwenda huko zinapita wapi. Sasa hivi nchi karibia zote zinategemeana japo kuna maeneo ambayo unaweza kuelekezwa usipite la route zipo za kupita ndege za kiraia. Utaratibu wa anga kwa ndege za kiraia upo chini ya International Civil Aviation Organization kukiwa na sheria na kanuni maalum.
Umenikumbusha ICAO
 
Ndiyo kifaa hiki kipo kwenye ndege miongoni mwa vifaa vya avionics. Kifaa hiki kazi yake ni kurekodi taarifa za ndege tangu inapoanza safari. Kifaa hiki kipo protected na material ni ngumu kushika moto.
Ndo hicho kinachoitwa black box??!!
 
Ndege inapokaribia kutua kuna hali flani inatokea, sijui ni kitu gani husababisha hiyo hali. Hali hiyo hufanya masikio yazibe na kunakuwa na kelele flani kama mruzi mkali sana, na hiyo hali abiria hutangaziwa na wahudumu kuwa rubani amefungua kitu flani ili ndege iweze kutua. Mkuu hii ni kitu gani, na je inatokea kwa ndege zote zinapokaribia kutua au baadhi.
Mkuu kuna vifaa vipo kwenye mabawa ambavyo husaidia kuzalisha kani-mnyanyuo (LIFT FORCE) kwa kiasi kikubwa, vinaitwa Flaps na Slats. Wakati wa kutua huwa rubani anavirudisha normal, hivyo wakati vinarudi huwa vinapiga kelele kama miruzi.
 
Back
Top Bottom