Asante mkuuAhsante sana ndugu Shebbydo kwa kutupatia/kutuongezea ufahamu ya usafiri wa anga ambao tunautumia mara kadhaa bila hata kuwa na ABC yake.
Labda ningekuomba utujuze juu ya mifumo/classifications za ndege maana tunasikia majina kama JET Engines na kuna hizi zenye mapangaboi mengine yako kwenye pua ya ndege na mengine yameshikizwa kwenye mabawa nk. Natanguliza shukrani
mkuu huyu jamaa alikuwa ni wa tunduma na ile ndege yake bado imepaki tu kando ya barabara ya mbeya tundumaHapana mkuu haijawahi kutokea. Kuunda ndege hasa helicopter iweze kupaa ni gumzo. Zaidi tutaishia kutengeneza midoli. Kama stori ya yule jamaa sikumbuki alikuwa wa wapi waliyedai katengeneza helikopta kwa kutumia vifaa vya gari, mimi nilibaki kucheka. Jambo kama hulijui ni sawa na usiku wa giza. Sifa ya kwanza ya vifaa vinavyounda ndege ni imara lakini vyepesi. Suala la injini ya gari kurusha helikopta ni ndoto za mchana kwa sababu hata kama utaunga unga shaft zako pamoja na mapangaboyi yako, haiwezi kuwa na power ya kutosha. Ndege kila kifaa kilichopo kipo kwa hesabu maalum. TCAA walivyopiga marufuku watu wakalalamika eti tunaua vipaji, mimi niliona ni kwa sababu watu hawaelewi tu. Laiti wangeelewa hata kidogo kuhusu airworthness wangeandamana kwenda kumzuia yule jamaa asilete majanga ya majariribio ya kitu asichokuwa na ufahamu nacho.
Asante kwa maswali yako nduguIvi angani kuna njia ambapo ndege inapita???
-pilot anatumia kifaa gani kujua amefika sehemu gani?
-ni mambo gani yanayoweza kupelekea ndege kupotea angani
-ndege ikiishiwa mafuta ipo angani ni utaratibu gani unafuata kusaidia abiria
Naomba unisaidie majibu mkuu
Hili swali lako ni la physics concept kwa kuwa katika uhalisia huwezi kuruhusiwa kufungua sehemu yoyote ya ndege urushe kitu nje ukiwa angani. Ila kasome theory of relativity.Kwanini ukiwa ndani ya ndege ukarusha kitu juu wima mfano pen au kitu kidogo kinarudi hapo hapo wakati chombo kipo kwenye mwendo mkali kwanini kisiishie kutua nyuma zaidi kutokana na mwendo mkali uliopo?
Samahani mkuu kama nitakuwa nimetoka nnje ya mada kidogo ni kuwa kutokana na maelezo yako naona kama umesomea either "AERONAUTIC ENGINEERING and maintanance " au " URUBANI " kwa ujumla nilikuwa nataka kujua KAMA HAPA BONGO WANATOA B.ENG ya AERONATIC AND MAINTANANCE AU HATA AERONATIC AND AVIATION " ni hivyo tu mkuu kuuliza si ujingaHabari Wanajukwaa
Ni matumaini yangu kuwa mu wazima bukheri.
Kuna tangazo moja la redio la malaria huwa linanivutia sana, mtoto anamuuliza baba yake kuhusu ndege inavyoweza kupaa angani. Mzee kutokuwa na elimu hata kidogo tu ya aviation anajitetea kwa kumwambia mwanaye hayo ni maarifa ya juu sana.
Ndege nini! Ndege ni chombo ambacho kinasafiri angani kwa kutumia kani mnyanyuo (Lift force) inayozalishwa hasa kwenye mabawa kutokana na uhusiano wa mwendo kati ya hewa na ndege yenyewe.
Ndege ina sehemu kuu tano, yaani; Injini (Power plant), bodi la ndege (fuselage), mabawa (wings), Mkia (Empennage) na Mfumo wa matairi (Landing gear).
1: POWER PLANT; hii ni sehemu ya ndege inayohusika na uzalishaji wa kani msukumo (Thrust force). Hii ndiyo kani (force) inayoisogeza ndege kutoka point A kwenda point B ikiwa angani.
2:FUSELAGE; Hii ni sehemu ya ndege ambapo sehemu zingine zimeunganishwa kwayo. Pia nyiyo sehemu ambapo abiria, wafanyakazi wa ndege na mizigo hukaa.
3:MABAWA; Hii ni sehemu ya ndege yenye umbo la "aerofoil" ambayo inahusika na kuzalisha kani mnyanyuo (LIFT FORCE). Hii ndiyo kani inayoifanya ndege ielee angani.
Aerofoil ni umbo ambalo huzalisha kani-mnyanyuo kutoka na tofauti ya mgandamizo wa hewa wa chini na juu ya umbo hili. Hii ni kutokana na utofauti wa ukubwa wa eneo la chini na juu. Eneo la juu huwa kubwa zaidi ya lile la chini, hivyo kusababisha hewa ya juu kusafiri kwa kasi zaidi ya ile inayopita chini ili kuweza kukutana pamoja katika muda ule ule (LAW OF CONTINUITY). Kasi ya hewa ikiongezeka basi mgandamizo wake hupungua (PRESSURE)
Hiki ndicho kinachotokea kwenye mabawa ya ndege. Mgandamizo wa hewa chini unakuwa mkubwa kuliko juu, hivyo kani-mnyanyuo kuzalishwa. Ikumbukwe kwambo umbo zima la ndege lipo katika aerofoil. Hivyo nalo huchangia kani-mnyanyuo japo kwa kiasi kidogo ikilinganishwa na ile inayozalishwa kwenye mabawa.
4:EMPENNAGE; Hii ni sehemu ya ndege kwayo kunapatikana maumbo yanayoipa ndege "U-stable" katika mihimili yake na vifaa vinavyoifanya ndege iweze kutembea (move) katika mihimili yake. (Tutaangalia huko mbele mihimili ya ndege ni nini). Katika sehemu ndipo kuna "horizontal na vertical stabilizers".
5:LANDIND GEAR; Huu ni mfumo mzima wa matairi ambao unaohusika na kuisaidia ndege kutembea juu ya njia ya kurukia (RUNWAY) wakati wa kuruka na kutua, vilevile wakati wa kwenda sehemu ya matengenezo (HANGAR)
Kwa leo tuishie hapo, sehemu itakayofuata tutaangalia kan (FORCES)i zilizopo kwenye ndege na mihimili ya ndege (MOTION ALONG AIRCRAFT AXES). Mwenye swali lolote kuhusu ndege unakaribishwa.
Asante mkuuhongera mkuu kwa uzi murua.... hii ni elimu tosha kwakweli
maswali
1. je tunaambiwa kwamba kuna ndege zenye uwezo wa kukaa hewani mpaka 24plus hrs, kwa nn safari kama ya dubai ama germany unalazimika kupanda ndege zaidi ya moja... ukizingatia mashirika makubwa kama fly emirates wanaingia hapa kwetu.
2. inaaminika ndege ndio usafiri ulio safe kuliko usafiri wowote ule (japo mm naamini ni treni), kwa nn pamoja na sifa hyo ndege ndio usafiri ambao mkipata ajali kuna risk kubwa sana ya watu wote kupoteza uhai ? maelezo kdg naomba
maswali mengine nadhani yameshaulizwa, mwisho tupe walau brief.. ww ni ruban au ulishawahi kusomea haya mambo ? au huwa unajifunza tu mitandaoni. thanks
hongera mkuu kwa uzi murua.... hii ni elimu tosha kwakweli
maswali
1. je tunaambiwa kwamba kuna ndege zenye uwezo wa kukaa hewani mpaka 24plus hrs, kwa nn safari kama ya dubai ama germany unalazimika kupanda ndege zaidi ya moja... ukizingatia mashirika makubwa kama fly emirates wanaingia hapa kwetu.
2. inaaminika ndege ndio usafiri ulio safe kuliko usafiri wowote ule (japo mm naamini ni treni), kwa nn pamoja na sifa hyo ndege ndio usafiri ambao mkipata ajali kuna risk kubwa sana ya watu wote kupoteza uhai ? maelezo kdg naomba
maswali mengine nadhani yameshaulizwa, mwisho tupe walau brief.. ww ni ruban au ulishawahi kusomea haya mambo ? au huwa unajifunza tu mitandaoni. thanks
Hapa Bongo kuna Bachelor of Aircraft Maintenance Engineering hapo NIT ila bado wanachangamoto ya mazingira ya kujifunzia na walimu pia. Lakini unaweza kwenda hapo ukapambana wewe mwenyewe.Samahani mkuu kama nitakuwa nimetoka nnje ya mada kidogo ni kuwa kutokana na maelezo yako naona kama umesomea either "AERONAUTIC ENGINEERING and maintanance " au " URUBANI " kwa ujumla nilikuwa nataka kujua KAMA HAPA BONGO WANATOA B.ENG ya AERONATIC AND MAINTANANCE AU HATA AERONATIC AND AVIATION " ni hivyo tu mkuu kuuliza si ujinga
Mkuu kumbe ile kusikia ndege kama imejiachia inakaribia kudondoka au kusikia inapanda kwa kasi uwa ni kukwepa mawinguuAsante mkuu kwa ushauri na mimi napenda sana kutumia lugha rahisi ila wakati mwingine nashindwa kutokana na uhaba wa misamiati ya Kiswahili katika lugha ya ndege.
Swali lako kuhusu ndege kujiongoza yenyewe ni kweli kwa sababu zina mfumo wa Auto flight au unaweza kuita Auto pilot. Lakini swala la kusema kuicha ndege ukafanye shughuli zingine ni ngumu. Kwa sababu lolote likitokea lazima wewe ndiyo unawajibika si hiyo autopilot. Auto pilot unaitumia kwenye cruising altitude yaani baada ya kufika katika level ambayo hupandi wala hushuki upo katika the same altitude kwa muda mrefu. Yenyewe auto pilot unapoicommand inachojua ni altitude peke yake. Ndege ikitaka kuhama altitude kutokana na hali ya hewa autopilot inairudisha katika altitude ambayo imeambiwa. Lakini haiwezi kujua hapa kuna wingu ambalo siwezi kulipita ni kwepe. Autopilot inakupumzisha kung'ang'ana na "CONTROL STICK" tunaweza kuita usukani japo siyo hasa.
Anhaaaa sawa shukran mkuuHapa Bongo kuna Bachelor of Aircraft Maintenance Engineering hapo NIT ila bado wanachangamoto ya mazingira ya kujifunzia na walimu pia. Lakini unaweza kwenda hapo ukapambana wewe mwenyewe.
hata mimi nipenda swali lako,ngoja arudi tupate majibuMkuu nasikia kuna baadhi ya nchi huwezi kuingia kwenye anga zao,hizo njia za ndege mnazitengenezaje vip na kwa vigezo vipii..... vile vile nasikia baadhi ya nchi kama china huwezi kupita kwenye anga lao ovyo ukiwa hewani nyie mnachukua utaratibu gani??? au kila nchi mnatoa taarifa???