Tujiandae na 'lock down' nyingine kubwa

Tujiandae na 'lock down' nyingine kubwa

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
359,887
Reaction score
828,469
Madhila ya vita ya Iran na Marekani/Israel yameanza kuonekana tangu mwanzo mwa mwezi huu kwenye usafiri wa ndege

Baada ya airport za Qatar na Dubai kufungwa tickets za ndege zilipanda maradufu.. Imagine ticket ya ndege kutoka China kurudi Bongo ilipanda kutoka 2M mpaka 10M

Hii vita haina dalili na kumalizika leo wala kesho na ukosefu wa mafuta umeshaanza kushika kasi duniani .. Leo pipa moja la mafuta ghafi limefikia dola 175.

Mataifa mengi yameshaanza kutoa tahadhari kwa wananchi wake kupunguza matumizi ya nishati (mafuta na gesi) sisi bado.. Lakini hatuko mbali

Lockdown ijayo si ya maradhi na barakoa na kujivukiza tena! Bali ni lockdown ya " movement limitations" kwakuwa mafuta yatapanda bei kupitiliza na yatakuwa hayapatikani kwa urahisi

Fursa fursana! Lockdown ya mafuta wakati itakapokuwa janga kwa wengine, kwingineko itakuwa ni neema na fursa ya kupiga ndefu.

Jiandae ufaidike ama ujipange lockdown yaja!
 
uzuri tanzania tumesha funga mkanda kitambo
Subiri mtasogeza matundu ya mikanda

Kufungwa kwa Mlango-Bahari wa Hormuz: Njia hii muhimu ya bahari, inayopitisha takriban 20% ya mafuta yote duniani, imekumbwa na usumbufu mkubwa na kusababisha meli nyingi za mafuta kukwama.

Kupanda kwa Bei:
Tangu kuanza kwa mashambulizi tarehe 28 Februari 2026, bei ya mafuta ghafi (Brent) imepanda kutoka takriban $70 hadi zaidi ya $100 kwa pipa, huku wakati mwingine ikigusa hadi $170.

Uharibifu wa Miundombinu:
Mashambulizi ya anga yamelenga vituo vya kusafishia mafuta na nishati nchini Iran na nchi jirani, jambo linalopunguza uwezo wa uzalishaji duniani.

Hatua za Kimataifa:
Ili kudhibiti hali hiyo, Marekani ilitoa ruhusa ya muda ya siku 30 (Waiver) mnamo Machi 20 kuruhusu mauzo ya mafuta ya Iran yaliyokuwa tayari baharini ili kuongeza kiasi cha mafuta sokoni.

Kwa Tanzania, kama nchi inayoagiza mafuta kutoka nje, mabadiliko haya ya bei na usambazaji katika Mashariki ya Kati yanaathiri moja kwa moja gharama za uagizaji, jambo ambalo linaweza kusababisha kupanda kwa bei za ndani au foleni kwenye vituo vya mafuta ikiwa usambazaji utachelewa.
 
Madhila ya vita ya Iran na Marekani/Israel yameanza kuonekana tangu mwanzo mwa mwezi huu kwenye usafiri wa ndege

Baada ya airport za Qatar na Dubai kufungwa tickets za ndege zilipanda maradufu.. Imagine ticket ya ndege kutoka China kurudi Bongo ilipanda kutoka 2M mpaka 10M

Hii vita haina dalili na kumalizika leo wala kesho na ukosefu wa mafuta umeshaanza kushika kasi duniani .. Leo pipa moja la mafuta ghafi limefikia dola 175
Mataifa mengi yameshaanza kutoa tahadhari kwa wananchi wake kupunguza matumizi ya nishati (mafuta na gesi) sisi bado.. Lakini hatuko mbali

Lockdown ijayo si ya maradhi na barakoa na kujivukiza tena! Bali ni lockdown ya " movement limitations" kwakuwa mafuta yatapanda bei kupitiliza na yatakuwa hayapatikani kwa urahisi

Fursa fursana! Lockdown ya mafuta wakati itakapokuwa janga kwa wengine, kwingineko itakuwa ni neema na fursa ya kupiga ndefu
Jiandae ufaidike ama ujipange lockdown yaja!
Yapande mpaka tununue V8 kwa Tsh 2.5m
 
Tumsifu Trump Kristo

1774204119747.png

1774204253506.png
 
Back
Top Bottom