MamaSamia2025
JF-Expert Member
- Mar 29, 2012
- 19,294
- 39,977
Kina mama mna tatizo gani aisee? Mikopo.. mikopo.. mikopo. Kuna case kadhaa za kina mama kujiua kwa sababu ya kuzidiwa mikopo. Kuna cases za ndoa kuvunjika pia. Wanawake wengi mnakopa sana bila kufikiria mara mbili. Hali ni mbaya sana. Mitandaoni nimeona watu wengi wakilalamika kuona mama zao wana mikopo inayowazidi kiasi kwamba inabidi waingilie kati kuwanusuru.
Sababu kubwa inayowafanya wanawake kuchukua mikopo ni kuzidiwa na hisia na matamanio yao. Utakuta kaona mwenzake anafanya biashara fulani na yeye hukimbilia kuiga na kuishia kuangua kilio. Lakini sababu kubwa sana kwa sasa ni hivi VIKUNDI VYAO VYA KUKOPA NA KUWEKA wenyewe wanaita michezo. Utakuta mtu kajiingiza kwenye kikundi cha kuweka labda 10k kila siku huku hana kipato cha kutosha. Ninadhani mmeshawahi kukutana na wanawake wanaoomba walipiwe hela za mchezo.
Wachungaji na manabii wa uongo kama Tony, Mwakasege na Mwamposa pia ni sababu nyingine za wanawake kujikuta kwenye madeni. Wanawake wengi wako tayari kukopa na kwenda kumpa mchungaji wake hiyo pesa. Yaani ujinga mtupu.
Kimsingi wanawake wengi kwa sasa wanasumbuliwa na madeni. Wanateseka mno. Kina mama wengi wamekuwa mizigo kwa watoto wao kisa madeni wanayotakiwa kulipa. Waume zao pia wamekuwa wahanga wa hii mikopo. Athari ni kubwa. Ninawasihi wanawake wote mfikiri mara mbilimbili kabla ya kukimbilia kuchukua mikopo.