TUCTA: Nyongeza ya Mshahara itaanza kulipwa Mwezi August

CK Allan

JF-Expert Member
Aug 14, 2013
2,729
5,923
Barua ndio hii ngoja tusubiri! Ingawa naona dalili za mkutano kuahirishwa au ukiwepo hautakuwa na tija. Tunajua kabisa TUCTA ndio Serikali yenyewe.

IMG-20230726-WA0000.jpg


======

SHIRIKISHO LA VYAMA VYA WAFANYAKAZI TANZANIA
(TUCTA)

TARIFA KWA WAFANYAKAZI KUHUSU AHADI YA NYONGEZA YA MSHAHARA YA KILA MWAKA (ANNUAL SALARYINCREMENT)

Ndugu Waandishi wa Habari,
Ninamshukuru Mungu kwa kutukutanisha tena tangu sherehe zetu za Mei Mosi za 2023 zilizofanyika Mkoani Morogoro kitaifa na pia kwenye mkutano wa waandishi wa habari tulioufanyia kwenye chumba hiki.

Aidha, mtakumbuka katika mkutano wetu wa mwisho tulioufanyia hapa, pamoja na mambo mengine tulitoa ufafanuzi wa hoja mbalimbali zilizowasilishwa kwa Mh. Rais Daktari Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye sherehe za Mei Mosi za 2023.

Katika kipindi cha miezi taakribani mitatu tangu tarehe 1 Mei 2023, tumeona serikali imeanza kutekeleza baadhi ya ahadi ilizozitoa kwa wafanyakazi kwenye sherehe hizo kikamilifu. Kwa moyo wa dhati TUCTA tunamshukuru Mh. Rais na timu yake kwa utekelezaji huu.

Ndugu Wanahabari, katika ahadi muhimu ambayo iliahidiwa na Mh. Rais ilikuwa kwa mwaka mpya wa fedha 2023/24 kwa wafanyakazi ni pamoja na nyongeza ya Mishahara ya kila mwaka katika mishahara ya wafanyakazi kwa kuzingatia miundo ya mishahara kwa kila kada na kidato. Sisi wafanyakazi tulitarajia ahadi hiyo itatekelezwa kupitia mishahara ya mwezi Julai 2023, ambayo kwa kweli haikuwa imetekelezwa.

Kwa kuzingatia Misingi ya Utawala Bora na utamaduni wa TUCTA ikiwa ni chombo cha kuwawakilisha wafanyakazi katika majadiliano na Mwajiri Mkuu yaani Serikali, tulichukua hatua haraka kuwasiliana na Waziri wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya utumishi wa Umma na Utawaka Bora Komredi George Simbachawene na baadae kikao cha pamoja na Katibu Mkuu wake Komredi Juma Mkomi ili kupata ufafanuzi wa jambo hili.

Nichukue fursa hii kuwajulisha kuwa ni kweli Serikali ilitarajia kutekeleza ahadi hii kuanzia mwezi Julai 2023 lakini kutokana na sababu za kitaalum kulisababisha kuchelewa kutekeleza suala hili kwa mwezi huu wa saba. Serikali imeahidi kukamilisha swala hili kupitia Mishahara itakayotolewa kwa wafanyakazi mwezi Agosti 2023.

Kupitia hadhara hii niiombe serikali kutekeleza suala hili muhimu kama ambavyo imeahidi ili kuendelea kuongeza morali kwa wafanyakazi katika kufanyakazi na kutoa huduma kwa wananchi. Pia niwaombe wafanyakazi wa umma kote nchini kuwa tuendelee kuwa na subira na kuendelea kufanya kazi kwa morali na viwango vya juu.

TUCTA kikiwa chombo chenu kinacho wawakilisha wafanyakazi kwenye majadiliano na serikali kitaendelea kufuatilia utekelezaji wa jambo hili na kuwapa taarifa sahihi kadiri zinavyopatikana.

MSHIKAMANO DAIMA,
TUMAINI PETER NYAMHOKYA,
RAS WA TUCTA.
 
Wasijikite kwenye annual increment, waongelee ile 23% iliyoota mabawa dakika za majeruhi, TUKUTA bhanaa..
 
Wamepata nguvu kupitia sakata la DPW. TUCTA iliishakosa nguvu tangu awamu ile kali sasa wanajititimua baada ya haki za wafanyakazi kuporomoka
 
Back
Top Bottom