TTCL Corporation: Support thread (Maswali, ushauri na malalamiko)

TTCL Corporation: Support thread (Maswali, ushauri na malalamiko)

TTCL habari zenu Bwana!

Ninapoishi panahesabika kama mjini (ni pembezoni kabisa mwa jiji).

Nilipata mgeni, alipohitaji vocha ilifaa nimtume kijana kwa pikipiki nauli ya 2000 kununua vocha ya buku. Hawa mitandao mingine (isipokuwa Zantel) vocha nanunulia hatua nne kutoka nilikopanga.

Tukashauriana na mgeni kwa kuwa atakaa muda kidogo ni vyema aweke fedha katika T-Pesa (nadhani inaitwa hivyo) ili awe anajinunulia vocha pole pole, hii tulizunguka kabisaaa jijini tukabahatisha vendor mmoja.


Vocha tukapata, sasa mgeni kuingia mitandaoni kama hivi ikawa ni kisanga kipya. Je leo ataona hili "Jambo Lenu" vipi kama mtandao ni shida?

Nashauri embu jichangamsheni asee, vijana hawana ajira wapeni deals za kusambaza mavocha, lines, wapeni laini za uwakala kwa bei nzuri hivi.

Sent from my SM-A7000 using JamiiForums mobile app
 
Naona wamemwaga ma GB ya kutosha kweli tuna jambo letu 🌿
 
Back
Top Bottom