Traffic maeneo ya Bomang’ombe kuelekea Daraja la Kikavu wanavuna hela bila uoga

Ngongo

JF-Expert Member
Sep 20, 2008
18,933
31,178
Sasa ni wazi kila mtu anakula kulingana na urefu wa Kamba yake.

Askari wa usalama barabarani eneo la Bomang’ombe kuelekea daraja la kikavu wamekuwa wakikwapua fedha za maderava bila uoga wa aibu.

Wamekuwa wakiendeleza tabia mbovu na mbaya kama wale jamaa waliofungua Account China.

Ukifika eneo husika unasomamishwa Askari anakuonyesha speed kutoka simu yake binafsi wala hujui eneo ulipopigwa picha.

Baada ya hapo wanakuzingua uwape rushwa !.

Huu utaratibu wa kupiga toach sehemu isiyojulikana bado unaendelea ?.Askari anatumia simu yake ambayo anaweza ku edit huu ni wizi kama wizi mwingine.

WaTanzania tunapigwa mfumuko wa bei na Trafic wanatupiga sijui tutaponea wapi !.

Ni kwanini tunaendelea kuubeba huu mfumo wa kuwaneemesha trafic wakati tunaweza kutumia technology kuondokana na hizi kero za kujitakia !.
 
Wewe wape tu pesa ya shoeshine, Magufuli alishawaruhusu.

Siku ukiwa mtamu wewe simamisha gari bila kusimamishwa wape pesa ya maji halafu nenda zako utaona faida yake.
 
Hao jamaa wanabebwa na mfumo kazi kusindana kuhonga kununa magali majumba hata awaulizwa hizo mali kapata wapi

Hizo nafasi zinauzwa azipatikani bule latizama haikali atoe hongo matokeo yake wanaenda kujificha pembeni kusipo watu wanaanza kutoza ushulu matokeo ya boda noha wanakuwa jeuli wanagonga watu masikini wanawavunja viunga kuwa kujivunia sh 2000 wanzo wapa rais kila siku anawakemea bila kuwaajibisha mwisho wamemzoea wana mpuuza tu
 
Wengine wapo njia ya tpc kabla hujafika pale shule ya kiyungi. Ila wenyewe wanapambana na daladala, bajaj, noah za abiria na canter za majani
 
Kuna siku Mr alikua anatokea Arusha tunaelekea Dar. Wala hatukuwa speed, mbele tukasimamishwa. Askari bila aibu akatoa simu yake akatuonesha picha kwenye simu yake eti gari yetu ime over speed, Mr anajitahidi kumuelewesha kwamba hajatembea zaidi ya 50 kwa umbali mrefu sana kwasababu kulikua na coaster mbele yetu haitembei kabisa na upande wapili magari yalikua mengi so asingeweza ku overtake.

Askari kakomaa. Mr akamuomba ile simu aangalie vizuri, khaaa! Kumbe gari sio ile ila zinafanana. So wanabambika. Mr akamwambia sasa mbona picha yenyewe ina ukungu hata plate number haionekani? Alafu taa za gari letu kuna fog light na ile
Gari nyingine haina fog light. Hiyo ndo tofauti, Mr alimpangua kwa muonekano wa ile gari ila kama ningekua mwenyewe wangenikomalia wale wajinga!

Hizo njaa acheni. Najua mpo humu mmejazana kibao! Na mtasoma. Mna tamaa sana nyie
 
Hawa jamaa nuksi sana.
 
Wakawaida sana hao, Ila na wewe unaowajibu wa kuzingatia sheria za barabarani, vinginevyo ujiandae kwa fine na vijisent vya kuhonga!!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom